Serikali kuingilia biashara ya usafirishaji kutaka kuboresha huduma ya treni sio haki

Wafanyabiashara binafsi wamekosa uaminifu, wamekuwa walafi na wakwepa kodi wakubwa. Baadhi wamenyonya sana wananchi na kujilimbikizia utajoro mkubwa huku wakitoa huduma duni sana.

Ingawa serikali huwa inashidwa hasa kwenye usimamizi, wakati umefika sasa wa either serikali ifanye huku ikiboresha usimamizi au kuwe na ubia wa 50/50 ili kuimarisha uendeshaji na usimamizi wa huduma kwa jamii.
Dala dala - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Sijaona hoja hapo zaidi ya ubinafsi uliogubika nafsi yako. Usafiri wa umma mijini ukiboreshwa hutia chachu ya maendeleo. Hebu fikiri ifikapo jioni daladala znamaliza ruti zao? Tunatumia muda gan kwenye foleni na tunaamka saa ngapi ili tufikekazin saa 1:30/2:30 asbh?
 
Kuna watu hufuraia wanapoona watz wanateseka kwenye magari
Kwa taarifavyako serikali hutumia billion 200 kukarabati reli wakati hutumia billion 300 kukarabati barabara fanya hesabu then chukua hatua
 
Nimesikitishwa na uhamuzi wa Mh Mwakyembe.

wa kuanzisha usafiri wa trani jijini Dar es Salaam;

1. Hii ni serikali kuanza ukiritimba wa kufanya biashara ambayo ilishindwa toka kipindi kile.tunarudi socialism

2. Ni uhamuzi wa kisiasa zaidi badala ya kitaalamu (zima moto)

3.Kunenepesha matumbo ya watu fulani wkt wa tenda ya kusafirisha ; tunarudi kwenye MATATIZO YA UDA

4. Kuna watu wanamikopo ya biashara ya Daladala kwenye mabenki ; sijui watailipaje kutokana na kupato kupungua na abiria wenye kukimbilia usafiri wa trani.

5. Foleni inasababishwa na magari binafsi sio DALADALA; Sijui hizo takwimu wamezitoa wapi. wangetakiwa kufungu mageti ya kuingilia mjini kwa kucharge gari binafsi shillingi 5000; ili kudiscourage foleni.

6.Biashara ya mafuta itaongezeka kwa kuiba ya kwenye trani km tunavyo shuhudia

umbali wako mkubwa wakufikiri ni pua yako huwezi fikiri zaidi na ndio maana ukaamua kunadika kitu kama hiki .
kila siku tunapiga kelele tuache ubinafsi lakini watu hatukomi
reli ya kati wameua ili wasafirishe mizigo na malaori ambayo yana uabarabara zetu kisa tu wewe unapata na wendine hawapati.

sehemu zakufanyia kazi na hiyo daladala yako mbona zipo nyingisana ndje na nadani yadar ? shirikisha ubongo wakati wakufikiri utaona opportunity nying sana
 
Mlizoeshwa vibaya. Kuua vitu vya umma ili muanzishe vyenu na kujitajirisha.

Hoja zako ni dhaifu sana. Majibu uliyopata yanatosha.

Nakuongezea tafakari yako kwa hoya hizi: Hivi reli nazo zikifufuliwa utasema malori yenu mliyokopa itakuwaje? Bandari je? Viwanja vya ndege?
 
Kutumia train na feri ni mojawapo ya njia kuu ya kupunguza foleni ya magari jijini Dsm na kurahisisha usafiri kwa abiria. Lakini kuna tatizo kubwa mpaka sasa Watanzania tunashindwa kulipigia kelele,barabara zetu zote ni nyembamba,hata hizi zinazojengwa na kupanuliwa sasa bado ni nyembamba. Mpaka sasa Dsm hakuna magari ya kusababisha foleni hizi kama tungekua na barabara pana na vivuko vya juu sehemu za makutano! Jiulize kwanini barabara za Kilwa, Nyerere, Kawawa, Morogoro na Bagamoyo zisiwe na njia 6 kutoka na 6 kuingia? Tatizo jingine ambalo tuna uwezo nalo,kwanini hakuna sheria kwamba ktk barabara kuu kama hizo nimetaja hapo juu,zitahudumiwa na mabasi ya abiria kuanzia 100? Hatuhitaji misaada toka nje kuyafanya haya!
 
train.JPG

Mbona usafiri wa treni ; kipunguni-lumo-tandika hatupati update nipo kituoni, sijaona train tatizo nini?
 
Mtoa hoja anaumizwa na mkopo wake wa kidaladala tu hana lingine na huo ni ubinafsi mbaya sana wa kuona bora wengi waumie ili wachache wanufaike, principal za maendeleo hazisemi hivyo. Treni itasaidia sana watumishi kuwahi kazini na kurudi nyumbani mapema maana kuamka saa 11 kurudi nyumbani saa 2 wakati muda wa kazi ni saa 1 na nusu mpaka saa 9 sio adhabu ndogo, kama usafiri huo ukitengemaa na kuenea maeneo mengi ni malimbukeni tu ndio wataenda kazini na private car.
 
Tatizo la usafiri mbovu wa daladala ndo umetulazimisha watu wengi kujiingiza kichwa kichwa na kukubali kukopa mamikopo ya riba za ajabu ili kuondokana na kero ya usafiri wa daladala, kimsingi serikali lazima ianze kufanya biashara kwenye sekta muhimu ili kuweka competition ya ukweli na hata ikibidi ukwasi coz hii free market yenu iliyokaa kideal maana mnaforce demand iwe kubwa ili mjustify hikes za price. Serikali agiza sukari, lete train, uza mafuta, uza mchele halafu hawa wanaotuchezea akili zetu wakome. Hivi ni nani anaeona ufahari kutoa elfu 20,000 kununua mafuta ya gari kila siku, hapo bado maintance ya gari? Watu wanakuwa forced kununua magari ili atleast ukivaa shati lako jeupe basi ufike kazini ukiwa msafi, daladala chafu, makonda na madereva (sio wote) wachafu, ruti mnakatisha, what a shame? tena wala msiongee nyinyi ni wapuu kazbisa na mnachangia umasikini wetu. Laki sita za mafuta si una tofali mia sita? banda la kuku hazitoshi?
 
Mimi sioni tatizo coz hakuna kipengele ambacho wamekataza wafanyabiashara kuendelea na hiyo sekta ya usafirishaji i mean daladala na aina nyingine za usafiri hata hii ilikuwa wazi ila kwakuwa hakuna Creativity na kutokuwa na uthubutu ndiyo maana hakukuwa na mwekezaji wa kibongo aliyekuwa amefikiria kuwekeza kwenye area kama hiyo. Issue hapa ni wananchi wapate huduma bora siyo nani anatoa hiyo huduma. Kuna nchi kama dubai Sekta nzima ya Usafiri inamilikiwa na Serikali na Life linakwenda murua kabisa.
Tusiwe negative kwa kila kitu vingine lets support.:poa
 
ana mawazo ya kimaskini, ndio hao hao wanaroga hata vyuma, kitu hakijaanza ulishaonyesha njaa zako, nyie mkopo mnalipage wakati kila siku migomo, kukatisha ruti na kulipa faini ndio zenu, daladala nyingi hazina madreva wenye akili, wengi kibangi bangi. Tumechoka na uchakavu, wazipele chuma chakavu bado zinahitajika.
 
Pole sana ndugu yangu naona utakua umeelimika kwa post zilizotumwa. Sikuamini kuwa mpo mnaofuraia watu kuumia ili mfanye vurugu na vipanya vyenu, sasa mtashika adabu. Ukitaka biashara ya daladala lazima ujipange na uwe mbunifu utoe huduma sio kero.
 
Mkuu R.B lazima uwe na hisa huko SUMATRA. Na pia ndio maana mlitaka kumfupishia maisha mtu wa Mungu. Nani alikwambia ukipeleka dala dala mikonani au vijijini haitalipa!!!
 
Nimesikitishwa na uhamuzi wa Mh Mwakyembe.

wa kuanzisha usafiri wa trani jijini Dar es Salaam;

1. Hii ni serikali kuanza ukiritimba wa kufanya biashara ambayo ilishindwa toka kipindi kile.tunarudi socialism

2. Ni uhamuzi wa kisiasa zaidi badala ya kitaalamu (zima moto)

3.Kunenepesha matumbo ya watu fulani wkt wa tenda ya kusafirisha ; tunarudi kwenye MATATIZO YA UDA

4. Kuna watu wanamikopo ya biashara ya Daladala kwenye mabenki ; sijui watailipaje kutokana na kupato kupungua na abiria wenye kukimbilia usafiri wa trani.

5. Foleni inasababishwa na magari binafsi sio DALADALA; Sijui hizo takwimu wamezitoa wapi. wangetakiwa kufungu mageti ya kuingilia mjini kwa kucharge gari binafsi shillingi 5000; ili kudiscourage foleni.

6.Biashara ya mafuta itaongezeka kwa kuiba ya kwenye trani km tunavyo shuhudia

We kweli ***** unatumia masaburi kufikiri. Wananchi wanahusikaje na mikopo ya daladala. Gari binafsi zinahusiana nn na treni. Think b4 post.
 
Mtoa mada kuna haja ya kumpeleka ngambo akapate exposure na aone serikali za wenzetu zilivyojikita kwenye fast moving trains.
Inchi nyingi treni hutumika kama public transport convenient ya haraka na rahisi apa kwetu serikali ililala sasa imezinduka mnaona hasara.
 
Nimesikitishwa na uhamuzi wa Mh Mwakyembe.

wa kuanzisha usafiri wa trani jijini Dar es Salaam;

1. Hii ni serikali kuanza ukiritimba wa kufanya biashara ambayo ilishindwa toka kipindi kile.tunarudi socialism

2. Ni uhamuzi wa kisiasa zaidi badala ya kitaalamu (zima moto)

3.Kunenepesha matumbo ya watu fulani wkt wa tenda ya kusafirisha ; tunarudi kwenye MATATIZO YA UDA

4. Kuna watu wanamikopo ya biashara ya Daladala kwenye mabenki ; sijui watailipaje kutokana na kupato kupungua na abiria wenye kukimbilia usafiri wa trani.

5. Foleni inasababishwa na magari binafsi sio DALADALA; Sijui hizo takwimu wamezitoa wapi. wangetakiwa kufungu mageti ya kuingilia mjini kwa kucharge gari binafsi shillingi 5000; ili kudiscourage foleni.

6.Biashara ya mafuta itaongezeka kwa kuiba ya kwenye trani km tunavyo shuhudia
Mkuu usiogope biashara yako ya daladala itarudi ndani ya siku 50 tokea treni ianze kufannya kazi
siku ya tatu treni itaishiwa mafuta
siku ya kumi reli itatakiwa kufanyiwa ukarabati
siku ya arobaini itajulikana kuwa dereva ana leseni ya kughushi
siku ya 49 kichwa kitaharibika kwa kuwa kina miaka 74 tokea kianze kufanya kazi
siku ya 50 unarud na daladala lako kubeba abiria na kuendeleza unyanyasaji kwa abiria kwa kasi zaidi
kuwa na subira tafadhali
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Back
Top Bottom