Serikali Kushindana na JF?

Wanatafuta channel za kujisafisha, hawana jipya na watapewa comment huko mpaka watakimbia wenyewe,
 
Watavumilia madongo against serikali? Naona Mwanakijiji keshaanza kuwachokoza kuhusu Kiwira/Mkapa.

Mbona nimeona Makala ya Mwanakijiji kuhusu Mkapa, Yona wanyanganywe Kiwira Coal Mine imekatwa had robo au Mwanakijiji ndiyo alivyotaka itoke? Mwanakijiji tuhabarishe! Wameshindwa kuvumilia nini?

Mzee Mwanakijiji

Joined: 27 Nov 2007
Posts: 1
Location: Kijijini
Posted: Tue Nov 27, 2007 5:53 am Post subject: Mkapa, Yona; Wanyang'anywe Kiwira?

--------------------------------------------------------------------------------

Wakiwa madarakani Rais Benjamini Mkapa na Waziri wake wa Nishati na Madini waliingia ubia na kuanzisha kampuni ya Tanpower Resources. Wakati Yona analiambia Bunge kuwa wanatafuta wawekezaji wa "kufufua" Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira, sirini walikuwa wanapanga yeye na Rais wake kuwa "wawekezaji" hao watakuwa ni wao wawili. Na miezi michache kabla Rais Mkapa hajaachia madaraka, Mgodi wa Kiwira ulikuwa chini ya viongozi hao wawili wakiwa na hisa zaidi ya asilimia 80. Hadi leo hii hakuna aliye tayari kueleza ni jinsi gani viongozi hao wawili waliweza kusimamia uuzwaji wa Kiwira wakati wao wenyewe wakiwa ndio wanunuzi wakubwa. Kabla watu hawajashangaa maajabu hayo ya "Musa" wakajikuta wanashuhudia serikali ya awamu ya nne ikiingiza Tanesco kwenye mkataba na kampuni ya kina Mkapa na Yona ambao waweza kuligharimu taifa zaidi ya shilingi bilioni 300. Binafsi naona inatosha kuoneana aibu; Rais Mkapa na Yona Wanyang'anywe mgodi huo ambao walijipatia kwa kutumia madaraka yao vibaya.

Tatizo ni kuwa nani, atamfunga paka kengele? Au tuwaachie tu waendelee kugawa na kugawana hazina za Watanzania?
_________________
Hoja hujibiwa kwa Hoja!.. wenye kushindwa hoja, huleta vioja!
Source: http://forum.dailynews.habarileo.co.tz/viewtopic.php?t=6
 
Nimetumia computer ya kazini kujaribu kupitia hii forum ya daily news. Jamaa hapa wanasystem kali sana ambayo huwa si tu inablock virus toka nje, bali pia ina uwezo wa kusoma system ya attackers.

Nilivyofungua some staff kwenye hiyo forum, nimepata warning kuwa kuna cookiez ambazo ziko set up kwenye hiyo website ili kutrack some information.

Bado sijui kama wamefanya on purpose au ni vile original script ya hiyo forum iliandikwa. Kwa wale ambao wanataka kujiunga nawapa tahadhari tu kuwa makini. Unaweza kujiunga moja kwa moja na kuwa muwazi kama Kitila na Mwanakijiji walivyofanya.

Ila kwa wale mulioko Tz na ambao munapenda kuficha majina yenu na kazi zenu kwa sasa, inabidi muwe makini kidogo. Hata hivyo, kwa wale watakaopenda kujiunga huko nadhani huu ni wakati mzuri wa kwenda kugive hell some guys huko.

Mimi nitakaa na JF maana ndiyo forum pekee so far ninaiamini kwa protection ya ID za membaz wake.

Thanks
 
Naona hapa sasa MFK ametukumbusha kitu na huenda hata aliyeleta hiyo site yao huku alitaka kutupa taarifa ili tuanze kujiunga huko na baada ya muda waweze kujua nani huwa anawashambulia kwenye forum zingine na haswa JF hivyo kuweni macho kwa RA anaweza akawa ndio katoa sponsorship ya hiyo kitu ili kuweza kujua wabaya wake na kuwasulubu.
 
Binafsi nimegundua moja, siingii kwenye forum yao kutoka kompyuta yoyote ya hapa kwenye kibanda changu au ya kwenye shamba la kijiji. Nikitaka kuingia kule kwao naenda kwa jirani (i mean kijiji cha Jirani) so wataniona naingia mara moja moja tu..
 
Kwani sisi tuna cha kuficha? Katika yote tunayoyaandika ni lipi hasa la kututia hatiani. kama tunaamini tunayoyasema tutakuwa tayari kuyasimamia iwe ni hapa, huko Daily News au popote. The problem with anonymity is that it reduces accountability and responsibility for what you say, which I personally find it disturbing. So, dont be afraid of somebody tracing your information so long as you trust and you are ready to stand for whatever you say. Just a piece of advice.
 
ni ushauri mzuri, kwani wakati wa sisi wengine nasi kuweka majina yetu hadharani ukifika tutafanya hivyo ili kusiwe shaka yoyote kuwa tunawahofia.. for now, angalau hoja hazigeuzi kutushambulia watoa hoja; Ndio maana majibu yao wakati mwingine kwetu inakuwa vigumu kuya spin kisiasa au kibinafsi..
 
Kwani sisi tuna cha kuficha? Katika yote tunayoyaandika ni lipi hasa la kututia hatiani. kama tunaamini tunayoyasema tutakuwa tayari kuyasimamia iwe ni hapa, huko Daily News au popote. The problem with anonymity is that it reduces accountability and responsibility for what you say, which I personally find it disturbing. So, dont be afraid of somebody tracing your information so long as you trust and you are ready to stand for whatever you say. Just a piece of advice.

Mkuu Kitila,

Unachosema ni kweli kabisa na ndio maana nimesema kuwa kwa wale wasioona tatizo kuficha ID zao kama wewe ni vizuri wakaingia huko bila tatizo lolote.

Ila kwa wale walioko serikalini au kwenye ajira ambazo wanoko wa serikali wanaweza kuwafanya vibaya, nimewapa tahadhari tu kuwa waingie hiyo forum ya daily news kwa uangalifu mkubwa.

Usiri muda mwingine ni mzuri sana hasa katika mambo ya siasa. Hapa US kuna kiongozi mmoja mkubwa tu wa serikali alikuwa akitoa siri za serikali kwa waandishi akitumia jina la "deep throat"

Siri za deep throat zilipelekea Rais wa nchi Richard Nixon akajiuzulu kutokana na mambo ambayo deep throat aliyatoa kwa jamaa wa washington Post.

Nakuhakikishia kuwa kama deep throat angetumia jina lake la halali, Nixon angemshukia kama 18 wheelers na jamaa asingeacha urais wala nini.

Kuficha ID kwa ajili ya kutoa info kama jamaa wengi wanavyofanya hapa ni kitu kizuri sana.

Thanks!
 
Vizuri sana bi mdogo, kuna wengine tunaaminiwa kutoa info mbalimbali kwa sababu ya kutotumia majina yetu na nadhani hilo ni jambo zuri. Siyo kwamba hatufahamiki bali hatuko tayari kufahamika hadharani namna hiyo. Tuendelee kukata issues..
 
Hivi kuna mtu humu anayedhani jina lake halijulikani na watu...? Basi tu watu wanakuwa wastaarabu kwa sababu hakuna cha ku-gain lakini si kwamba watu hatujuani humu. Labda mtu uwe unaishi kwenye kisiwa peke yako lakini kama unaishi na jumuia ya Watanzania wengine jua kwamba unajulikana na kutolitangaza jina lako hadharani ni staha tu
 
Hiyo ni kweli kabisa Nyani ukichukulia hizi babikiu za kila weekend! watu tunafamiaana siku hadi siku ila kutokana na hii heshima ya JF watu wanatumia staha uliyosema.

Hiyo heshima huko daily news haitakuwepo. Ukiwashika wazee kwenye koo watakimbilia kukutaja majina yako na wazazi wako na ya wadogo zako na kila mtu wanayemjua na kisha watakuanzishia gharika personal ambazo hazitaisha.

Unakumbuka majibu ya Lowasa kwa Mwanakijiji? Alikimbilia kutaka kumjua Mwanakijiji ni nani na akataka ID yake iweke wazi? Huko watu wakishindwa hoja wanaanza personal atttacks - nadhani email za uongo dhidi ya Slaa na Mbowe zilivyosambazwa na wanaccm ni ushahidi tosha of what those guys wanafanya.

Ndio maana mi nimesema kuwa sitoenda huko na nitabaki hapa JF maana so far naona heshima ya ID za watu hapa iko juu sana na inalindwa kwa nguvu kubwa.
 
Ukisha sema daily news unaisema sirikali kwa hiyo ukae ukijua maneno yenye mwelekeo tofauti na UCCM yatakuwa hayana nguvu kwa mtazamo rahisi ni kioo cha kujua nani ni nani na yuko wapi?
 
Niko huko tayari. nitwapa madongo yao na ole wao waondoe maana watakuwa wameshindwa kazi. unless waendelee kumuenzi Vasco da Gama.
 
Mkuu Kitila,

Ila kwa wale walioko serikalini au kwenye ajira ambazo wanoko wa serikali wanaweza kuwafanya vibaya, nimewapa tahadhari tu kuwa waingie hiyo forum ya daily news kwa uangalifu mkubwa.

Usiri muda mwingine ni mzuri sana hasa katika mambo ya siasa.

Na kweli, hao kwa kweli itabidi wakae mguu sawa maana yale majamaa yakikasirika hayashikiki. Good advice.
 
Ukisha sema daily news unaisema sirikali kwa hiyo ukae ukijua maneno yenye mwelekeo tofauti na UCCM yatakuwa hayana nguvu kwa mtazamo rahisi ni kioo cha kujua nani ni nani na yuko wapi?

Hii si mara zote ni kweli. Ushahidi upo, hasa ukisoma makala za Adamu Lusekelo!
 
hivi kweli mnafikiri wameanzisha hiyo forum kwa bahati mbaya? Wanataka kuwa na "chombo" chao... lakini papa hukaangwa kwa mafuta yake..
 
Nimetumia computer ya kazini kujaribu kupitia hii forum ya daily news. Jamaa hapa wanasystem kali sana ambayo huwa si tu inablock virus toka nje, bali pia ina uwezo wa kusoma system ya attackers.

Nilivyofungua some staff kwenye hiyo forum, nimepata warning kuwa kuna cookiez ambazo ziko set up kwenye hiyo website ili kutrack some information.

Bado sijui kama wamefanya on purpose au ni vile original script ya hiyo forum iliandikwa. Kwa wale ambao wanataka kujiunga nawapa tahadhari tu kuwa makini. Unaweza kujiunga moja kwa moja na kuwa muwazi kama Kitila na Mwanakijiji walivyofanya.

Ila kwa wale mulioko Tz na ambao munapenda kuficha majina yenu na kazi zenu kwa sasa, inabidi muwe makini kidogo. Hata hivyo, kwa wale watakaopenda kujiunga huko nadhani huu ni wakati mzuri wa kwenda kugive hell some guys huko.

Mimi nitakaa na JF maana ndiyo forum pekee so far ninaiamini kwa protection ya ID za membaz wake.

Thanks

Tatizo lingine pia kuhusiana na hizo tracking cookies linasababishwa na aina ya Forum wanayotumia ambayo ni phpBB, hii Forum ni very buggy na huwa inakuwa attacked kila siku na spammers na hackers. Sitoshangaa baada si mrefu ukaanza kuona postings za Porn na uchafu kibao. Moderators inabidi wawe fast au labda wa-implement security mods za maana.
 
geeque, point nzuri hiyo; tatizo nimeona majina ya ma mods tu lakini sidhani kama kuna mtu ameipa kweli umakini unaostahili. Iweje Zitto iwe category? au ndio wameamua kutafuta gia ya kuingilia...
 
geeque, point nzuri hiyo; tatizo nimeona majina ya ma mods tu lakini sidhani kama kuna mtu ameipa kweli umakini unaostahili. Iweje Zitto iwe category? au ndio wameamua kutafuta gia ya kuingilia...
Hiyo Kweli kabisa Mwanakijiji hata mimi nimeshangaa Zitto kuwekwa kama Category nadhani labda hawajapata mtu anayejua ku-set up Forums vizuri au labda wanasubiri hadi Kikwete aende tena Scandinavia kuomba watalam wa ku-set up Forums.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom