Serikali kujenga magereza 39 mapya; sasa kila wilaya itakuwa na gereza lake

Mafuchila

JF-Expert Member
Apr 29, 2006
751
65
Tanzania yangu huwa haiishiwi vituko. Baada ya ukarabati na ujenzi wa nyumba kubwa na ya kisasa zaidi ya kuhifadhia maiti katika nchi za SADDC, sasa tunawapiga bao jirani zetu kwa kuhakikisha kila wilaya inajitosheleza na kujitegemea kwa kuwa na gereza lake yenyewe....

Magereza nchini yaelemewa

na Ghisa Abby, Morogoro
amka2.gif
MAGEREZA nchini zinakabiliwa na msongamano wa wahalifu kutokana na kuwapo 38,000 wakati magereza hayo yana uwezo wa kuchukua waharifu 29,522.

Hayo yalibainishwa jana mjini hapa na Kamishana Jenerali wa Magereza, Augustino Nanyaro, baada ya kuwavisha nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Nne maofisa na askari magereza 37 katika sherehe iliyofanyika katika viwanja vya gereza la Mtego wa Simba Kingorwila mkoani Morogoro.

Alisema kukosekana kwa magereza katika baadhi ya wilaya kunachangia kwa kiasi kikubwa msongamano huo ambapo wahalifu wake wanalazimika kuwekwa katika magereza za wilaya za jirani.

Alisema ili kukabiliana na msongamano huo, wanatarajia kujenga magereza 39 katika wilaya ambazo hazina magereza.

Aidha, alisema wameweka mkakati na vyombo vya dola kupunguza msongamano huo kwa mahabusu ambao kesi zao zinaweza kufanyiwa upelelezi haraka na kutolewa hukumu badala ya kuchukua muda mrefu.

Alisema mara nyingi msongamano huo husababishwa na mahabusu ambao kesi zao ziko katika hatua za upelelezi.

Source:Tanzania Daima 6.6.2012
 
Hizo hela zingepelekwa katika shughuli nyingine za maendeleo, wakajaribu kuwafunga watu kifungo cha nje kwa kushiriki kazi za mikono hususan kwa zile kesi ndogo ndogo.
 
Hata wakijenga kwa kila kata bado haisaidi, sababu wengi wanafungwa kesi feki. Wezi wenyewe hawaguswi ila itawaongezea polisi-nyinyiemu standing allowance kwa kuwapa kesi sizo ndizo.
 
Kama kuna wakati serikali ya CCM imewahi kufanya jambo la maana, basi ndio hilo. MAGEREZA

Ifikapo mwaka 2015, serikali mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Au Tanganyika kutegemeana na Uamsho watafanikiwa vipi katika fujo zao za kidini) chini ya CHADEMA, itakuwa na kazi kubwa na ngumu ya kusafisha majiji kwa kuwaweka magerezani viongozi wa serikali iliyopita.

Kama kuna kitu tutahitaji sana kwa wakati huo ni PINGU na JELA. Hebu fikiria hizi rushwa na ubadhirifu vilivyokithiri kwenye halmashauri kiasi kila leo tunasikia bajeti zimekataliwa na kamati ya bunge bila wahusika wa madudu kuchukuliwa hatua.

Nawashauri waweke facilities za maana huko kwani ni kwa ajili yao wenyewe.
 
mahospitali mengi yamejengwa na kanisa wao wanawaza wahalifu badala ya kufikiri kujenga hospital na kuzuia uhalifu wa kufunga watu kwa udokozi wakati wezi wanasifia na rais na chama chao
 
kuwa na magereza mengi hakubadilishi hali ngumu ya maisha ya nnchi hii, kuna mambo mengi sana ya kushughulikia kabla ya magereza..mfano kureview mfumo mzima wa kimahakama kutapunguza msongamano wa wafungwa.
 
wanaandaa makazi yao bora maana wanajua 2015 wengi saana wataishia jela baada ya CDM kuchukua nchi.
 
They won't build no schools anymore
All they build will be prisons, prisons (2*)
They won't build no schools anymore
All they build will be prisons, prisons

... you got to love lucky Dube
 
wanaandaa makazi yao bora maana wanajua 2015 wengi saana wataishia jela baada ya CDM kuchukua nchi.
Umenikumbusha joke kama hii:
Mwanasiasa kijana: Kwa nini wananchi walipokuomba kuwajengea shule ulisema "wakikuchagua utawajengea" lakini wafungwa walipokuomba uwapatie kila mmoja chumba chake self contained, digital TV, computers na raha nyengine umewaambia "kesho ujenzi utaanza?".
Mwanasiasa Mkongwe: Sitarajii kurudi tena shule lakini kama mwaka huu hatukushinda nina hakika gerezani ndiko yatakuwa makazi yangu.

:focus:Badala ya kutumia fedha kujenga magereza, hizo fedha wazianzishie miradi ya maendeleo ili kupunguza/kuondosha uhalifu.
 
I am a prisoner
they are not building schools any more but what they build is only prisons. Why? Badala ya kuwaelimisha watu zaidi ili waepuke uovu, wanajenga magereza, kwa ajili ya nani? Wanamwandaa nani kuwekwa huko, kwanini wasiyaboreshe yaliyopo yawe na hadhi ya kuishi binadamu kuliko yalivyo sasa ambapo hata mbwa hawawezi kukubali kufungiwa huko?
 
Kukimbilia kujenga magereza ni layman solution, magereza hayapunguzi uhalifu.
Kama kweli lengo ni kupunguza uhalifu, ni aheri hizo fedha zitumike kujenga shule zenye viwango vya juu na pia zitumike kuratibu mfumo wa ajira kwa vijana ili kupunguza uhalifu.
Wahalifu wa siku hizi ni askari hivyo ni bora kuongeza mishahara ya askari ili waweze kujikimu na kuacha tamaa zinazowapelekea kuwa majambazi.
Fedha hizo za kujengea magereza zitumike kuratibu mipango ya kupambana na mfumuko wa bei unaopelekea watendaji wa idara mbalimbali za serikali kuwa wala rushwa na kushiriki ktk wizi na ufisadi.
Hii serikali inakosa watu makini wa kupanga mipango endelevu ya kupunguza umaskini unaopelekea watanzania wengi kushiriki ktk uhalifu kwa nia ya kupambana mfumuko wa bei.
Tanzania imezidi kuwa kituko kwa kukosa viongozi wenye dhamira endelevu.
 
kesi ndogo ndogo kama za kuiba kuku ingekuwa ni viboko na kufanya usafi mijini kuliko kurundikana gerezani.
 
akili matope ya viongozi wetu. Badala ya kufikiria kifungo cha nje na kuboresha mfumo wa polisi na mahakama wao wanafikiria kuendelea kufunga watu. Au ni maandalizi ya wapinzani wa katiba ya nyinyiemu? Hata pimbi somtimes huwa anakuwa na akili lakini siyo viongozi wa hii serikali. Raisi ajaye atapata kazi kubwa sana ya kuwabadilisha hawa vichwa mgando ili taifa liweze kusonga!! Thanks uliyeweka kibwagizo cha prisoner ya dube,tuna wakoloni weusi wanatupa shida sana!
 
Usisikitike mwana jf ukiona mgonjwa anasema maneno mengine yasiyo na usawa ujue uwezo wa kufikiri umekaribia mwisho
Tanzania yangu huwa haiishiwi vituko. Baada ya ukarabati na ujenzi wa nyumba kubwa na ya kisasa zaidi ya kuhifadhia maiti katika nchi za SADDC, sasa tunawapiga bao jirani zetu kwa kuhakikisha kila wilaya inajitosheleza na kujitegemea kwa kuwa na gereza lake yenyewe....

Magereza nchini yaelemewa

na Ghisa Abby, Morogoro
amka2.gif
MAGEREZA nchini zinakabiliwa na msongamano wa wahalifu kutokana na kuwapo 38,000 wakati magereza hayo yana uwezo wa kuchukua waharifu 29,522.

Hayo yalibainishwa jana mjini hapa na Kamishana Jenerali wa Magereza, Augustino Nanyaro, baada ya kuwavisha nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Nne maofisa na askari magereza 37 katika sherehe iliyofanyika katika viwanja vya gereza la Mtego wa Simba Kingorwila mkoani Morogoro.

Alisema kukosekana kwa magereza katika baadhi ya wilaya kunachangia kwa kiasi kikubwa msongamano huo ambapo wahalifu wake wanalazimika kuwekwa katika magereza za wilaya za jirani.

Alisema ili kukabiliana na msongamano huo, wanatarajia kujenga magereza 39 katika wilaya ambazo hazina magereza.

Aidha, alisema wameweka mkakati na vyombo vya dola kupunguza msongamano huo kwa mahabusu ambao kesi zao zinaweza kufanyiwa upelelezi haraka na kutolewa hukumu badala ya kuchukua muda mrefu.

Alisema mara nyingi msongamano huo husababishwa na mahabusu ambao kesi zao ziko katika hatua za upelelezi.

Source:Tanzania Daima 6.6.2012
 
Acha wayajenge tuu, si ndo yatatumika kuwafunga wao baada ya 2015 tukiwatoa ikulu
 
Duh. magamba kweli wameanza kuona mbali, kwenye katiba mpya wamesema kiwepo kifungu cha kuruhusu kupinga matokeo ya Rais mahakamani, jambo linaloonyesha weshanusa kushindwa uchaguzi wa 2015, na hili la kuongeza magereza ambayo bila shaka yatakuwa na vyumba self contained, bila shaka sasa anguko, wanaliona dhahiri,wameamua kuanza kujiandalia makao na ukiangalia na takukuru nao wameanza kuwa na meno kwa kuwapeleka vigogo mahakamani kwa idadi kubwa!
 
Back
Top Bottom