Serikali kununua samani kutoka nje

Nyauba

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
1,098
105
Kwa muda mrefu sasa serikali na idara zake imekuwa ikitumia mamilioni ya fedha kutokana na bajeti yake kununua samani za maofisi yake kutoka makampuni mbalmbali yanayofanya biashara ya samani (fenicha) kutoka nje.

Hali hii si tuu imedumaza ukuaji wa sekta ya samani hapa nchini bali imezuia ukuaji wa ajira na kipatoo kwa umma wa watanzania wanaojihusisha na biashara hii amabayo mali ghafi yake hupatikana kwa wingi hapa nchini.

Je bado ni halali serikali kuendelea na utaratibuu huu?? wapi TCCIA, TPSF, WIZARA YA VIWANDA, IKULU, OFISI YA WAZIRI MKUU kupiganiaa ununuzi wa wa samani za ndani ili kukuza ajira na kuongezaa kipato..

naomba mwenye data za kiasi cha fedha kitumiwacho kutokana na bajeti ya serikali kwa ajili ya ununuzi wa samani.

Kenya nakumbuka Mh Kibaki ametoa maelekezo ofisi zote za umma kununua samani kutoka JUA KALI GROUP na serikali iwezeshha kundi hilii katika kujiimarishaa kibiashara kwa kuwapatia mtaji..

Tanzaniaa tuko wapi?????
 
Jamani samani zetu zina walakini sana, quality yake ni mbovu sana especially zile za keko pale:frusty:, mtoto akiruka mara mbili tu kwenye kiti basi kochi linabomoka na unakumbana na uchafu uliojazwa ndani humo. Siungi mkono hili swala la kununua samani nje lakini wangejitaidi kuwapa ujuzi vijana wetu kwa kutengeneza vitu vyenye ubora
 
Hivi hakuna makampuni yanayotengeza fanicha hapo bongo? Nashangaa sana, tunauza logs (magogo) China then tunaenda kununua fenicha aibu hii. Hivi VETA, wawekezaji wa ndani, workshop za Serikali/Halmashauri, mashirika ya dini na watu binafsi wameshindwa kuanzisha viwanda vya fenicha? Aibu hii
 
usanii kila sekta!! ukisema tutumie thamani za bongo itakuwa aibu; labda kidogo zitoke mikoani si viwanda vya hapa dsm wizi mtupu
 
Ni nini samani ??? Kidogo naomba upembuzi yakinifu kuhusu huo msamiati uliotumia sikumbuki kukutana nao nilipokuwa shule pale Kirare !!
 
Nimekuwa nikiona baadhi Watanzania walioko Marekani na Uingereza wakiwa wanaendesha magari ya bei mbaya kama Range Rover kwa pesa za mikopo au za kuchanja huku bado wanaishi kwenye nyumba za kupanga.Hawana tofauti na Serikali,kujaribu kujikuna pale mkono usipoweza kufika.

Nchi kama ni masikini ni masikini.ofisi za serikali hata uzipambe kwa samani za hali ya juu,Baadhi ya shule ziwe na internet access,ujenge barabara za juu kwa juu n.k,Bado ukweli unabakia pale pale Watanzania wengi bado wanaishi kwenye mazingira ya umaskini wa kutupwa.
 
Jamani samani zetu zina walakini sana, quality yake ni mbovu sana especially zile za keko pale:frusty:, mtoto akiruka mara mbili tu kwenye kiti basi kochi linabomoka na unakumbana na uchafu uliojazwa ndani humo. Siungi mkono hili swala la kununua samani nje lakini wangejitaidi kuwapa ujuzi vijana wetu kwa kutengeneza vitu vyenye ubora
Samani zao zinawalakini kwasababu soko lao bado ni dogo.Serikali ikiwawekea guarantee kwenye mikopo ya kununua Nyenzo na kununua samani kutoka kwao baada ya muda kuna ambao watatengeneza nzuri kama hizo zinazotoka Malaysia au Dubai.Lakini tukiendelea kusema kwamba zinawalakini after a few years tutaanza kununua kutoka Kenya zenye kiwango sawa na hizo zinazitoka Italy.
 
Ni nini samani ??? Kidogo naomba upembuzi yakinifu kuhusu huo msamiati uliotumia sikumbuki kukutana nao nilipokuwa shule pale Kirare !!

kiongozi mimi nilidhani unatokea Pwani au visiwani kumbe huu msamiati hujakutana nao! ndiyo hivyo ni samani.
 
usanii kila sekta!! ukisema tutumie thamani za bongo itakuwa aibu; labda kidogo zitoke mikoani si viwanda vya hapa dsm wizi mtupu
Aibu hiko pale Wageni wanapolinganisha ofisi ya Pinda au za Bunge na maisha ya Mtanzania anayeishi Kijijini.
 
Hivi hakuna makampuni yanayotengeza fanicha hapo bongo? Nashangaa sana, tunauza logs (magogo) China then tunaenda kununua fenicha aibu hii. Hivi VETA, wawekezaji wa ndani, workshop za Serikali/Halmashauri, mashirika ya dini na watu binafsi wameshindwa kuanzisha viwanda vya fenicha? Aibu hii
Pale mwenge karibu na Efatha ministry kuna kampuni inaitwa maridadi unaweza tembelea show room yao, inatengeneza high quality furniture ila ndo hivo tena bei yake ni noma kwa akina yakhe
 
Jamani samani zetu zina walakini sana, quality yake ni mbovu sana especially zile za keko pale:frusty:, mtoto akiruka mara mbili tu kwenye kiti basi kochi linabomoka na unakumbana na uchafu uliojazwa ndani humo. Siungi mkono hili swala la kununua samani nje lakini wangejitaidi kuwapa ujuzi vijana wetu kwa kutengeneza vitu vyenye ubora

Nilipokuwa jeshini tulikuwa tnatengeza samani nzuri sana kule Chang'ombe.

Ni wajibu wa serikali kukuza products za nchini badala ya kukuza za nje:

Serikali ya Japan haitumii bidhaa yoyote iliyotengezwa na kiwanda kilicho nje ya japan, unless Japan haina kiwanda cha aina hiyo.
 
Mkuu inasikitisha, lakini ukweli ni kwamba ile sehemu ni kama kagofu flani na imegeuka mradi binafsi japo si rasmi!
 
hata sekta binafsi kwa maana ya muungano wa watengenezaa samani nchini upo?? kama upo basi haujawa na sauti imara ya kuisukuma serikali na taasisi zake kutoa kipaumbelee kwa soko la ndani..

nashangaa pale TCCIA inapofanana na taasisi ya umma kwa viongozi wake kupendeleaa kupiga picha na viongozi na vikao vya kunywa chai katika mahoteli makubwa nchini badala ya kuwa mtetezi wa kweli wa sekta ya biashara nchini..
 
Kama magufuli alisema viatu majeshini na secta zingine zitokane na viwanda vya ngozi zinazotengenezwa hapa TZ, Mery nagu kinamshinda nini kutangaza?
Wenye nafasi kwenye maamuzi wangekuwa serious tungekuwa mbali lakini?
 
Back
Top Bottom