Serikali inaogopa maandamano?

potokaz

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
530
486
Wadau,

Kuna haja ya ya kuja na paln B au tuamue kuitekeleza plan A. JF kama great thinkers tujadili hili.

Mbowe ameongelea civil disobedience. Hivi tunatakiwa kutii kila kinachosemwa na polisi hata kama ni cha hovyo?

Wanakataa maandamano badala ya kuyalinda yasizae vurugu.

Wajuzi watupe muongozo, endapo sauti zetu zinamimywa zisitoke kupitia maandamano, tutaziolea wapi?

Endapo tunapingana na uchafu wa watawala tuta demnstrate vipi?

Endapo tuna sababu za kuandamana na polisi wanakataza, njia ipi tuifuate?

Nawasilisha.
 
Iwapo Chadema watathubutu kuandamana kesho, na kutojali vitisho vya jeshi la polisi, basi huo utakuwa ndio mwisho wa utawala wa Kikwete.
Hatulali mpaka kieleweke
 
Statergies ndio sizioni. Hivi Mnyika humu hayupo?.

Uhamasishaji.

Kabla tujihoji yafuatayo.

Nia tunayo?

Sababu tunazo?

Uwezo tunao?

Bila hayo matatu, tutahitaji wajukuu zetu kuyaleta mabadiliko tunayoyatamani sasa.
 
Maandamano - yawe ni ya kupongeza au kupinga/kutokubaliana na vitendo vya watawala - ni HAKI YA MSINGI ya binadamu. Ni sehemu ya demokrasia. Kwa bahati mbaya magamba na serikali yao bado wana hangovers za enzi cha chama kushika hatamu.

Kinachoendelea katika jamii yetu sio mapinduzi (revolution) bali ni mchakato wa mageuzi (evolution).

Maandamano tunayoyashuhudia na piga ua ya policcm ni sehemu ya mchakato huo. Ni vigumu kutabiri ni lini mchakato utafikia ukomo. Kwa hiyo tuunge mkono kila hatua inayofanywa na vijana - ndogo na kubwa. Kila hatua ni tofali la ukuta wa mageuzi.

Inawezekana kabisa huo ukuta usikamilike katika kizazi hiki. Vijana fyatua matofali hadi kieleweke.:hatari:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom