Serikali inatuangusha wananchi kwa kuwaachia mafisadi nchi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
benderatanzania.jpg
Bendera ya Tanzania

Mhariri
KILA mwaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amekuwa akifanya ukaguzi wake na kugundua upotevu mkubwa wa fedha, swali ni je wahusika wanachukuliwa hatua gani?Mbona naona kama usanii, nafikiri kuna haja CAG akapewa meno ya kuwafikisha mahakamani wahusika wote wanaofilisi nchi yetu kwani ukiaangalia hayo mabilioni yanayopotea hauwezi ukakaa jukwaani na kusema kama nchi yetu bado changa na kufunga safari za kwenda kuomba msaada nje kila siku wakati pesa zipo sema zinafujwa.
Vijana tuamke vinginevyo wajukuu wetu watakuja kutupiga viboko kwa kushindwa kulinda rasilimali za nchi kwa ajili ya future. Vijana wa Tanzania mnayaona hayo? Kumbuka mustakabali wa Taifa letu uko mikononi mwetu.
Hakuna ajira: wote tunajua. Elimu ni ghali sana: wote tunaona, bidhaa madukani ni bei juu sana, mnaona. Kana kwamba haitoshi, mabilioni ya jasho letu na la wazee wetu nalo hilo linaliwa!!! Je, mnadhani ni wajibu wa nani kulikomboa Taifa?
"INUKA, KWA MAANA KAZI HII YAKUHUSU WEWE, UKAITENDE." Nguvu ya umma tu itatukomboa na ufisadi huu jamani.
Cha msingi Watanzania tuhamasishane na kuelimishana kwa kila jambo kuhusiana na hali halisi ya nchi hii yenye asali na maziwa, na kuwa na msimamo mmoja, tukiwa waoga na kusikiliza za Vijitaarifa vya kintelejesia kamwe hatutatoboa.
Uwajibijaji uchukue mkondo wake bila kuwaonea haya wahusika wakuu, kwani wametenda dhambi hii kubwa hali wakielewa.
CAG na PCCB ni nafasi yao ya kushirikiana ili kuwawajibisha wahusika wote bila kulindana. Ni vyema wahusika waliosababisha hali hii CAG kwa ushirikiano wa karibu na PCCB wachukue nafasi yao kwa utekelezaji wa uhakika bila kulindana, mlipa kodi/mwananchi wa kawaida ajisikiaje na uharibifu huu.
Kama kamati ya Mrema imeweza kuamuru mafisadi huko Kilosa na kwingineko wakamatwe na wapelekwe polisi ni kwa nini ofisi ya CAG ambao wana ushahidi kamili wasiwashughulikie wahusika moja kwa moja?? Nimeona wengine wakishauri PCCB waungane na CAG, hili ni jambo la kushangaza, kwani hakuna kitu kinachofanywa na PCCB, hata ikifutwa leo hakutakuwa na hasara kwa Tanzania.
Francis Marela
Mwenge-DSM


Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Back
Top Bottom