Serikali kutaifisha shule Binafsi

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
ni muhimu kwa sasa serikali kutaifisha shule hizi binafsi ambazo zimejaa na kuota kama uyoga,Shule hizi ndizo zinazo sababisha matatizo kwa shule zingine za serikali, wewe unaonaje ??
 
mbona husomeki? weka mambo wazi tuelewe unamaanisha nini? naona bado una mawengemawenge ya usingizi mkuu
 
Vipi zile za kata, ubora wake ukoje? Au ndio kutapatapa kwa serikali yetu bila kujitambua? Labda wafanye exchange kwa kuchukua za binafsi alafu binafsi wachukue za kata wawasaidie kuboresha?
 
Uwepo wa shule za binafsi zinaleta changamoto sana kwenye upande wa perfomance kwa wanafunzi, hivyo zinaleta ushindani mzuri sana, mi nadani serikali iziache tu ziendelee kutoa huduma.
 
ni muhimu kwa sasa serikali kutaifisha shule hizi binafsi ambazo zimejaa na kuota kama uyoga,Shule hizi ndizo zinazo sababisha matatizo kwa shule zingine za serikali, wewe unaonaje ??
mie naona wewe ni mwehu,umekosa cha kuongea.
 
hapo kwenye red, hebu tuambie shule binafsi zinasababishaje matatizo kwa shule za serikali na matatizo yepi?

mwisho kabisa tatizo halisuluhishwi kwa kukimbia tatizo......

kwa nchi yenye utajiri na maliasili kama tanzania wanafunzi hawapaswi kusoma chini ya mti, au shule kukosa hata maabara.........

ni muhimu kwa sasa serikali kutaifisha shule hizi binafsi ambazo zimejaa na kuota kama uyoga,Shule hizi ndizo zinazo sababisha matatizo kwa shule zingine za serikali, wewe unaonaje ??
 
yaani mijitu imejikalia tu bila kufanya kazi inasubiri madodo yadondoke chini , kweli hii ni laana..
 
ni muhimu kwa sasa serikali kutaifisha shule hizi binafsi ambazo zimejaa na kuota kama uyoga,Shule hizi ndizo zinazo sababisha matatizo kwa shule zingine za serikali, wewe unaonaje ??

Kwa vipi zinasababisha matatizo kwa shule za serikali. usitoe sweeping statements!!!!
 
Serikali yenyewe imeshindwa kuziendesha shule zake na sasa wamezifanya kuwa viwanda vya kuzalisha wajinga. Wakichukua za binafsi ndiyo wataweza kuziendesha? Labda kama lengo ni kuleta usawa wa ujinga kwa watanzania wote!
 
ni muhimu kwa sasa serikali kutaifisha shule hizi binafsi ambazo zimejaa na kuota kama uyoga,Shule hizi ndizo zinazo sababisha matatizo kwa shule zingine za serikali, wewe unaonaje ??

Wazo ni zuri kabisa na hii itatusaidia sana kushuka kwa ghalama za kusomesha watoto zetu. Isue iko kwenye utekelezaji wa hilo suala kwani hao hao viongozi wa serikalini nao wanamiliki hizo shule na ndio hupandisha sana ada kwa visingizio eti ni english media, matokeo yake mtoto anamaliza shule na anachoambulia ni kuzungumza kingereza tu.
 
ni muhimu kwa sasa serikali kutaifisha shule hizi binafsi ambazo zimejaa na kuota kama uyoga,Shule hizi ndizo zinazo sababisha matatizo kwa shule zingine za serikali, wewe unaonaje ??
Sioni umuhimu na wala sioni sababu ya kutaifisha. Naona sababu ya kurejesha shule ambazo ilizitaifisha miaka ya nyuma.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom