Serikali na Hatima ya ATCL

Jana/juzi press imeripoti Mattaka kasema hivi kuhusu kufungiwa kwa ATC:

Na Mwandishi Wetu
Mwananchi

"Taarifa hizo ni za uzushi, na hivi sasa niko kwenye kikao na watu wengine na si TCAA," alisema Mataka.


Leo wanaripoti:


na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima

"Kwa hiyo walibaini kuwa cheti kilichotolewa kwa ATC na ambacho muda wake ulikuwa umalizike Desemba 15, 2008, hakikuwa kimefuata taratibu. TCAA kwa hiyo iliamua kuiondolea ATC cheti hicho hadi hapo itakapokamilisha taratibu za kuwa na vielelezo vinavyokidhi masharti ya TCAA," ...alisema Mattaka

"Tunajutia usumbufu wowote uliojitokeza kwa wateja wetu na tunawaomba watuvumilie wakati tukiendelea kulishughulikia suala hili," alisema.

Hakuna hata pressman mmoja aliuyemuuliza Mattaka "sasa juzi ulikuwa unakanusha kanusha nini ?"

Au, alichokikanusha juzi sicho walichotuambia kakanusha. Yani hawakumuelewa.

Tunashindwa kujua nini kinaendelea uongozini kwa sababu hakuna wa kutuhabarisha. Na nusu ya matatizo yetu, I can almost guarantee, nusu ya matatizo yetu yangepotea kama tungekuwa na viable press. Watu wa serikali wangetia akili. The press is the weakest link, followed by parliament offcourse (parliament kazi yao wao ku rubber stamp bills za wizara ya sheria na kupigiana makofi vikaoni.)

Watu wa crummy press wanatu feed madudu na machafuchafu kushoto na kulia. You can not pick a single news piece devoid of crummy coverage. Nionyeshe taarifa, outlet yeyote ile, ambayo haijapindapinda!!
 
Jana/juzi press imeripoti Mattaka kasema hivi kuhusu kufungiwa kwa ATC:


Leo wanaripoti:



Hakuna hata pressman mmoja aliuyemuuliza "sasa juzi ulikuwa unakanusha kanusha nini ?"

Au, alichokikanusha juzi sicho walichotuambia kakanusha. Yani hawakumuelewa.

Tunashindwa kujua nini kinaendelea uongozini kwa sababu hakuna wa kutuhabarisha. Na nusu ya matatizo yetu, I can almost guarantee, nusu ya matatizo yetu yangepotea kama tungekuwa na viable press. Watu wa serikali wangetia akili. The press is the weakest link, followed by parliament offcourse (parliament kazi yao wao ku rubber stamp bills za wizara ya sheria na kupigiana makofi vikaoni.)

Wanatu feed madudu na machafuchafu watu wa crummy press. Tanzania hakuna press hata chembe. You can not pick a newspaper and read a piece devoid of crummy coverage. Not one. Hakuna kitaarifa, news outlet yeyote ile, ambacho hakijapinda pinda!!

Kuhani I agree with you. This is the challenge of our time.

Hivi unajua juzi nilikuwa najiuliza, mpaka leo tangu nianze kuangalia internet, website ya IPPMEDIA haijawahi kubadilishwa (Yaani kwa kweli waga nakuwa irritated sana nikifungua ile webpage). Features zake ni zile zile..miaka nenda miaka rudi!....Wakati ukifungua hata zile za watani wetu wa jadi unaopna kabisa mabadiliko...Uptodate za website ndo usiseme kabisa....Yaani these people arent creative at al. Not all. Hawana webmaster jamani?

Newspapers ndo kabisa...hatuna waandishi critical wakuuliza HARD QUESTIONS.

Man we have a longway to go.
 
Hakuna falsafa ya RESPONSIBILITY AND ACCOUNTABILITY to most of our leaders.
Kama MATTAKA alikuwa RESPONSIBLE kuongoza ATCL sioni kwa nini asiwe ACCOUNTABLE! Ni shurti awajibishwe kama hataki kujiwajibisha mwenyewe.
 


...I agree with you. This is the challenge of our time.

Hivi unajua juzi nilikuwa najiuliza, mpaka leo tangu nianze kuangalia internet, website ya IPPMEDIA haijawahi kubadilishwa (Yaani kwa kweli waga nakuwa irritated sana nikifungua ile webpage). Features zake ni zile zile..miaka nenda miaka rudi!....Wakati ukifungua hata zile za watani wetu wa jadi unaopna kabisa mabadiliko...Uptodate za website ndo usiseme kabisa....Yaani these people arent creative at al. Not all. Hawana webmaster jamani?

Newspapers ndo kabisa...hatuna waandishi critical wakuuliza HARD QUESTIONS.

Man we have a longway to go.

Masanja ahsante.

Ku update website ? Huko unaenda mbali mbona. That's just too technical for them to keep up with.

Website zao kuna vitu vya msingi wanavuruga. Kwenye home page huwa kuna lipicha kuubwa hapo mbele la kiongozi au somebody in the news I guess. Uki click li picha halifungui news piece yeyote. Yani wamebandika tu lipicha. Leo kuna ya Waziri Kawambwa. No news story associated with it. Pembeni kulia nako kuna vipicha vya watu kibao. Ukibonyeza hola. Sasa vipicha vya kina nani hivi? Vya nini kwenye front page?

Tukirudi kwenye mada ya hapa, kuhusu Mattaka, umesema hatuna journalists wa kuuliza hard questions. Lakini Masanja, hivi ni hard question kweli kumuuliza Mattaka kwa nini jana alikuwa anabisha kwamba ATC haijafungiwa leo anakuja kuomba wateja msamaha kwa kufungiwa ? Hiyo ni hard question kweli ?

Una lower the bar too low, Masanja, tukisema hiyo ni hard question. Yani mtu jana kabisha wamefungiwa, leo anakubali. Hata Kipepe angekumbuka kuuliza, mbona jana ulibisha?

I don't know, Masanja, we have a long way to go. I hope and pray kwamba wenyewe nao wana recognize kwamba tuna njia ndefu. Kama ma editor wao wanatambua kwamba tuna matatizo hapo tuwasamehe.
 
Waandishi wa habari huwa wanapewa bahasha ili ku-cover story. Sijui kama hii kitu bado inaendelea. Elfu tano tano au elfu kumi kumi. Sasa hapa maswali yatatoka wapi? Uulize swali gumu ukose mshiko?

Wanachoangalia ni maslahi zaidi kuliko ethics za kazi yao. Mimi naona matatizo mawili kwenye hii fani ya uandishi, kudumazwa na hali ngumu ya maisha au hawajaqualify professionally.
 
Ona sasa, ashasahau hata jana kasema nini, anazunguka tuu, kiongozi gani huyu.

Pamoja na matatizo yote ya ATCL, bado sielewi ni vigezo gani vilitumika kumpa David Matakka jukumu la kuendesha ATCL. Hana rekodi nzuri ya kazi huyu. Alisimamishwa kazi PPF kwa kashfa ya kuhujumu shirika. Yeye pamoja na huyu/hawa waliompa Mattaka uongozi wa ATCL lazima wawajibishwe.
 
Hivi wandugu nchi yetu inaelekea wapi? we seem not to have learnt anything in our failures. Bado tunapeana nafasi za muhimu kwa kuangalia undugu na urafiki. This is WRONG.

Hivi kweli tujiulize mtu kama Mataka ana record gani ya ku-run public parastatals au hata private companies? (naomba nisimuhukumu mwenye kujua aniambie)

Lakini naamini kabisa Tanzania tunahitaji mapinduzi ya kiukweli jinsi tunavyoteuana na kupeana kazi. Shirika kama AIR TANZANIA ile ndo bendera yetu ambayo ingebidi tujivunie! Lakini mpaka leo shirika limekuwa burden kuliko chochote!

I suggest the following:

1. Kujaza nafasi nyeti kama za ukurugenzi wa mashirika muhimu (na mengineyo) kazi tuzitangaze GLOBALLY kwenye magazeti kama economist, guardian na mengineyo. Wenye sifa kutoka pande zote za dunia watume maombi. After all hii itasaidia hata kuwapata watanzania waliobobea katika management ya makampuni makubwa huko nje na ndani. Tukishampata tunayemtaka tunampa job discription na malengo tunayotaka ayatimize. Na Masharti ni kwamba mkataba utaongezwa kwa perfomance na delivery! after every ONE year.

2. TUPUNGUZE POLITICS!! kwenye shughuli nyeti kama hizi. Hebu angalia Management ya KQ ni wazawa na wageni (they complement each other). Jamani tunahitaji kujifunza. Kama tumekumbatia globalization, matakwa yake ndo hayo-let those who can deliver do the job.

3. Raisi ajitoe kufanya appointment kama hizi za maswala ya kiuchumi. Adeal na politics mengine awaachie wataalamu wake. Jamani iweje mkuu wa nchi afanye almost uteuzi wa kila kitu?

4. AIR TANZANIA inahitaji management mpya ya wazawa na wale wa nje. Ni shirika linaloweza kujiendesha kwa faida kabisa. Lakini people are obsessed with corruption and incompetence. Tangazeni nafasi hizo watu watume vyeti..tuache porojo. Tupeane kazi kwa kuangalia vyeti na utendaji wa mtu.

5. Mataka should just give way to another person.

It doesnt matter who runs the organization/company hata kama mtu anatoka El Salvador or Fiji...As long as He/She can deliver thats all we want!

Nimeuliza weeeee hilo swali kwa karibu miaka 15 sasa sijapata jibu
 
Ona sasa, ashasahau hata jana kasema nini, anazunguka tuu, kiongozi gani huyu.

Pamoja na matatizo yote ya ATCL, bado sielewi ni vigezo gani vilitumika kumpa David Matakka jukumu la kuendesha ATCL. Hana rekodi nzuri ya kazi huyu. Alisimamishwa kazi PPF kwa kashfa ya kuhujumu shirika, huyu/hawa waliompa Mattaka uongozi wa ATCL inabidi wawajibishwe.

Hawa watu wangekuwa wanafanyiwa confirmation hearing kabla hawajapitishwa. Kwenye confirmation hearing huwa machafuchafu yote ya nyuma yanaibuka. Rais anapeleka jina, wabunge kwenye kamati wanachambua wanapiga kura kama wanamwona anafaa au hafai. Vinginevyo ndo unachagua mtu Waziri wa mambo ya ndani unakuja kuta kakwepa National Service au kafilisi PPF huko in his past life halafu kawa reincarnated kapewa ATC. Duuuh!
 
mkuu kuhani ni kweli vyema kupeleka majina kwa wabunge wakafanya hivyo ila ujue hata wabunge nao ni binadamu,,kama jana waandishi wa habari nasikia walijazana kama njugu hapo mjini office za atc,,na wakapewa jumla ya million 2 kuandika kwenye gazeti unafikiri kuna jipya lolote...
swala hapa ni kumwomba mungu hata atakaechagliwa awe ana hofu ya mungu
 
mkuu BULESI usidanganye umma,kwanza naomba utoe samahani kwa maneno yako hapo juu....leo hii na jana tumesoma kwenye gazeti sababu za kufungiwa ATCL si mtaji kama unavyosema ATCL isipooongezewa mtaji na serikali hawatorudishiwa kibali cha kuruka,,pili walichonyanganywa si licence ya kuruka,,tatu soma NIPASHE/MAJIRA utaona ni UZEMBE WA VIONGOZI LIOKUWA NAO BWANA MATTAKA NA HATA KUKIRI KWAMMBA NI UZEMBE WA UFANISI..WA KUTOPELEKWA DOCS KWA MUDA UNAOFAA!!!!HIVYO SERIKALI HATA IWEKE BILLION 200 KAMA WATU WAMEKAA KATIKA MIAJILI YA AKULA NA TUSHIBE LINI!!!!
HAKUNA SHRIKA LITAKALOKUWEPO...TATIZO LILILOKUWEPO KATIKA UONGOZI WA NCHII HII NI UADILIFU HASA PALE PANAPOONGELEWA MASWALA YA MASILAHI...WENGI WANAKUWA WAGUMU KUTENDA KAZI INAVYOTAKIWA NA HIVYO KUISHIA KUKIMBILIA ASILIMIA KUMI(10%)...HATA HAPO NYUMA NILIPOKUWA ATC KILA MTU ANAANGALIA ASIIMIA KUMI...HADI WALE WA STORE ...KARATASI BUNDA 3000 WANANDIKA 5000
NA KWA KUKUAKISHIA TU ,KAMA WATAANZA KUCHUNGUZA UKWELI HALISI PESA ZINATOKEA WAPI WATU WATAKIMBIA OFISI WENYEWE,,MUNGU AENDELEE KUMLINDA MZEE WETU MMOJA ALIKUWA DIR ...KIMARO...TUKIWA NA NDEGE MOJA TU AINA YA BOEING WAFANYAKAZI WOTE WALIKUWA WANALIPWA MSHAHARA KAMA KAWAIDA..NA RUTI MWANZA PEKEE....TUNAITAJI VIONGOZI WAADILIFU KAMA HAWA WANAOJALI MASLAHI YA TAIFA NA SI MASILAHI BINAFSI...SIJUI YUKO WAPI MUDA HUU...HAKIKA AKUNA AMBAE ATAMSAHAU PAMOJA NA WAKINA SANARE!!!!!!
 
Huyu jamaa inabidi aachie ngazi... vinginevyo tutarudi kwenye mashirika ya ugavi watu wanatafuna wanapewa kwingine. Jamaa si alikuwa Bima huyu sasa si aliharibu kule hata shirika liko hoi then now bado wanamchelewesha!! Au kuna kamchezo kama kale kaTANESCO shirika life mashirika fulani ya ndege yapete?

Nguvu za ushikaji zinaanza kukwama lakini JK anaamini kwamba nguvu hizo bado zina nguvu , na kama haamini ngojeni mtaona .
 
Hawa watu wangekuwa wanafanyiwa confirmation hearing kabla hawajapitishwa. Kwenye confirmation hearing huwa machafuchafu yote ya nyuma yanaibuka. Rais anapeleka jina, wabunge kwenye kamati wanachambua wanapiga kura kama wanamwona anafaa au hafai. Vinginevyo ndo unachagua mtu Waziri wa mambo ya ndani unakuja kuta kakwepa National Service au kafilisi PPF huko in his past life halafu kawa reincarnated kapewa ATC. Duuuh!

Hakuna confirmation hearing, na hivi, hata hiyo Board of Directors kazi yao nini? Hawawi involved na recommendations za maamuzi kama haya ? Au Rais yeye ana bypass tu, executive decision manake.

Kwa vile Rais anajua rekodi ya Mattaka (siwezi amini hajui,) anachotueleza hapa ni kuwa, hata kama umeharibu sehemu moja, all you need to do is make nice na Mr. President, then, you are set! Disgusting!
 
Watumishi wa shirika la ndege la ATCL katika mkutano wao uliofanyika leo, wametoa tamko la kumtaka Mkurugenzi wa ATCL DAvid Mattaka ajiuzulu pamoja na menejimenti nzima. Mkutano huo umefanyika siku moja baada ya Mkurugenzi Mattaka na wenzake kutoa kauli yao hapo jana.
 
Kwa nini wanamshinikiza Mattaka ajiuzulu, wakati ameshakataa kwa sababu anazozijua yeye?

Kwa nini wasimuambie boss wa Mattaka kwamba wanataka boss mwingine huyo hawezi kazi?
 
Date::12/12/2008
ATCL yakiri uzembe

matakaa.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, David Mattaka

WAZIRI SEMA ILISTAHILI ADHABU

Na Boniface Meena na Peter Edson

SHIRIKA la Ndege (ATCL) limekiri kuwa licha ya kukaguliwa na kitengo cha ukaguzi cha Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga (IOSA) tangu Desemba mwaka jana, lilishindwa kukidhi utashi wa viwango vipya vya usafiri huo na kusababisha linyang'anywe cheti cha kuendesha shughuli zake na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Kutokana na kunyang'anywa cheti hicho kinachoitwa AOC (Air Operations Certificate), shirika hilo limesema litakuwa likikosa karibu Sh300 milioni kwa wiki katika kipindi ambacho litakuwa halifanyi safari za anga kusubiri TCAA kufanyia kazi nyaraka zilizowasilishwa na ATCL juzi.

ATCL imezuiwa kufanya safari za anga baada ya TCAA kuinyang'anya cheti cha usafiri huo tangu Desemba 8 baada ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) kukagua shughuli za TCAA Novemba mwaka huu na kubaini nyaraka za ATCL zilizokuwa kwenye mamlaka hiyo ya Tanzania hazikuwa zikiendana hata na sheria za TCAA za mwaka 2006 na hivyo kushauri linyanyang'anywe cheti hicho kwa muda usiojulikana.

Ukaguzi huo wa ICAO umekuja baada ya IOSA kufanya ukaguzi mwingine Desemba mwaka 2007 na kubaini jumla ya dosari 482 ambazo hazikufanyiwa kazi na ATCL hadi ukaguzi mwingine ulipofanyika mwezi uliopita.

"Novemba mwaka 2008, ICAO ilikuja nchini kukagua jinsi TCAA inavyofanya shughuli zilizo chini yake za kuangalia mashirika ya ndege yanayofanya kazi nchini," alisema mkurugenzi mkuu wa ATCL, David Mattaka katika mkutano wake na waandishi wa habari jana.

"Katika kufanya hivyo, (ICAO) walibaini kuwa zile nyaraka za kiutaratibu ambazo zilikuwa TCAA, hazikulingana na sheria za TCAA za mwaka 2006. Nyaraka hizo ndio zile ambazo zilikuwa zikiandikwa upya ili ziendane na sheria mpya," aliongeza Mattaka.

"Kwa maana hiyo, walibaini kuwa cheti cha AOC kilichokabidhiwa kwa ATCL na ambacho muda wake ulitakiwa kuisha Desemba 15, 2008, hakikutolewa kwa kufuata utaratibu. Kwa hiyo, TCAA iliamua kunyang'anya AOC hadi hapo ATCL itakapokamilisha nyaraka na kukidhi utashi wa TCAA."

Akijibu swali juu ya sababu zilizoifanya ATCL ishindwe kukamilisha utashi wa viwango vya usafiri wa anga tangu Desemba mwaka 2007 wakati IOSA ilipobaini mapungufu hayo 482, Mattaka alisema hiyo ilitokana na kampuni walizoziteua kuwashauri kiufundi kutoka nje ya kushindwa kukamilisha kazi yao hadi siku ya mwisho ya muda ambao TCAA iliwapa ATC ambayo ilikuwa juzi.

Hata hivyo, Mattaka alisema tayari shirika lake limeshakamilisha nyaraka hizo na kuziwasilisha TCAA, ambayo imeahidi kwa maneno kuwa inahitaji siku kumi za kazi ili iweze kuzishughulikia na kuirudishia ATCL cheti hicho cha usafiri wa anga.

Shirika hilo limekuwa taaban tangu ndoa yake na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) ivunjike, likiwa linashindwa kusafirisha wateja wake mara kwa mara, kukataliwa kujaza mafuta wakati ikiwa nje kutokana na kudaiwa na kampuni ya mafuta ya BP na kupungukiwa na ndege kutoka tano hadi mbili baada ya tatu kuharibika.

Akifafanua matatizo hayo, Mattaka alisema katika dosari 482 ambazo IOSA ilibaini, 39 zilikuwa katika muundo na menejimenti, dosari 206 zikiwa katika safari, huku dosari 55 zikiwa katika huduma ya mizigo.

Alitaja dosari nyingine kuwa katika maeneo ya matengenezo (45), wahudumu (7), huduma baada ya kutua (50), utumaji mizogo (44), na usalama wa uendeshaji ambao ulikutwa na dosari 36.

Mattaka alisema kutokana na matakwa ya TCAA tayari ATCL imeshafanyia kazi nyaraka hizo na kuziwasilisha TCAA tangu juzi na inasubiri ahadi ya mamlaka hiyo kuzishughulikia katika muda wa siku kumi za kazi.

"Tungependa kusisitiza kuwa matatizo katika nyaraka hayahusiani na usalama wa safari za ndege na wasafiri hawajawahi kuwa hatarini kutokana na matatizo (hayo ya nyaraka)," alisema Mattaka, ambaye alikuwa mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Pensheni ya Mashirika ya Umma (PPF).

Kuhusu ahadi ya kuisaidia ATCL iondokane na mzigo wa matatizo hayo, Mattaka alisema serikali ina nia ya kulisaidia shirika hilo kwa dhati, lakini ili kuisaidia ni lazima itumie kodi za wananchi au kutafuta mwekezaji.

Alisema kuna kampuni ya Kichina ambayo inataka kulichukua shirika hilo na mazungumzo na serikali yanaendelea.

