"Serikali itafanya kila linalowezekana kuwatafuta samaki wote walioingia sokoni mpaka wapatiakane"

Laptop01

JF-Expert Member
Nov 29, 2009
1,362
791
Jamani baadhi ya hawa Mawaziri wetu wanataka kutupeleka wapi na kauli zao Bungeni? Jana nilimsikia Naibu Waziri- Kilimo na Chakula akiliarifu Bunge juu ya hatua za Serikali kufuatia Sakata la Samaki wanaosadikika kuletwa hapa nchini kutokea Japani wakihofiwa kuingiwa na mionzi ya nyuklia ambayo ni hatari kwa afya za viumbe hai.

Naibu waziri anasema Serikali imechukua hatua ikiwa ni pamoja na kuzuia mauzo zaidi ya samaki hao na kufanya kila linalowezekana kuhahikisha samaki walioingia sokoni (yaani walionunuliwa na wauzaji mbalimbali na walionunuliwa na walaji pia kwa maana hiyo) wanapatikana!

Jamani hivi utawapataje samaki walioliwa kama siyo utani mjengoni? cha ajabu zaidi wapo waheshimiwa humohumo Bungeni waliokuwa wakiipigia makofi kauli hii isiyotekelezeka na yenye kukosa umakini.

Ushauri: Dear Serikali jaribu kuwa makini na kauli zako kwa umma hata kama wabunge waliowengi mjengoni wameamua kukukubalia udanganyifu wako.
 
sasa kama wameshaliwa watawakamua watu matumbo?? au kwenda kukusanya vinyesi na kuunganisha??

kauli za wanasiasa hazina tofauti na maneno ya kwenye khanga
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom