Serikali italinda Amani kwa Nguvu Zote - Dk Shein

zanzibar siyo nchi ndo maana rais wake ana consult kila kitu hata kwa vitu vidogo na vyepesi kama hivi...
 
Baada ya kimya kingi toka makanisa yapigwe kibiriti huko z'bar hatimaye Mhe. Mkuu wa kisiwa hicho ameongea jana. Katika hotuba hiyo alisikika akipinga vikundi vya kidini kutumika kisiasa. Pia alitoa pongezi nyingi kwa jeshi letu la polisi kwa kuleta udhibiti wa machafuko! Hapa ndipo aliponikera mhe huyu.

Hivi ni kweli polisi hawa wanastahili pongezi? Ni pongezi kwa lipi walilofanya, wakati tunaambiwa jumla ya makanisa 25 yamepigwa kibiriti toka mwaka 2001? Polisi hawa wamekuwa wapi hadi matukio haya yanatokea? Je ni kweli polisi hawana intelijensia ya kuangalia viashirio vya uvunjifu wa amani? Au wanasubiri hadi waone moto unawaka ndio wanachomoza na kurusha moshi wa machozi?

Kinachonikera zaidi katika hili ni kitendo cha serikali ya smz hasa viongozi wake wa juu kutokuwa wazi kulieleza hili moja kwa moja umma uelewe. Tunajua ni wazi hawataki muungano! Wawe wazi basi! Waliweke hilo bayana, tujue badala ya kuendelea kunyanyasa wabara waishio huko visiwani. Mbona wao wamejazana bara na hakuna anayewabugudhi? Nenda dsm, mbeya, songea, tabora n.k utakuta waz'bar tele! Wanafanya mambo pasipo bugudha yoyote! Hivi Tunafaidika nini na muungano huo, zaidi ya makelele ya kila siku eti tunawanyonya waz'bar. Tunawanyonya vipi? Haileweki!

Kwa upande wa bara pia, ni wakati viongozi wetu wachukue hatua tumechoka na haya matusi na manyanyaso wanayopata hawa wenzetu waishio visiwani. Acheni siasi chukueni hatua kabla hatujashuhudia mambo mabaya (mungu aepushie mbali) yakitokea! Uongozi unapaswa uchukue hatua ngumu kuhusu muungano badala ya kusema tu mambo ya muungano hayapaswi kujadiliwa. Matokeo yake ndio haya.

Wote tumekuwa mashahidi wakati wa utawala wa mhe. Karume. tulikuwa tukimsikia shamuhuna na bwana himid wao walikuwa wazi kuelezea wanavyokereka na muungano. Japo litabaki swali je walikuwa wanawakilisha mawazo ya nani, je ni msimamo wa serikali yao au ni mawazo yao binafsi? Kwa kiasi kikubwa naamini huo ndo msimamo wa smz kwa sababu hakuna aliyekuwa akiwapinga watu hawa!

Kauli zingine chafu za kupinga muungano na kuvunja heshima zilitolewa na bwana jussa, tena hadharani na media zilimrekodi, Lakini hakuna mamlaka yeyote (si z'bar wala bara) iliyotoa tamko lolote kuhusu kauli hizi za huyu mheshimiwa. Leo hii tunaaminishwa eti wale walochoma makanisa ni wahuni wachache, kweli?

Kitakwimu ni zaidi ya makanisa 25 yamechomwa toka mwaka 2001 huko z'bar, hawa wanaachwa na kupuuzwa kwa kauli nyepesinyepesi tu eti ni WAHUNI!
 
Mkuu ni kweli hata mimi nalipongeza jeshi la polisi kwa kutokuua, Ilikuwa ni kawaiga kwa polisi kuua lakini hatujasikia mauaji wakuu, TUWAPONGEZE, Hata arumeru hawakuua!
 
Amechelewa. Makanisa hayakuanza kuchomwa juzi na wanaUAMSHO, miaka yapata 10 sasa yanachomwa, lakn kama kawaida ya serikali zetu mbili, kimyaaaa!
 
Hivi ni kweli polisi hawa wanastahili pongezi? Ni pongezi kwa lipi walilofanya, wakati tunaambiwa jumla ya makanisa 25 yamepigwa kibiriti toka mwaka 2001? Polisi hawa wamekuwa wapi hadi matukio haya yanatokea? Je ni kweli polisi hawana intelijensia ya kuangalia viashirio vya uvunjifu wa amani? Au wanasubiri hadi waone moto unawaka ndio wanachomoza na kurusha moshi wa machozi?
Atakauwa anazungumzia tukio la hivi karibuni. Anawapongeza kwa kutumia busara ya kutokutumia nguvu ya ziada kama kufyatua risasi za moto hivyo kuua/kujeruhi waandamanaji.

Kama ingetumika nguvu hiyo ya ziada nadhani hali ingekuwa mbaya zaidi maana hawa jamaa wameaminishwa hata jeshi la polisi ni la bara.
 
Amechelewa. Makanisa hayakuanza kuchomwa juzi na wanaUAMSHO, miaka yapata 10 sasa yanachomwa, lakn kama kawaida ya serikali zetu mbili, kimyaaaa!

Sasa hii kitu ndio haifai
Wanapaswa wavunje ukimya badala ya kungoja kupongeza watu au kutoa rambirambi kwa wafiwa!
 
June 1, 2012 | Na Jabir Idrissa | zanzibaryetu

HALI mbaya ya usalama iliyoanza Jumamosi usiku, imesadifu nilichokieleza wiki mbili zilizopita. Nilimsihi Rais Dk. Ali Mohamed Shein, kupitia safu hii, kuwa asikubali maneno ya fitna anayolishwa na wasaidizi wake. Nikasema akikubali fitna, atajishawishi kukasirika; na matokeo ya mtu kukasirika, ni kuchukua hatua yenye madhara makubwa.

Ilikuwa katika makala iliyojadili uhuru wa watu kusema na kujadili mambo ya nchi yao – ilitoka na kichwa cha habari kisemacho, "Hasira zako Dk. Shein, ni hasara kwako."

Kweli, hasira zilizowajaa viongozi wa serikali na vyombo vyao, zimezaa hasara. Sasa nchi, iliyokuwa imetulia kabisa, watu wakienda na kurudi kwenye shughuli za kutafuta maisha, imerudi kwenye hofu kubwa.

Rais hakuongoza vizuri au walioelekezwa kuongoza hawakutenda vizuri. Hapa, hapakutumika hekima na busara kwa kiwango. Hapa, kuna hali ya serikali kutoonyesha uvumilivu kwa raia.

Kwa kuwa Rais Dk. Shein ndiye kiongozi mkuu Zanzibar, analazimika kubeba lawama kwa madhara yaliyotokea. Yeye atatafuta wengine wa kuchangia lawama hizo.

Kosa kubwa lililofanywa katika kadhia hii, ni uongozi kuruhusu Jeshi la Polisi kukamata kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Mussa Juma.

Hapana. Kumkamata mtu si kosa, ila mazingira yaliyotumika. Ya Sheikh Mussa yalikuwa ya kigaidi na kijambazi. Yaliwashtua walioshuhudia. Wakajenga chuki dhidi ya serikali.

Hebu nitangulize hali ilivyokuwa Jumapili kabla ya kurudi kueleza kilichotokea Jumamosi usiku.

Soko la Darajani (maarufu la Mkunazini), lilifungwa kutwa nzima. Ndio tegemeo kwa wakazi wote wa maeneo ya katikati ya mji na nje kidogo (ng'ambo).

Stendi kuu ya magari (daladala) inayohudumia wananchi (daladala) ilifungwa. Stendi hii pia inahudumia wasafiri watokao vijiji vya mkoa wa Mjini Magharibi, na mkoa wa Kusini Unguja (Wilaya ya Kati na ya Kusini).

Usafiri wa umma na binafsi ulikwama kwa kuwa eneo la mkabala na lilipo soko hilo lilizuiwa kuingia magari.

Mji mzima na vitongoji vyake ulienea sauti/milio ya risasi za mipira na mabomu ya machozi zilizofyatuliwa na polisi.

Watalii walifadhaika sana kila waliposikia milio ya risasi.

Vijana wenye hasira walienea mitaani kuleta tafrani.

Mali nyingi ziliharibiwa, yakiwemo makanisa mawili.

Inafaa sasa kueleza kwanini hayo yalitokea. Najadili yaliyojiri Jumamosi. Ilianza kwa utulivu kama kawaida, mpaka jioni. Nilikuwa mjini katika moja ya hoteli tukijadiliana masuala ya kitaifa na wenzangu.

Tulipotoka saa 11, nilikimbilia waandishi wa habari kupata hili na lile – mambo yanayohusiana na habari. Utulivu mtupu.

Nikasimuliwa Jumuiya ya Uamsho iliendesha mhadhara mpaka mchana kwenye uwanja wa Lumumba katika mfululizo wa ratiba inayoendelea kwa miezi sita sasa.

Mihadhara ya asasi hii ya kidini, imekuwa na mvuto mkubwa kwa wananchi, hasa vijana ambao huwa wengi na kuifuata mpaka maeneo ya mikoani. Uamsho wameshaendesha zaidi ya mihadhara 50 Unguja na Pemba.

Mhadhara ulihusisha matembezi yaliyoongozwa na Amir wa Uamsho, Sheikh Farid Hadi, msafara ukipitia Gulioni, Msikiti Mabuluu, Mlandege, Michenzani, Rahaleo, Kwa Biziredi na kurudia uwanjani Lumumba.

Ilipofika saa 7 mchana, ulikuwa umekwisha; watu wametawanyika kwa amani na hakukuripotiwa tukio lolote la vurugu pamoja na askari polisi kuingilia msafara eneo la Kombawapya, wenyewe ukiwa umeshaingia uwanjani. Shwari ikaendelea mjini.

Ilipokaribia saa 2 usiku, alitokea kijana mtanashati kufika msikiti wa Kwa Bizireni anaposali na kusomesha Sheikh Mussa, mmoja wa viongozi waliohudhuria. Hakuna aliyemfahamu kijana huyu.

Alitoa salamu na kuitikiwa na wote waliokuwepo. Yule kijana aliyeonekana akishuka kwenye gari aina ya Noah, iliyopaki pembeni, alimvuta kiungwana Sheikh Mussa akimuomba wazungumze pembeni kidogo.

Sheikh Mussa alimfuata kijana ambaye akiifuata gari. Alipofika akiwa nje ya gari, huku mlango wa nyuma ya dereva ukiwa wazi, Sheikh Mussa alisalimiana na mtu aliyekuwa ndani. Lakini, ghafla akavutwa ndani ya gari, mlango ukafungwa kwa nguvu, na dereva akaondoa gari kwa kasi.

Ile ikashtua watu waliokuwa msikitini. Wakabaini Sheikh Mussa amechukuliwa na gari imeelekea Kariakoo.

Walibaini baadaye iliishia kituo kikuu cha Polisi Mkoa kilichopo Mwembemadema. Wakapata uthibitisho kuwa Sheikh Mussa amekamatwa na kushikiliwa Madema.

Waumini waliokuwa Kwa Biziredi walifadhaishwa. Hawakulala. Viongozi wa msikiti wakateua ujumbe kwenda kufuatilia Madema.

Hakukuwa na kiongozi wa polisi kuthibitisha. Taarifa zilivuja kutoka ndani ya kituo kwamba Sheikh Mussa kweli anashikiliwa pale kituoni.

Jitihada za viongozi wa msikiti kusihi Polisi wamuachie na kama kuna tuhuma apewe dhamana, hasa kwa kuwa familia yake haijui, zilishindikana. Taarifa za kukamatwa kwake zikaanza kuenea taratibu mjini.

