Serikali ina mipango, mikakati na sera katika kuinua uchumi

Salas

JF-Expert Member
Feb 15, 2009
382
82
Maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana, fikra huru haziwezi kuibishana katika hii hoja, Kwa mujibu wa serikali tawala ukianagalia mipango mikakati na sera zote zinathibitisha hili kwa uwazi mkubwa. Narudia tena na pia nasisitizia, Rais wa Jamhuri anahujimia na watendaji wake, haiingii akilini kwa waziri mwenye dhamana kukaa kimya wakati nchi inaingia kwenye uhaba wa mafuta katika uzandiki Mkubwa.

Msaliti namba moja wa Kikwete ni Ngeleja, Waziri mkuu to mention the few.... Haiwezekani baba ajue kuwa chumvi jikoni imeisha au ped za bintie zimeisha wakati mama na housegirl wapo, Huu ni usaliti na lazima ukemewe, haiwezekani Ngeleja kubali yaishe.

Wassira kitendo chako cha kulala bungeni kimenikwaza sana, lazima ujipime na ujiwajibishe mwenyewe, Haiwezekani serikali iitwe legelege na nyie watendaji mpo, leo mmeambiwa mnafikiri kwa makalio kesho mtaambiwa vikao vyenu mnaendesha kwa ndoto, kwani uongo si mnalala tu halafu rais anaonekana hafai.

Mabadiliko ni lazima, lazima watu wajiwajibishe wenyewe, Nape uko wapi wewe, mbona nawe unakuwa kama unachuki binafsi na watu kwenye mambo ya msingi kama haya ya kitaifa unakaa kimya nadhani unahujumu chama.................Lazima vijana warejeshwe kundini.

Mwisho wa siku uchadema na UCCM na UVINGINE huondoka bali maslahi ya TAIFA TU!
 
Back
Top Bottom