Serikali inapohangaika na mitihani ya Form 4 na Form 6

bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
495
Nimeikuta habari hii nikaona niilete hapa tujadili;

WIZARA YARUDISHA MIHULA YA ZAMANI YA MITIHANI FORM FOUR NA SIXW

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imerudisha utaratibu wa mihula kama ilivyokuwa zamani kutokana na kile ilichoeleza kuwa utaratibu wa sasa unasababisha walimu kutumia muda mwingi kusimamia na kusahihisha mitihani wakati wa masomo.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amesema kwamba mwakani utaratibu wa kufanya mitihani kwa Kidato cha Nne na wa Kidato cha Sita utakuwa kama ilivyokuwa zamani.


  • Wakati hivi sasa mitihani ya Kidato cha Nne imekuwa ikifanyika Oktoba, mwakani itafanyika Septemba.
  • Kwa upande wa Kidato cha Sita ambao mitihani imekuwa ikifanyika Februari, mwakani itakuwa Mei.
  • Utaratibu wa likizo utaendelea kuwa Juni na Desemba.

“Mwakani tunarudi kama ilivyokuwa mihula ya zamani. Kidato cha Nne wafanye mitihani Novemba badala Oktoba na Kidato cha Sita itakuwa mitihani Mei kama zamani ili walimu wabaki kufundisha shuleni badala ya kuzunguka kwenye mitihani na kusimamia,” alisema Naibu Waziri.

Uamuzi huo unalenga kuondoa kile ambacho baadhi ya wabunge walilalamikia kuwa baadhi ya walimu wamekuwa badala ya kufundisha, kutumia muda mwingi kusimamia mitihani na pia kwenda kusahihisha.

Kwa utaratibu uliorejeshwa, usahihishaji kwa Kidato cha Sita utafanyika kipindi ambacho wanafunzi watakuwa likizo ambacho ni Juni.



Source: wavuti - wavuti

MY TAKE; Najiuliza sana, form six baada ya mtihani Mei, watakuwa na muda gani hadi kupata matokeo yao, na kisha ku-apply vyuo vikuu na bodi ya mikopo ili ikifika Septemba wawe wameshaingia vyuoni tayari?
 
Another episode in a silly season,wizara inaongozwa na under performers,dr kawambwa alitimuliwa udsm baada ya kushindwa kuandika maandko yanayo defend position yake.Mulugo alipata zero form six na anakashfa ya shule yake kuiba mitihan
 
Huyo mulugo mpaka jina kafoji.hamna kitu hapo,hii sisiemu kwa kweli ni janga la kitaifa.huyo mulugo achunguzwe ni hewa hamna kitu hapo
 
Duh! Ule utaratibu wa kumaliza shule kwa form six na kukaa nyumbani mwaka mzima wanaurudisha tena!?
 
Duh! Ule utaratibu wa kumaliza shule kwa form six na kukaa nyumbani mwaka mzima wanaurudisha tena!?
Filipo inawezekana kabisa vijana wakaanza kukaa mwaka mzima home kusubiri matokeo na kisha kufanya applications za vyuo kama enzi za mwinyi
 
Last edited by a moderator:
Yaani mtoto amalize Form IV Novemba, aende Form V July? Si nzuri kwa watoto wetu, hasa wa kike. Kwa nini tusifuate mifumo ya kwingineko duniani?
 
kichwa cha mwenda wazimu.....ndo mfumo wetu wa elimu, kila waziri akiingia huingia na "kichaa chake"
 
kwaiyo alifafanua sasa itakuweje kwa form six na bodi ya mikopo pamoja na lini haswa wanaingia chuo?au mfumo nao umebadirika?
una nasikia hasira sana awa mabozo mawaziri wanapoongea maneno yanayoacha maswali badala ya kutoa utatuzi!!!
 
Kwani tatizo nini kwa mfumo wa sasa naona hayo mawazo yao si sahihi.
 
Nimeikuta habari hii nikaona niilete hapa tujadili;

WIZARA YARUDISHA MIHULA YA ZAMANI YA MITIHANI FORM FOUR NA SIXW

.....

  • Wakati hivi sasa mitihani ya Kidato cha Nne imekuwa ikifanyika Oktoba, mwakani itafanyika Septemba.
  • Kwa upande wa Kidato cha Sita ambao mitihani imekuwa ikifanyika Februari, mwakani itakuwa Mei.
  • Utaratibu wa likizo utaendelea kuwa Juni na Desemba.

"Mwakani tunarudi kama ilivyokuwa mihula ya zamani. Kidato cha Nne wafanye mitihani Novemba badala Oktoba na Kidato cha Sita itakuwa mitihani Mei kama zamani ili walimu wabaki kufundisha shuleni badala ya kuzunguka kwenye mitihani na kusimamia," alisema Naibu Waziri....
Mbona kama hii taarifa inachanganya!
 
Back
Top Bottom