Ngambo Ngali
JF-Expert Member
- Apr 17, 2009
- 3,517
- 1,360
Wakati hoja hiyo ikisugua vichwa vya wabunge, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) imesema serikali haitalitelekeza Shirika la Umeme nchini (Tanesco) iwapo litaamua kwenda Mahakama Kuu kuwasilisha pingamizi dhidi ya maombi yaliyowasilishwa Dowans.
Maombi hayo yanataka hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC) isajiliwe katika Mahakama Kuu ya Tanzania ili Tanesco iilipe fidia ya Sh. bilioni 94 kwa kuvunjiwa mkataba wake.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa serikali ina kila sababu ya kuisadia Tanesco katika jambo hilo kwa vile shirika hilo ni mtoto wake kwa asilimia 100. "Tanesco wakiamua kwenda mahakamani, si mtoto wa serikali, vipi tumtelekeze?" alihoji Masaju.
Masaju alitoa kauli hiyo baada ya kutakiwa na NIPASHE kueleza nafasi ya serikali kuhusu hatma ya maombi hayo ya Dowans dhidi ya Tanesco yaliyowasilishwa Mahakama Kuu ya Tanzania Januari 25, mwaka huu.
Swali hilo la NIPASHE kwa Masaju lilikuja baada ya Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Salvatory Bongole, kuwaambia waandishi wa habari juzi kuwa Tanesco wenyewe na mtu mwingine yeyote, wanaruhusiwa kuwasilisha pingamizi mahakamani hapo.
Masaju alisema mbali ya kuwa Tanesco ni mtoto wa serikali, pia hawawezi kupuuza maslahi ya taifa. "Vyovyote vile, hatuwezi kupuuza maslahi ya taifa hili. Kwani nani hiyo hela haimuumi?" alihoji Masaju.
Aliwataka Watanzania kusubiri kwani iwapo maamuzi ya kupinga maombi hayo ya Dowans mahakamani yatafikiwa, jambo hilo litakuwa bayana mahakamani.
NIPASHE ilipomtafuta Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, William Mhando, kueleza kama shirika lake litaweka pingamizi Mahakama Kuu dhidi ya maombi ya Dowans, juhudi zake ziligonga ukuta.
Badala yake, mwandishi alishauriwa kuwasiliana na Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud, ambaye alipotakiwa kueleza suala hilo, alisema kwa ufupi: "No comment" (Sina la kuzungumza) na alipotakiwa kueleza kwanini hana la kuzungumza, alisisitiza kusema: "No comment."
CHANZO: NIPASHE
Mambo hayo, baada ya kusema kuwa Dowans lazima ilipwe serikali yetu hiihii inabadilika ghafla na kusema kuwa itaingia kuisaidia Tanesco kwa maslahi ya taifa. Kwa nini mwandishi wa habari hakuuliza maslahi ya taifa yamejulikana lini ndani ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ambaye amekuwa akisisitiza kuwa Dowans Lazima ilipwe, kiasi cha kumfanya abadili mawazo yake
Mwanzoni ofisi ilikuwa na mtazamo kuwa Dowans lazima ilipwe na kwa kuwa na msimamo huwo kulikuwa na vigezo fulani vilivyomshawishi AG kuwa na msimamo huo. Vigezo hivyo bado vipo lakini AG kabadili msimamamo AG haoni kuwa hata akishindwa kihalali Wtanzania hatutamuelewa na badala yake tutajua bayana kuwa katusaliti kutokana na msimamo wake wa awali? Kimadili AG hakutakiwa kufanya Uturn ya ghafla hivyo bila hata kujustify sababu ya hiyo U turn.
Kufanya hivyo ( kuwa na misimamo miwili katika issue moja) kimaadili ni kosa. Ndio maana scale of justice ile nembo ya sheria haiko balanced imelala upande mmoja.