Serikali kuregister watumiaji wa Simu

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
Serikali kupitia wizara ya sayansi na teknologia na kushirikiana na tume ya masiliano nchini ina mpango wa kuregister watumiaji wote wa simu za mkononi ili kuwathibiti wanaotumia simu hizo kwa uhalifu ama kuwakashfi wengine ama kuwanyanyasa wengine. Habari hii ni kwamujibu wa taarifa ya habari ya TBC1 leo hii. Zoezi hili kwa kweli litakuwa gumu sana hasa kwa watumiaji ambao tayari wana kazi za simu za mikononi.....
 
Kwa kweli swala hili linatia aibu sana kwa Tanzania, wataalamu wa mawasiliano na komputer na pia wataalamu wa polisi wa mambo ya upelelezi (surveillance). Nijuavyo mimi ni kwamba hata kama mtu ataficha namba bado watu wa kampuni watajua huyu mtu amepigia akiwa maeneo gani na kwa kutumia namba ipi. Mfano halisi ni kwamba hamjawahi tembea na simu zenu mara ukaona inaonyesha uko mwenge, upanga, oysterbay au kariakoo. Sasa kama watu wa mawasiliano wanaliwezesha hili ishindikane vipi kumjua mtu anayepiga simu kwa kuficha namba? Kutunga sheria ni kupoteza muda tu kwani sheria hiyo haitekelezeki kwa Tanzania, kwanza hatuna anwani au makazi ya kueleweka. Hata mtu akija na jina la uongo na anwani anayokaa ya uongo watu wa kampuni za simu hawawezi confirm identity ya mtu huyu. Hata kama vitambulisho au barua za utambulisho zitatakiwa bado serikali itakuwa inaongeza tatizo jingine la rushwa na forgery. Mimi binafsi naamini kuwa tatizo hili linatokana na uvivu wa wataalamu wetu kufikiri na kubuni namna za kitaalamu kuzuia hili. mfano watu wa mawasiliano wanaweza ku-trace/track down mawimbi hadi wakajua huyu mtu anayepiga simu yuko eneo gani kwa wakati anaoongea. Pia katika simu kuna facilities za kuzuia kupokea unknown numbers/simu zilizofichwa namba au kurekodi maongezi. Maongezi ambayo yanakuwa ushahidi iwapo kesi itakwenda mahakamani. tatizo la nchi yetu ni kuwa na wataalamu waliosoma darasani tu na muda mwingi wakishinda kwenye vilabu vya mataputapu badala ya kushinda maabara wakijaribu kugundua vitu. Tumebaki kuwaachia wazungu tu kubuni kila kitu tukiamini kuwa anachogundua mzungu ndicho bora kuliko anachogundua mswahili. Na pia wanasiasa wetu wasikurupuke tu kusema vitu bali watuambie wataalamu wao wamewashauri vipi ili tupime kama wanawashirikisha. Tusije tukawalaumu wataalamu kumbe hawana hatia isipokuwa utaalamu wao hausikilizwi.
 
Mfunyukuzi, hili zoezi la kusajili watumia simu ni zuri sana, ila labda utekelezaji wake kwa nchi kama TZ unaweza kuwa mgumu kidogo. Lakini kama watafanikiwa katika zoezi la utoaji "Vitambulisho vya Uraia" suala la kughushi litakuwa dogo. Manake mpaka ukaghushi kitambulisho cha uraia ndio upate namba ya simu. Na kumbuka kitambulisho cha uraia kitakuwa na maelezo kibao ikiwemo picha, hivyo kumtafuta mtu kama amefanya uhalifu itarahisishwa. Unaposema kampuni za simu zinaweza kufuatilia wapiga simu hilo ni sawa, lakini kumbuka wafanya maovu hununua ile kadi ya simu, huitumia nakuzima ama hata kuitupa baada ya huo uhalifu. Hapo utampata vipi hata kama unajua alipiga akiwa Kayanga, Kagera. Ni hivi juzi tu kuna habari iliandikwa katika gazeti (silikumbuki) kuwa kuna dada alijiua kisa mme wake alitumiwa ujumbe unaoeleza uchafu afanyao huyo dada, naye mme wake akautuma huo ujumbe kwa mke wake. Sasa hawa wanaotuma ujumbe hivi unaweza kuwa kweli, ama wanataka kuvunja ndoa. Ukianzishwa huo mpango wa kusajili kutakuwepo ugumu fulani wa kufanya uhalifu kupitia simu.
 
Kadi za simu kwa vitambulisho
Maulid Ahmed
Daily News; Thursday,January 15, 2009 @20:01

WIZARAya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia inatarajia kupeleka bungeni Muswada wa Sheria ya Mawasiliano ambapo mtu atanunua kadi ya simu na kupata namba ya simu kwa kitambulisho, badala ya utaratibu holela unaotumika sasa.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla, alisema hayo jana wakati akielezea mafanikio ya Wizara yake kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Alisema muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Mkutano ujao wa Bunge la Jamhuri utakaoanza mwishoni mwa mwezi huu. Sambamba na hilo, wizara hiyo inatarajia kuanzisha rejesta ili kubaini matumizi mabaya ya simu za mkononi yakiwamo ya watu kutukanana au kutishana.

Akizungumzia wingi wa minara ya simu, alisema, “tumezishauri kampuni za simu zishirikiane kutumia minara kwa kila mtu kuweka antena yake katika mnara mmoja, hasa iliyo maeneo ya makazi ya watu; Vodacom na Zantel wameshaanza kushirikiana”.

Alisema jumla ya watumiaji wa simu nchini hivi sasa ni 11,719,000 na kati yao 163,300 ni wa simu za mezani na 11,555,700 za mkononi. Hata hivyo alisema takwimu hizo zinatokana na kadi za simu zilizouzwa mpaka sasa.

Alisema wizara yake kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wamefanikiwa kuondoa simu za kukoroga na kuanzisha huduma za simu za mkononi zinazotumia teknolojia ya ‘Code Division Multiple Access’.

Alitaja mafanikio mengine kuwa ni kukamilisha ujenzi wa mitambo mipya ya kupitisha taarifa za intaneti katika manispaa za Arusha, Dar es Salaam na Mwanza. Ujenzi wa vituo vingine vya Dodoma na Zanzibar unatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha. Kadi
 
Back
Top Bottom