Serikali katika hali mbaya kifedha

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Kuna taarifa kuwa kufuatia fedha nyingi zilizotengwa katika bajeti ya mwaka 2011/12 kutumika kwa shughuli za maazimisho ya miaka 50 ya Uhuru ambazo hazikuwa na tija, Serikali kupitia Hazina imekata zaidi ya asilimia 50 ya Bajeti za Idara na Wizara zake pasipo kueleza fedha hizo ambzo zilitengwa kwa kazi za maendeleo zinahitajika kurejeshwa Hazina kwa kazi ipi. Hatua hii imeelezwa kuwa itaathiri kwa kiasi kikubwa sana ugharimiaji wa shughuli za maendeleo ..hivi karibuni watanzania wategemee hali mbaya.

Kuna taarifa kuwa katika bajeti iliyopitishwa na Bunge kwa mwaka 2011/12 Serikali ilitioa mgao awamu moja tu katika Wizar zake ambao ulifanyika Mwezi Agosti 2011 na sasa imeamua kurejesha Hazina sehemu ya fedha hizo zilizotengwa kwenye Bajeti ya Serikali.

Ikumbukwe kuwa hata ile Bajeti ya maazimisho ya Uhuru haikuwahi kupitishwa Bungeni. Hivyo yawezekana kabisa ilitoka katika fedha zilizotengwa kwa ajili ya Maendeleo.
 
Wakati huo huo Serikali imewaongezea wabunge posho ya kuketi kitako kutoka 70,000 kufikia 200,000 kwa siku
 
Tetesi?
Umenichanganya hapo kidogo..

"SERIKALI imekiri kwamba haijapeleka fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri nchini na kuna matatizo makubwa ya fedha" ~ HabariLeo 02/02/2012
 
Tetesi?
Umenichanganya hapo kidogo..

"SERIKALI imekiri kwamba haijapeleka fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri nchini na kuna matatizo makubwa ya fedha" ~ HabariLeo 02/02/2012

Serikali yakiri kuwepo kwa upungufu wa fedha katika bajeti Send to a friend
Tuesday, 06 December 2011 20:40
0digg
Nora Damian
SERIKALI imesema kiwango cha ukusanyaji mapato nchini kiko chini hali inayoifanya kuomba misaada ya nje kufidia hasara ya asilimia 13 wanayoipata kila mwaka kwenye bajeti yake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, wakati wa maadhimisho ya tano ya siku ya mlipa kodi Waziri wa Fedha , Mustafa Mkulo alisema kiwango cha ukusanyaji mapato nchini kiko chini ukilinganisha na nchi nyingine zilizoko kusini mwa jangwa la sahara.

Mkulo alisema licha ya mamlaka hiyo kukusanya Sh604 bilioni mwezi Septemba lakini kiwango hicho bado ni kidogo ukilinganisha na nchi hizo.

Kwa mujibu wa Mkulo, kwa sasa Tanzania inakusanya asilimia 16 tu ya pato la taifa wakati kiwango kilichowekwa ni asilimia 17.4 na kwamba kiasi cha asilimia 1.4 ni kikubwa na kinatosha kulipa mishahara ya wafanyakazi kwa mwaka mzima.

"Makusanyo duni yanasababisha kuwepo na pengo kubwa kwenye bajeti yetu la asilimia 13 na kuifanya Serikali kuomba misaada na mikopo ya ndani na nje ya nchi ili kuziba pengo hilo," alisema Mkulo.Waziri huyo aliitaka TRA kupanua wigo wa kodi na kuongeza makusanyo na kwamba walipakodi wanaokwepa kulipa kodi hawaikomoi serikali bali wanajikomoa wenyewe.

Akizungumzia tozo mbalimbali, Mkulo alisema wanaangalia namna ya kupunguza tozo hizo katika mwaka ujao wa fedha baada ya kubaini kuwa kuna tozo 28 katika lita moja ya bidhaa ya petroli.

Naye Mwakilishi wa walipa kodi nchini, Ndibalema Mayanja aliitaka serikali kupunguza kiwango cha kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kutoka asilimia 18 hadi 15 ili kuwawezesha kupata faida.

Alisema mara nyingi wafanyabiashara wamekuwa wakipata hasara kutokana na kodi kubwa ya ongezeko la thamani pamoja na mianya mbalimbali ya rushwa baina ya mamlaka hiyo na walipakodi husika.

Alisema wameandaa mkakati utakaomwezesha mlipakodi kukataa rushwa kwa kushirikiana pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili kuhakikisha rushwa inadhibitiwa miongoni mwao pamoja na maofisa wa TRA.

"Tumeandaa maadili yatakayomwezesha mlipakodi kukataa kutoa rushwa kwa maafisa wa TRA na katika hili tunaomba serikali itulinde kwa sababu walipa kodi wengi ni wafanyabiashara," alisema Mayanja.

Mwakilishi huyo pia aliishauri serikali kushirikisha vizuri wafanyabiashara wakubwa na wa kati katika eneo la upanuzi wa kodi kwani sekta binafsi ina mchango mkubwa zaidi katika suala zima la mapato.Pia aliitaka serikali kuziagiza Idara na Taasisi zake kuacha kununua samani kutoka nje ya nchi badala yake wanunue samani za ndani ili kukuza pato la ndani.

Alisema biashara na ukusanyaji mapato bila rushwa inawezekana.Katika maadhimisho hayo TRA ilitoa tuzo kwa taasisi mbalimbali zikiwemo zile zilizosaidia katika makusanyo ya kodi, mlipakodi mwenye mafanikio katika biashara, mlipa kodi aliyelipa kiwango kikubwa cha kodi na walipakodi watatu waliofanya biashara katika miaka 50 iliyopita.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites




















[h=2]SUNDAY, DECEMBER 11, 2011[/h][h=3]Waziri Mkuu aeleze ufujaji wa sherehe za Uhuru[/h]

Vyombo mbalimbali vya habari vya leo tarehe 11 Disemba 2011 vimeeleza kwamba kesho tarehe 12 Novemba 2011 Waziri Mkuu Mizengo atakuwa mgeni rasmi katika shughuli maalumu ya kufunga Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru itakayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Mkoani Dar es salaam.

Kwa makadirio ya vyanzo mbalimbali kiwango cha fedha kilichotumiwa mwaka huu kwa ajili ya ‘sherehe' za miaka 50 ya uhuru kinazidi bilioni 50; hivyo natarajia kwamba Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ndiye mwenyekiti wa maandalizi ya maadhimisho hayo atatumia shughuli hiyo ya kufunga kueleza pia kiwango halisi cha fedha ambacho kimetumiwa hivi sasa na Serikali kupitia Wizara na taasisi zake.

Toka wakati wa bunge la bajeti nimekuwa nikisikitishwa na kiwango kikubwa cha fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya ‘sherehe' za uhuru katika bajeti za Wizara mbalimbali huku kukiwa na upungufu wa fedha za miradi ya maendeleo.

Gharama za maisha kwa wananchi ziko juu na uchumi wa nchi uko kwenye hali tete kwa sababu ya pamoja na mambo mengine mfumuko wa bei na kuporomoka kwa shilingi. Hali hii inachangiwa pia na ubadhirifu na matumizi ya anasa ya fedha za umma ambapo ‘sherehe' hizi ni sehemu za matumizi hayo.

Wakati wa bunge la bajeti nilipiga kura ya HAPANA ya kukataa bajeti ambayo ilitenga fedha nyingi kwenye posho za vikao na matumizi mengine yasiyokuwa ya lazima huku mipango mingine muhimu ya maendeleo mathalani ya kuwezesha jiji la Dar es salaam kupata maji, ujenzi wa barabara za pembezoni kwa ajili ya kupunguza foleni, malipo ya madeni ya walimu, askari na watumishi wa umma pamoja na mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ikiwa haijatengewa fedha za kutosha.

Majibu ya serikali wakati wote yamekuwa ni kwamba hakuna fedha za kutosha sasa ni muhimu Waziri Mkuu Pinda watanzania mabilioni ya ‘sherehe' hizo yametoka wapi; kwa kuwa kiwango cha matumizi yaliyofanyika kinaonyesha kuwa juu hata ya kile ambacho kimekuwepo kwenye bajeti iliyopitishwa bungeni.

Kiwango hicho cha fedha kingeweza kugharamia masuala yafuatayo ambayo yangefanyika katika kipindi cha mwaka mmoja maadhimisho ya uhuru yangekuwa na maana zaidi kwa sababu tarehe 9 Disemba 1961 Mwalimu Nyerere akihutubia taifa alieleza kuwa ‘uhuru ni kazi' wala hakusema ‘uhuru ni sherehe'.

Maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru yangekuwa na maana kama yangeacha kumbukumbu ya mwaka 2011 kwa kulipa madeni yote ya walimu, askari na watumishi wengine wa umma; pamoja na kuelekeza fedha hizo kwenye miradi iliyotengewa fedha kidogo.

Mathalani ujenzi wa barabara za pembezoni za kupunguza foleni Dar es salaam umetengewa bilioni tano tu, ujenzi wa bwawa la maji la Kidunda umetengewa bilioni sita, na kuna watoto wa maskini ambao wamekosa mikopo na kushindwa kuendelea na elimu tofauti na ahadi ya Kikwete; fedha hizi zingetosha kufanya matumizi haya yote na mengine.

Aidha katika kufunga maonyesho hayo Waziri Mkuu Pinda afafanue pia sababu za maonyeshoya Wizara na Taasisi mbalimbali kufanyika zaidi mkoani Dar es salaam kama vile miaka 50 ya Uhuru ilikuwa kwa ajili ya watu wa Dar es salaam pekee. Fedha hizi za umma zingekuwa na maana kama zingetumiwa kuzunguka nchi nzima kuhamasisha maendeleo mitaani na vijijini ili kusonga mbele kama taifa kwa kuwa mafanikio ya miaka 50 ya Uhuru yanapaswa kujionyesha yenyewe katika maisha ya wananchi.

Wakati Wizara na Taasisi hizo zikiwa zinatumiwa fedha nyingi kufanya maonyesho kwa gharama za posho, machapisho na matumizi mengine yasiyokuwa na lazima; watumishi wa umma wako kwenye hali mbaya na mishahara katika taasisi zao imekuwa ikicheleweshwa. Hivyo, pamoja na kufunga maonyesho Waziri Mkuu Pinda anapaswa kufuatilia kwa kina matumizi ya wizara zote na taasisi zote zinazowahusu ili kuwa na uwajibikaji kutokana na matumizi haya.

Izingatiwe kwamba matumizi haya yamehusisha pia matumizi ya mara nyingi ya fedha za umma kwenye masuala yale yale ya maonyesho kwa kuwa toka mwaka huu uanze Wizara na Taasisi zimekuwa zikifanya maonyesho yao kila moja pekee na kutumia fedha za umma. Wizara na Taasisi hizo hizo nyingi zikashiriki tena maonyesho ya Saba Saba na Wizara na Taasisi hizo hizo zimerudia tena kushiriki maonyesho ya Uhuru katika viwanja hivyo hivyo; katika mkoa huu huu mmoja wa Dar es salaam.

Haya yanafanyika wakati wakina mama wajawazito na wagonjwa wengine wanafariki katika Hospitali ya Mwananyamala, Temeke, Amana, Muhimbili na Ocean Road kwa ajili ya kukosa madawa na huduma nyingine za msingi miaka 50 baada ya uhuru; haya yanafanyika wakati bado kuna shule nyingi za msingi na sekondari katika Mkoa huu huu wa Dar es salaam ambazo hazina vifaa muhimu ikiwemo madawati miaka 50 ya Uhuru.

Hivyo, ili kushughulikia mianya ya ufujaji na ubadhirifu kutokana na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru ni kamati ya maandalizi iliyoongozwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda itoe taarifa ya mapato na matumizi. Aidha, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aingize kipengele maalum cha matumizi ya fedha za ‘sherehe' za uhuru katika ukaguzi wake wa kila Wizara, Taasisi za Umma , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika ukaguzi wa Matumizi ya fedha za mwaka wa fedha 2011/2012.

John Mnyika (Mb)
11/12/2011









 
hadi tutaelewa tuu maana kwa maneno ya zitto somo halikueleweka sasa hadi kijijini wataelewa tu
 
Mustafa Mkullo ni mmoja wa watu wapumbavu waliowahi kuishi kwenye ardhi hii; hivi kweli kabisa anadiriki kusema eti kiwango cha ukusanyaji mapato kiko chini ndiyo maana wanalazimika kufanya umatonya? Nani ameizuia serikali kukusanya kodi kikamilifu? Si ndiyo haohao wanaopeleka vi-memo TRA vya kukwepesha kodi halafu leo hela hakuna ndiyo wa kwanza kulialia. Hawa ndiyo watu wanaotakiwa kufungwa maisha kwa uhaini kwa taifa, huu ni wendawazimu usiofikirika kabisa.
 
Back
Top Bottom