Haikuchukua muda, makundi ya watu wakakimbilia Madema kutaka kujua hatima ya Sheikh Mussa. Kwa kuwa Polisi hawakutaka kujadiliana, walijiandaa kulinda kituo chao na kulinda "mtuhumiwa" wao.

Mwanzo wa matatizo ukawa umewadia. Polisi hawataki kusema wamemshika kiongozi wa Uamsho kwa tuhuma gani; wala hawapo tayari kujadiliana na yeyote ili kumpa dhamana. Huku watu waliokuwa wanajazana kituoni wakitaka kujua hatima ya kiongozi huyo.

Ilipotimu saa 3 usiku, eneo la Michenzani, mita chache kufika Madema likawa limejaa watu wanaofuatilia hatima ya Sheikh Mussa. Ndipo polisi walipoanza kulinda hadhi yao baada ya kuamini wanachezewa.

Risasi za mipira na mabomu ya kutoa machozi zikaanza kufyatuliwa moja baada ya nyingine. Kwenye saa 5 usiku, eneo hilo likawa limeenea harufu ya kemikali na moshi mzito. Sasa hata waliokuwa wapita njia na waliolala wakalewa sumu.

Nilishindwa kupita kwa gari Kariakoo. Palikuwa na kundi kubwa la vijana; barabara imezibwa kwa mawe na mapande makubwa ya zege huku matairi yakiwaka moto.

Niliposogea kwa kutembea nikijaribu kufika Michenzani, niliishia kwenye mkunazi, mita 100 hivi kufika. Nikaona magari ya polisi waliosheheni silaha mbele ya ofisi kuu za Idara ya Majenzi.

Kila baada ya muda fulani, nikasikia milio ya risasi na mabomu ya machozi zikielekezwa walipo vijana Kariakoo. Moshi na kemikali ziliponichosha, nikarudi eneo la Posta tulipoegesha gari.

Pale Kariakoo, nikabaini vijana wamekata tamaa; hawakuwa na ujasiri wa kusonga mbele kwenda kufuatilia kiongozi wao Madema. Wafanyeje? Wakaanza kuondoka katika vikundi vidogovidogo wakielekea maeneo ya ng'ambo.

Wakati wakitembea huku wengi wakiwa na mawe, marungu na mapande ya nondo, nilisikia baadhi yao wakisema, "Sasa kwa kuwa wametuzuia kumpata kiongozi wetu, tunasaka makanisa na baa tutayateketeza."

Wamekasirishwa na maudhi ya dola. Nikajua kazi itakayofanywa kutoka hapo, ni kazi chafu.

Ndivyo ulivyokuwa usiku wa Jumamosi. Mpaka nilipolala, nikiwa hoteli ya Grand Palace, Malindi, nilikuwa nikisikia milio ya risasi ya hapa na pale.

Hata nilipokuja juu yapata saa 9.30, nilisikia milio ya risasi, hali iliyoendelea hadi nilipoondoka mjini Zanzibar saa 7 mchana Jumapili.

Sishangai kusikia Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa amesema walikamata watu saba baada ya vurugu. Hakusema kamwe kama walimchukua kihuni kiongozi wa watu na hatimaye kuvutia umati kufika kituoni Madema kufuatilia.

Taarifa yake ilikuja saa kadhaa baada ya uongozi wa Uamsho kutoa tamko wakisema hawahusiki na vurugu wala uharibifu wa mali uliofanywa. Uislamu unakataza vurugu, wamesema.
 
Sasa hii kitu ndio haifai
Wanapaswa wavunje ukimya badala ya kungoja kupongeza watu au kutoa rambirambi kwa wafiwa!

woga kweli mkuu hakuna mtu anayetaka Muungano uvunjikie mkononi mwake aingie kwenye historia ya kuuvunja muungano,
walitegemea CUF wangeuvunja waaapi kumbe jamaa zilikua njaa tu!
 
Wachukue hatua sio kuleta maneno matupu tuuu... Kama tunataka kujenga amani basi sheria ichukue mkondo wake na hoja za MSINGI kuhusu muungano zisipuuzwee..!!:horn:
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom