Serikali isiyoshindwa kesi na wenye haki....

Lord K

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
213
37
Kila mgomo Tanzania siyo halali, ukiwa wa wanafunzi vyuoni,walimu,madaktari na pia maandamano yoyote yanayodai au kuonyesha udhaifu wa serikali pia nayo tunaambiwa ni kinyume na sheria hasa yakiwa ya CHADEMA au WANAHARAKATI,tamwa,WANAVYUO nk, tena usiombe suala lolote la wanyonge lifike mahakamani....lazima serikali ishinde... ila sasa,kwenye miradi ya mafisadi kana DOWANS n.k Serikali inashindwa kesi....kuna nini hapa sielewi.
 
Waalimu ni kweli wanamadai ya msingi lakini mwanasheria wao ndio kawaangusha.
 
Na swala hapa siyo serikali ila ni sheria zetu zilizotungwa na wakoloni ambazo ndiyo zinazotuongoza mpaka leo.
Na kwa kuanzia ebu tujumuike kwenye mchakato wa kubadilisha katiba ili tuweze tengua sheria hizi kandamizi.
 
Huwa ninashangaa sana ninaposikia serikali imeshindwa kesi na taasisi.
Iweje serikali imteue hakimu halafu ishindwe kesi?
 
Idadi kubwa ya majaji wa mahakama zetu wameokotwa mitaani wakihangaika na kesi za wizi wa mifugo. Kwa urafiki, wakateuliwa ili na wao wainuke. Ndo maana wapo wanaohongwa milioni 5, 10, 50, .....

Hawa watu wanaambiwa hukumu na wanaitikia badala ya kutumia usomi wao.
 
Na swala hapa siyo serikali ila ni sheria zetu zilizotungwa na wakoloni ambazo ndiyo zinazotuongoza mpaka leo.
Na kwa kuanzia ebu tujumuike kwenye mchakato wa kubadilisha katiba ili tuweze tengua sheria hizi kandamizi.
lakini mkuu kama suala ni uchakavu wa sheria,..mbona sheria za zamani zote ni revised edition 2002 iweje tumsingizie mkoloni??
 
Na swala hapa siyo serikali ila ni sheria zetu zilizotungwa na wakoloni ambazo ndiyo zinazotuongoza mpaka leo.
Na kwa kuanzia ebu tujumuike kwenye mchakato wa kubadilisha katiba ili tuweze tengua sheria hizi kandamizi.

Hata katiba ya sasa hivi ambayo tunasema ni mbovu, inapingana na sheria zetu nyingi tu, mfano sheria ya magazeti inayompa nguvu Waziri kulifungia gazeti. lakini serikali inaendelea na sheria hizi. maana yake hata tukiwa na katiba mpya, bado serikali inaweza kuleta sheria kandamizi, au inaweza kuendeleza sheria hizo ambazo zilipingwa na Tume ya Nyalali, kwa jeuri tu. dawa ni wananchi wenyewe tuamue kwamba serikali ya namna hii haitufai
 
Tatizo kubwa ni mfumo wetu kwani ili jaji mambo yake yamnyooke au apate vyeo vikubwa zaidi inategemea na serikali kwajiyo utaona kuwa jaji au hakimu yoyote nia yake ni kuipendesha serikali ili kesho wamfikirie itapotokea nafasi ya jaji wa wilaya au kanda fulani kwahiyo maadam ndoa ya majaji na serikali itaendelea kuwepo basi ni vigumu wahuska wengine kupata haki zao.
 
kimsingi kila katiba huwa inatengeneza utegemano wa katiba kuwa na mihimili ambayo imetenganishwa kama serikali, bunge na mahakama.Nchi yetu hakuutenganisho wa mihimili, serikali na mahakama, ni kitu kimoja,Kwa hiyo serikali dhaifu lazima itumie mahakama, kukandamiza hoja zinazojotokeza kuishambulia serikali dhaifu.
 
Waalimu ni kweli wanamadai ya msingi lakini mwanasheria wao ndio kawaangusha.

Kwani mwanasheria wao ndio anayetoa hukumu? Angalia alichokisema JK ulinganishe na alichokisema hakimu ndio ujue kuwa jk huwa anaingilia uhuru wa mahakama. Inadhihirisha kuwa jk alishakaa na hakimu na wakakubaliana kabisa kuhusu hukumu. Eti jumamosi na jumapili serikali haifanyi kazi? Mbona mikataba mingine (mfano ule wa Buzwagi na mingine mingi) ilisainiwa jumapili?
 
Back
Top Bottom