Ndugu zangu wana JF, yaelekea tunashangaa sana yaliyojiri bungeni jana. Kwa wana demokrasia yameamsha hasira tena, lakini ndio hali ya nchi hii. Hebu tujikumbushe:
1. Ili kukwepa Mrema Lyatonga asigombee Urais kupitia CCM mwaka 1995, CCM iliweka vigezo kwa mgombea wao kuwa na digrii moja. Lyatonga akalazimika kuingia upinzani.
2. Mwaka 2000 CCM waliondoa kipengele hicho ili kumwezesha Aman Karume kugombea urais wa Zanzibar maana hakuwa na digrii.
3. Mwaka 2006 Hamad Rashid wa CUF alishinikiza kuwepo neno 'kambi rasmi ya upinzani bungeni' ili CUF ipate fursa ya kuongoza kamati tatu muhimu. Alidhani na kuamini kwamba CUF itakuwa kambi ya upinzani daima kwa sababu ya wabunge toka Pemba. Safari hii mambo yamegeuka si CUF tena, ni CHADEMA kilicho chama cha upinzani Bungeni. Kuona hivyo Hamad huyo huyo, amekula njama na swahiba zake CCM wanabadili kanuni ili Chadema kikose haki ya msingi kuisimamia serikali. Na kwa sababu ya ule mwafaka za Zenji, jamaa wamekubali.
So, hii ndio CCM na serikali yake ni vigeugeu kila wakati. Litakalofuata ni hili, siku Chadema ikishinda kwa asilimia 45 na CCM wakapata 41, basi CCM wataungana na vyma vingine ili kuweka kanuni ya Chama kinachoshinda kulazimika kufikisha asilimia 50. Watafuta kanuni za sasa na kuweka zingine ili uchaguzi urudiwe. Hapa kinachotangulizwa si maslahi ya taifa bali ya wao na wapambe wao.