share
JF-Expert Member
- Nov 22, 2008
- 6,062
- 10,461
Awali ya yote mwandishi awatendee haki baadhi ya wajumbe wa kamati ambao hawakutambulishwa kwa jamii kwa hadhi zao kitaaluma. Ninavyofahamu mimi Marcelina Chijoriga na Mussa Assad ni ma-Dk. pia waliobobea kwenye fani za biashara na uhasibu. Kwanini wengine mf. Dk. Ibrahim Juma, Dk. Gideon Kaunda, na Dk. Hamis Kibola wametambulishwa kwa U-Dk na wengine siyo? Anyway, hilo ni jambo dogo lakini lina umuhimu wake katika uchambuzi wa mambo ili kujua uzito na uwezo wa wanatume dhidi ya kazi waliyopewa na waziri. Pili, tunaomba kamati iliyoteuliwa itutendee haki watanzania. Watumie taaluma zao, busara zao na uzalendo wao kutupatia ripoti yenye mshiko itakayomfanya waziri na wizara husika kufikia maamuzi ya maana kwa shirika letu la ndege. Matatizo ya shirika hili yamepigiwa mayowe mwaka mzima kabla ya huduma zake kufungwa rasmi mwishoni mwa mwaka jana. Menejimenti iliyopo iliyajua matatizo hao yaliyokuwa yanapigiwa makelele lakini hatukuona dalili zozote za jitihada za makusudi za kulinusuru shirika hili zaidi ya ufisadi wa kununua mashangingi zaidi kwa mkopo wa Stanbic bank ili menejimenti iendelee kutanua mtaani huku shirika linadidimia polepole. Tume iliyoundwa itutendee haki. Isimfumbie macho kiongozi yeyote katika menejimenti. Ituletee ripoti iliyoenda shule. Tunatumaini wao wana tume wameenda shule, tunatarajia ripoti iliyoenda shule kama ile ya Dk. Mwakyembe. Imefika wakati tuiokoe nchi yetu badala ya kulindana kijinga. Tutatungulize uzalendo kwa taifa na maendeleo yake.