Mattaka alisema gharama za uendeshaji mashirika ya ndege ziko juu sana, akitoa mfano wa uendeshaji wa ndege aina ya Airbus kutoka Dar kwenda Mwanza na kurudi inagharimu kiasi cha Sh9 milioni wakati kurusha ndege aina ya Boieng hugharimu Sh10 milioni.

'Tunashukuru bei ya mafuta imepungua na gharama pia zimepungua," alisema Mattaka.

Wakati shirika hilo likiingia katika hasara hiyo, wateja wake ambao walikuwa wamekata tiketi kwa ajili ya safari kuelekea maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi kabla ya ATCL kusimamishwa watarudishiwa fedha zao ili waweze kutafuta usafiri mwingine.

Naye Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa alisema ATCL ilistahili adhabu hiyo ya kunyang'anywa cheti cha usafiri wa anga kutokana na kukiuka baadhi ya vipengele vya sheria.

Alisema kwa kawaida masuala yote ya anga yanasimamiwa na Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga (IATA) na kwamba baada ya chombo hicho kufanya ukaguzi, kilibaini makosa ya kiufundi yanaweza kusababisha athari, lakini wao ATCL hawayashughulikia.

Lakini alisema serikali imeshaingilia kati suala hilo na kwamba kuna baadhi ya marekebisho yanafanywa ili kulinusuru liweze kurudi katika hali yake ya kawaida.

Alisema pamoja na marekebisho hayo pia serikali ipo kwenye mchakato wa maongezi na muwekezaji mpya ambaye ameonyesha nia ya kuwekeza katika shirika hilo.
 
Hawa watu wangekuwa wanafanyiwa confirmation hearing kabla hawajapitishwa. Kwenye confirmation hearing huwa machafuchafu yote ya nyuma yanaibuka. Rais anapeleka jina, wabunge kwenye kamati wanachambua wanapiga kura kama wanamwona anafaa au hafai. Vinginevyo ndo unachagua mtu Waziri wa mambo ya ndani unakuja kuta kakwepa National Service au kafilisi PPF huko in his past life halafu kawa reincarnated kapewa ATC. Duuuh!

Unayosema ni sawa kweli tupu Kuhani. Utaratibu wa Rais kuendelea kuteua Wakurugenzi na Mameneja wakuu umepitwa na wakati. Kazi hizi sasa hivi ni lazima zitangazwe hadharani na kila mwenye sifa zinazostahili atume maombi yake na Board of Directors ambazo zina wajumbe imara ziachwe zichuuje majina hayo na hatimaye kumpaya yule wanayemuona anastahili kupewa wadhifa huo kutokana na vigezi vitakavyowekwa.

Board of Directors nazo zimejaa watu ambao hawastahili kuwa wajumbe katika board hizo maana hawajui lolote na huwa wanachapa usingizi tu na kusubiri sitiing allowance zao.
 
Tumeyazoea ayo,MBEYA wiki 2 wamekaa giza na hakuna aliyejiuzulu while kuna makampuni daily wanapata hasara ya mill 200 SEMBUSE IZO 300 ZA TTCL.
TZ lini tutakuwa serious jamani.....................................
Lets embrace the spirit of professionalism by resigning waje wengine,ni ustaarabu wa kawaida
 
ATC yanusa kifo

• Mattaka akataa wazo la kutakiwa ajiuzulu

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATC), limesema litapata hasara ya sh milioni 300 kila wiki kutokana na kusimamishwa kwa huduma za ndege zake.

Hatua hiyo imefufua maumivu kwa shirika hilo ambalo limekuwa katika jitihada za kuboresha huduma zake baada ya kukabiliwa na matatizo ya kifedha ambayo yalilikumba wakati na baada ya kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA).

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, David Mattaka, alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya sababu zilizofanya shirika hilo lifungiwe kurusha ndege zake kwa kushindwa kutimiza masharti 482 ya usalama wa anga.

Mkurugenzi huyo alisema kusitishwa kwa huduma ya ndege za ATC, kunatokana na Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) kusimamisha huduma za shirika hilo baada ya ukaguzi uliofanywa na Jumuia ya Kimataifa ya Usalama wa Anga (IOSA) kupitia Kitengo chake cha ukaguzi wa usalama (AYATA), kubaini kuwa TCAA haikufuata taratibu katika kutoa cheti cha kurusha ndege kwa shirika hilo.

Mattaka alisema, ukaguzi huo uliofanywa Desemba, mwaka jana (2007), ulibaini kuwepo dosari 482 katika maeneo ya operesheni yaliyo chini ya TCAA.

Kwa mujibu wa Mattaka, dosari 39 zilibainika katika eneo la oganaizesheni na usimamizi, uongozaji wa ndege, dosari 206, matengenezo dosari 45, sehemu ya mizigo, dosari 44, ulinzi, dosari 36, kitengo cha utoaji, dosari 55, na uwanjani dosari 50.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, Novemba mwaka huu, Shirika la Kimataifa Linalojishughulisha na Usalama wa Anga Duniani (ICAO), lilikuja kuifanyia ukaguzi TCAA kuhusiana na jinsi inavyosimamia mashirika ya ndege yanayofanya kazi nchini na kubaini kuwa vielelezo vya mashirika ya ndege vilivyokuwa TCAA, havikidhi masharti kwa mujibu wa taratibu zinazoongoza TCAA za mwaka 2006.

“Kwa hiyo walibaini kuwa cheti kilichotolewa kwa ATC na ambacho muda wake ulikuwa umalizike Desemba 15, 2008, hakikuwa kimefuata taratibu. TCAA kwa hiyo iliamua kuiondolea ATC cheti hicho hadi hapo itakapokamilisha taratibu za kuwa na vielelezo vinavyokidhi masharti ya TCAA,” alisema Mattaka.

Alisema kwa bahati nzuri, ATC iliweza kuwasilisha vielelezo vyote vilivyohitajiwa Desemba 10, 2008, na sasa shirika hilo linaisubiri TCAA ijiridhishe na vielelezo hivyo na kulirejeshea cheti ili liendelee kurusha ndege zake.

Kwa mujibu wa Mattaka, TCCA inatarajia kutumia takribani siku 10 kupitia nyaraka hizo za ATC na kurejesha huduma zake.

Alisisitiza kuwa mapungufu yaliyojitokeza ya kutokuwepo kwa vielelezo hivyo, hayana uhusiano wowote na suala la usalama wa ndege zake na hakuna kipindi ambacho wateja wake walikuwa katika hatari, kwa sababu ya ubovu wa ndege zake.

“Tunajutia usumbufu wowote uliojitokeza kwa wateja wetu na tunawaomba watuvumilie wakati tukiendelea kulishughulikia suala hili,” alisema.

Mattaka alisema hivi sasa shirika lake linarejesha nauli kwa abiria waliokata tiketi za kusafiri na ndege za shirika hilo katika siku za hivi karibuni, lakini waliomba kusafiri kwa tarehe za mbali, wataendelea kubaki nazo kwani wanaamini baada ya siku 10 kuanzia jana, watarejesha huduma zao.

Alipoulizwa kama yuko tayari kujiuzulu kutokana na kushindwa kuliendesha shirika hilo tangu alipokabidhiwa, Mattaka alisema hafikirii kufanya hivyo kwani anaamini bado anaweza na kutoa wito kwa serikali kuendelea kulisaidia shirika hilo linalochungulia kaburi.

Wakati Mattaka akitoa ufafanuzi huo, Waziri wa Miundombinu,Dk. Shukuru Kawambwa, alisema ATC imesimamishwa kutoa huduma kwa kutokidhi vigezo vya kimataifa vya usalama wa anga.

Alisema kufungiwa kwa shirika hilo hakutokani na ubovu wa ndege zake kama inavyofikiria na wengi bali kutokana na dosari zilizojitokeza wakati wa ukaguzi.

“Wamesimamishwa kwa muda tu na tatizo si mwekezaji, bali kutofuata utaratibu uliopangwa na IATA,” alisema Dk. Kawambwa.

ATC ni shirika pekee la ndege la umma na hadi Mei mwaka huu, lilikuwa na ndege sita, tatu ikiwa inazimiliki na nyingine za kukodi.

Hivi karibuni Kamati ya Miundombinu ya Bunge, ilisema kuwa kulikuwa na mpango wa shirika hilo la ndege kuingia ubia na shirika moja la ndege la China.
Ajiuzulu ale wapi?
 
Back
Top Bottom