Serikali inatengeneza yenyewe mazingira ya ufisadi kwenye ugawaji wa viwanja

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
Malalamiko yaliyojitokeza kwenye ugawaji wa viwanja uliofanywa na Manispaa ya Temeke ukihusisha viwanja vilivyopimwa kule Gezaulole ni matokeo ya mipango mibovu ya serikali kuhusu ugawaji huo.
Kanuni za soko zinasema ‘Low supply high demand’ kwa tafsiri rahisi isiyo rasmi ‘uchahce wa bidhaa sokoni huleta na uhitaji mkubwa’. Na popote penye uhitaji mkubwa wa bidhaa adimu husababisha wahitaji / wauzaji kutumia rafu katika kununua / kuuza bidhaa hiyo ili kujinufaisha zaidi wao binafsi. Kwa wanunuzi , wale wenye nguvu ya kufanya rafu ndiyo wanaopata hiyo bidhaa na kwa wauzaji, wale wenye nguvu hunufaika kwa kujipatia vipato visivyo halali – rushwa.

Haihitaji mtu kuwa genius kujua kuwa manispaa ya Temeke (wauzaji) imegawa viwanja kwa upendeleo usiomithilika kwa wenye nguvu ya kucheza rafu. Rafu hizi ni pesa, vyeo vya wanunuzi, umaarufu wa familia za wanunuzi n.k!
Napata tabu sana kuamini kama kulikuwa na equal chances za watu kupata viwanja pale Manispaa ya Temeke kutokana na idadi kubwa ya vigogo waliopata viwanja na idadi kubwa sana ya watu wasio na majina maarufu na/ama pesa waliokosa.
Najaribu pia kujilazimisha niamini kuwa kuna wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu wakuu ama watu wa nafasi kama hizo ambao waliomba viwanja na wamekosa lakini nafsi yangu inakataa!

Niliwahi kuwa victim wa hali kama hii pale halmashauri ya mji wa Kibaha wakati walipokuwa wanagawa viwanja vya mwanalugali. Kulikuwa na viwanja vya Super low Density. Nikaamua kuomba. List ya mgao ilipotoka nilijilaumu mwenyewe kwa nini niliomba viwanja hivyo na hapo ndipo nilipo jua hakuna equal chances za kupata viwanja. Watu waliopata viwanja hivyo ni ma-RC, wabunge, ma-RPC, Ma-DC, mwaziri, makatibu wakuu wa wizara na watu kama hao na orodha nzima ilijaa watu hao.

Iko wapi equal chance?
Kwa nini kuwe na viwanja 1,800 halafu zitolewe fomu zaidi ya 4,000 za kuomba kununua viwanja tena kwa shs 30,000 tena kukiwa na orodha tayari ya watakaopata viwanja?!! Huu ni uwizi wa mchana.
Kwa nini serikali / halmashauri zipime viwanja vichache wakati wanunuziwatalkipia gharama za upimaji?
Mbona wakati mradi wa viwanja 20,000 ulipoanza viwanja vingi sana vilipimwa na watu walinunua kwa urahisi sana mpaka wizara ikaruhusu kulipia kwa awamu? kwa nini visipimwe viwanja vingi ili kusiwe na hizo rafu?

Serikali iko kwa ajili ya nani kama siyo wananchi walio wengi?
Hivi kuna umuhimu gani wa kuwa na wizara ya Ardhi kanma kuna mapungufu kiasi hiki na haichukui hatua stahiki?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom