Serikali inafukuza wataalamu ili iweje?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Serikali inafukuza wataalamu ili iweje?


picture-10.jpg

Na Mwandishi Maalum - Imechapwa 11 July 2012

Gumzo la Wiki
Mwanahalisi


HISTORIA ya madai ya haki katika ujira na mazingira bora ya kazi kwa madaktari nchini hii hapa. Unganisha vipande vya makala hii ili ujue kinachoendelea…
MIGOMO YA MADAKTARI

  1. 2001 mgomo mkubwa wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba Muhimbili wakishinikiza uboreshwaji wa mazingira ya kusomea; hasa masomo kwa vitendo.
  2. 2005 mgomo mkubwa wa madaktari wa hospitali ya Muhimbili na sehemu nyingine wakidai uboreshwaji wa maslahi yao
  3. 2011 vuguvugu la mgomo wa madaktari
  4. 2012 mgomo wa sasa ambao umekuwa ukiendelea



  1. Tamko la madaktari Tamko la jumuiya ya madaktari Tanzania lililotolewa 28 Juni 2012 linasema:
    1. Madaktari wamechoka kuona huduma za afya nchini zikizidi kudorora mwaka hadi mwaka
    2. Tumechoka kuona wagonjwa wakilala chini na watoto wakilala wanne katika kitanda kimoja
    3. Tumechoka kuona msongamano mkubwa wa wagonjwa katika hospitali zetu huku kukiwa hakuna mpango wowote wa uboreshaji…
    4. Tumechoka kuona wagonjwa wakikosa dawa, vipimo sahihi na watumishi wa afya wakifanya kazi katika mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma…
    Kwahiyo, kwa moyo wetu leo, tumejitolea kutetea uboreshaji wa sekta ya afya ….''Madai ya awali
    1. Madaktari walisikitishwa na wimbi kubwa la viongozi wa kisiasa na serikali wanaotibiwa nje ya nchi.
    2. Madaktari walibaki kuwa waidhinishaji rufaa za kwenda kutibiwa nje ya nchi; jambo ambali linapunguza nia ya serikali katika kushughulikia kero za afya za wananchi kwa kuwa watawala wana uhakika wa matibabu nje ya nchi.
    3. Hali hii inaondoa usawa wa kimatibabu kati ya viongozi na wananchi, na serikali hutumia fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kuboresha sekta ya afya hapa nchini

    Nchini Malawi

    Kifo cha Rais Bingu wa Mutharika, kutokana na shinikizo la damu, tarehe 5 Aprili mwaka huu, kilihusishwa, kwa kiwango kikubwa, na serikali yake kushindwa kuboresha miundombinu na huduma za afya nchini mwake.
    Madhara ya upungufu wa dawa na vifaa vya tiba
    1. Uzito huwekwa katika kushughulikia wagonjwa waliozidiwa au walio na dharura pekee, hali ambayo inajitokeza katika zahanati na vituo vingi vya afya.
    2. Kuongezeka kwa usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa kutokana na kupata kiasi kidogo cha dawa
    3. Kuongezeka kwa madhara ya magonjwa yatokanayo na kutopata tiba sahihi (complications); kama ulemavu kwa watoto ambao wamekosa tiba sahihi ya malaria
    4. Kuongezeka kwa malalamiko kutoka kwa wananchi dhidi ya watumishi wa afya
    5. Kupungua kwa morali ya kazi kwa watumishi wa afya na kufanya kazi kinyume na misingi au maadili ya kitaalamu
    6. Kujitokeza kwa mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma.
    Upungufu wa vifaa
    Shirika la Sikika lilifanya uchunguzi mwaka 2011 katika wilaya sita (6) za mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na Dodoma.
    Kati ya vituo 38 vinavyotoa huduma kwa watu waishio na VVU (Care and Treatment Centers), ni vituo 13 tu vilivyokuwa na mashine za CD4+ zinazotumika kuangalia maendeleo ya tiba kwa watu waishio na VVU.
    Kati ya mashine hizo 13, ni tano (5) to ndizo zilikuwa zikifanya kazi. Hali ikoje mikoa mingine nchini? Bila shaka mbaya.

    Vifo vya wagonjwa
    • Tanzania hupoteza takribani asilimia 6% ya wagonjwa wanaohitaji huduma za CT Scan (chombo cha kuchunguzia magonjwa mwilini) kwa mwaka.
    • Kifaa cha CT Scan katika hospitali ya Muhimbili kimeharibika kwa zaidi ya miezi saba sasa bila matengenezo.
    • Wagonjwa wanaohitaji majibu ya kipimo hicho ili wapate tiba stahili, kwenda katika hospitali binafsi. Gharama za kipimo hicho katika hospitali ya Muhimbili ni takribani Sh. 170,000/= lakini katika hospitali binafsi ni kati ya Sh. 200,000 na 500,000.
    • Mbunge mmoja amesema bungeni hivi karibuni kuwa gharama ya kununua CT Scan inalingana na bei ya gari moja la kifahari (shangingi) serikalini.
    Madai ya mishahara na posho rasmi kitaaluma
    1. Uboreshwaji mapato yao ikiwa ni pamoja na mishahara
    2. Psho ya kuitwa kazini baada ya saa za kazi (on call allowance)
    3. Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu (hardship allowance)
    4. Posho ya makazi
    5. Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (risk allowance)
    6. Chanjo ambayo ni muhimu ili kuzuia uwezekano wa madaktari kupata magonjwa ambayo wanaweza kuyasambaza kwa wagonjwa wengine ambao tayari wana matatizo yao ya kiafya.
    Ulinganisho wa mishahara
    1. Kwa sasa, mshahara wa daktari ni Sh. 957,700/= na baada ya makato ya kodi hubaki na Sh. 680,000/= kwa mwezi.
    2. Ufuatiliaji wa shirika la Sikika wa Desemba 2011 hadi Januari 2012, ulikuta:
      1. Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam: Hakuna daktari anayepata mshahara chini ya Sh. 2 milioni (kabla ya makato)
      2. Hospitali ya Agha Khan, pia ya Dar es Salaam, daktari mwenye uzoefu wa chini ya miaka minne alikuwa akilipwa Sh. 1.8 pamoja na mafao mengine kama vile bima ya afya, posho ya nyumba.
      3. Madaktari wamependekeza kiwango cha kulipwa; lakini serikali imekataa kutoa kiwango inachoona inaweza kulipa, hadi rais alipotamka kuwa asiyetaka mshahara wa sasa atafute kwingine.
    Madai ya Posho

    Katika madai yao, madaktari wamependekeza, pamoja na mshahara, wapewe viwango vifuatavyo kwa posho mbalimbali (zinatambulika duniani kitaaluma na pengine kisheria):
    1. posho ya muda wa ziada wa kazi (call allowance) asilimia 5% ya mshahara kama ilivyo kisheria kwa kada yoyote;
    2. posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu asilimia 40% ya mshahara;
    3. posho ya makazi asilimia 40% au nyumba kama ilivyo kisheria
    4. posho ya kufanya kazi katikmazingira hatarishi asilimia 30%
    5. Au chanjo (Homa ya ini-hepatitis, HIV/AIDS, TB) Hapa serikali ilikuwa na nafasi ya kufanya majadiliano.



  1. Hoja, ukaidi wa serikali
    Serikali imeendelea kusisitiza kuwa kuna ufinyu wa bajeti na kwamba, kuwaongezea mishahara madaktari peke yao kutaondoa ulinganifu na kuongeza migogoro katika sekta nyingine.
    Hata hivyo, sehemu ya sheria ya kazi ya mwaka 2004 (Employment and Labour Relations Act, Kifungu cha 6 (20) (4)), inasomeka hivi:
    "Mwajiri atamlipa mwajiriwa walau 5% ya mshahara wa msingi wa mwajiriwa kwa kila saa aliyofanya kazi usiku''
    Kwa hesabu rahisi, daktari alipaswa kupata angalau Sh. 47,000/= kwa saa anapofanya kazi usiku. Serikali imekataa kufuata sheria yake.
    Katika nchi ya jirani ya Kenya, madaktari, wataalamu wa kinywa na wafamasia wanalipwa Sh. 38,000/= kama posho ya ‘call allowance.'
    Hali hii inaweza kusababisha wataalam wengi nchini kukimbilia nje, hasa wakati huu wa soko huria la ajira katika Shirikisho la Afrika Mashariki.

    Bajeti ya sasa 2012/213:
    1. Uendelezaji rasilimali watu Sh. 23.4 bilioni
    2. Matumizi ya kawaida Sh. 24.5 bilioni.
    3. Kati ya fedha iliyotengwa kuendeleza rasilimali watu, Sh. 21.6 bilioni (asilimia 92.3%) ahadi ya msaada wa wafadhili.
    Hali hii ya utegemezi inapingana na Sera ya Afya ya Taifa inayotaka serikali iwe mfadhili mkuu wa sekta ya afya.

    Mpangomkakati

    Mpangomkakati wa sekta ya afya (Health Sector Strategic Plan III) umeweka malengo ya bajeti ya sekta ya afya kufikia asilimia 10 ya bajeti yote ya serikali mwaka 2015.
    Hii inapingana na azimio la Abuja (asilimia 15) ambalo rais wa Tanzania alitia saini. Inapingana pia na sera ya afya ya mwaka 2007 inayosema, ‘Serikali itaendelea kuongeza bajeti ya sekta ya afya …hadi kufikia azimio la Abuja….ili kukidhi mahitaji muhimu ya kisekta.'
    Hii inadhihirisha kuwa serikali haina nia ya dhati ya kusimamia maamuzi yake katika ngazi za kimataifa na kitaifa.

    Maandalizi ya wataalamu

    Kwa miaka kadhaa sasa, idadi kubwa ya wanafunzi wa shule katika ngazi za chini imeendelea kuyakimbia masomo ya sayansi na wanafunzi wanaodahiliwa kusomea masomo ya udaktari ni wale ambao kiwango chao cha ufaulu katika masomo ya fizikia, kemia na biologia kiko juu sana, hivyo madaktari kulipwa mishahara mikubwa ili waweze kuokoa maisha ya Watanzania si tatizo…

    Serikali na matumizi yasiyo ya lazima
    1. Sh. 684 bilioni 2008/09
    2. Sh. 530 bilioni 2009/10
    3. Sh. 537 bilioni 2010/11.

    Posho serikalini:

    1. Sh. 171 bilioni 2008/09
    2. Sh. 269 bilioni 2010/11
    3. h. 155 bilioni 2008/09 (kusafiri ndani na nje ya chi)
    4. Sh. 124 bilioni 2010/11
    5. Sh. 15.3 bilioni 2010/11 pekee: Ununuzi wa magari ya serikali
    6. Zaidi ya Sh. 1 bilioni katika wizara ya afya wakati wa sherehe za NaneNane.
    7. Katika sekta ya afya pekee, matumizi yasiyo ya lazima yaliongezeka toka Sh. 16.1 bilioni mwaka 2010/11 hadi Sh. 22 bilioni mwaka 2011/12, na inakadiriwa kufikia Sh. 25 bilioni mwaka 2012/13, huku posho mbalimbali zikiongoza katika matumizi.

    Taarifa za CAG

    Taarifa za mkaguzi na mdhibiti wa fedha za umma (CAG) zinabainisha:
    1. Msamaha wa kodi uliongeze ka toka Sh. 680 bilioni mwaka 2009/2010 hadi Sh. 1.016 trilioni kwa mwaka wa 2010/11. Hii inawakilisha asilimia 18% ya makusanyo yote ya Pato la Taifa na ni kiwango kikubwa sana kuliko nchi nyingi za Afrika.
    2. Sh. 8 bilioni zimeelezwa kuwa matumizi yasiyokusudiwa
    3. Sh. 31 bilioni zimelipia vifaa ambavyo havikufika; na
    4. Sh. 1.4. bilioni ni malipo yanayotia shaka
    Fedha hizi zingeelekezwa katika maeneo ya afya, tusingesikia mgomo wala maandalizi ya mgomo wa walimu.

Rasimali watu katika Sekta ya Afya


  1. Shirika la Afya Duniani linataka kuwepo daktari mmoja kwa wajongwa 5,000 (1:5,000).
  2. Wakati wa kupata uhuru walikuwa daktari mmoja kwa watu 300 (1:300)
  3. Mwaka 2010 daktari mmoja kwa wagonjwa 30,000 (1:30,000)
Hata waliopo, ambao hawatoshi, wanapofukuzwa, lini taifa litafikia viwango hivyo?

Mpango wa kukuza rasilimali watu unaoisha 2013



  1. Bajeti ya jumla ya mpango huo ilikiwa Sh. 470 bilioni ambazo ni wastani wa Sh. 91 bilioni kwa mwaka.
  2. Mwaka 2011/12, wizara ya afya na ustawi wa jamii iliomba Sh. 66.3 bilioni ili kutekeleza mkakati wa rasilimali watu kisekta
  3. Serikali ilitenga Sh. 13.2 bilioni tu.
  4. Hadi Januari 2012, asilimia 20% tu (Sh. 2.7 bilioni) ndiyo ilikuwa imetolewa kwa wizara.
Wataalam watapatikanaje kwa njia hii ya "bajeti hewa?"

Muhimu sana

Serikali inaweza kuboresha huduma za afya na maslahi ya wafanyakazi kwa:

  1. Kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima
  2. Kudhibiti ufujaji wa kodi za wananchi kwa baadhi ya watendaji wake
  3. Kupunguza misamaha ya kodi
  4. Kutekeleza kikamilifu mikakati iliyo katika sera zake.
  5. Serikali iache kutumia vitisho na ubabe katika kutatua mgogoro wake na madaktari; badala yake ifanye mapatano na wataalamu hawa muhimu
  6. Ubabe na vitisho vinapunguza morali na ufanisi wa madaktari kiutendaji na pengine kupelekea wengine kuhama sekta ya afya au kukimbilia nje ya nchi. Sehemu kubwa ya andishi hili imetokana na utafiti wa SIKIKA – shirika lisilo la kiserikali linalofuatilia upatikanaji huduma bora za afya. Imewekwa katika mafungu ili kurahisisha usomaji.

 
Back
Top Bottom