Serikali iwajibisheni BOT kwa kutuibia/kutudanganya

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
WanaJF mambo vipi?,natumai mu wazima.
Nimeshindwa kuelewa wanajf wenzangu huu mlolongo wa madudu unaofanywa na baadhi ya viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza maamuzi yaliyo sahihi kutokuwa na uzalendo na nchi yao.Hivi BOT wanatudhihirishia kuwa sisi ni matajiri sana wa kuchapisha matoleo mbalimbali ya fedha? Tukiwa tunatumia thamani moja ya fedha yenye miundo miwili tofauti?? na kama walilolifanya ni sahihi mbona wameshindwa kuweka kikomo cha matumizi ya hizi pesa za zamani?ambazo ndizo(orijino) PIA BOT WAMETULETEA UMASIKINI MKUBWA:Nasema hivyo kwa sababu ndani nina pesa hizi mpya zenye thamani ya sh 35,000 nilikwenda nazo benki ya CRDB,NMB kudepost lakini walizikataa ukiwauliza sasa hizi nitazipeleka wapi hawakuelezi tena wanakuambia wamekatazwa na benki kuu kuzichukua sasa najiuliza kwa mwendo huu wa 10% si tutaitundika nchi juu ya mti?.
 
Pole kaka hii yote ni kutokana na udhaifu wa kikwete kukemea na kuwachukulia hatua watu wanaoharibu kazini,

Ukweli waliofanya order na waliotengeneza fedha hizo wapo na hautasikia wakiwajibishwa kwa fedha mbovu kama
hizo,kakaa kimya kama hajaziona leo ukimuliza kwann atajibu ''HATA MIMI NASHANGAA''
 
.....PIA BOT WAMETULETEA UMASIKINI MKUBWA:Nasema hivyo kwa sababu ndani nina pesa hizi mpya zenye thamani ya sh 35,000 nilikwenda nazo benki ya CRDB,NMB kudepost lakini walizikataa ukiwauliza sasa hizi nitazipeleka wapi hawakuelezi tena wanakuambia wamekatazwa na benki kuu kuzichukua sasa najiuliza kwa mwendo huu wa 10% si tutaitundika nchi juu ya mti?.

Hujafunguka vizuri...kwanini wamekataa kupokea fedha ulizowapelekea?
 
Back
Top Bottom