Serikali inapopigwa mkwara na mwarabu

Mwan mpambanaji

JF-Expert Member
Apr 3, 2008
482
131
Kwa kweli nimeshangazwana kuhuzunika kwa kauli za vitisho,kebehi,na kejeli zilizotolewa na Al adawi anayejiita mwekezaji,
Tanzania tumefika mahali mtu binafsi anatisha serikali yenye vyombo vyote vya dola,tena mtu ambaye si raia wa Tanzania,na serikali inakaa kimya,lazima sisi wazalendo tuhoji na kuhoji uhalali wa serikali,ndugu zangu nyote mmeshuhudia anayejiita mwekezaji tena mwenye zaidi ya wafanyakazi 25,000,duniani pote anaogopa kamera,serikali yetu imemwogopa mtu anayeogopa kamera aibuuuuu
wazalendo wenzangu tangu lini kabla na baada ya uhuru mgeni akaichimba biti serikali?
kama taifa hatuihitaji mwekezaji anayetutisha,imefika mahali serikali iwe na kauli na msimamo ambao kila mtu anaujua,vinginevyo itakuwa haina uhalali wa kutawala wala kuongoza..............
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom