Chipsi yaipembeni
Senior Member
- Jan 8, 2015
- 128
- 90
Wakuu,
Katika kupitia mitandao mbalimbali ili kupata habari mbili tatu, nilikutana na hii ambayo imeandikwa na Gazeti Mtandao la FikraPevu.
Eti hapa nchini Serikali imekosa kampuni inayoweza kubomoa majengo marefu ikiwemo lile lililopo katikati ya Jiji la Dar es salaam ambalo liliamriwa na Serikali yenyewe kuwa libomolewe kwa muda wa karibu miaka mitatu sasa.
Ninajiuliza kuwa, hivi kama hili jengo lingebomoka jana au leo, hiyo hasara ya raslimali watu na mali zilizopo pale zitalipwa na nani? Kwanini miaka yote hiyo tangu walivyounda tume yao haikulishughulikia hili jambo kwa kina hadi sasa tunaona danadana za Serikali?
===================

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema Serikali imelazimika kutangaza tenda kwa kampuni zilizo nje ya nchi zenye wataalamu wenye vifaa vinavyoweza kutumika kubomoa majengo marefu ili kubomoa jengo la ghorofa 16, lililopo makutano ya barabara za Indira Gandhi na Morogoro, katikati ya jijini la Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, hatua hiyo inafuata baada ya Tanzania kukosa wataalamu hao kwa kipindi kirefu, baada ya jengo hilo lililobaki likiwa limesimama baada ya jengo pacha lingine kuporomoka mwaka 2013 na Serikali kuagiza jengo hilo pia libomolewe kutokana na kujengwa chini ya viwango.
Jengo hilo bado limeendelea kusimama hali inayozidi kuwatia hofu wananchi wanaoishi pamoja na kufanya shughuli zao za kiuchumi katika maeneo yanayozunguka jengo hilo.
Amesema kutokana na tatizo hilo, Serikali imeamua kutangaza zabuni kwa kampuni za mataifa mengine ili kuepuka madhara kwa jamii wakati wa ubomoaji wa jengo hilo.
Amesema jengo hilo lipo katika kiwanja kinachomilikiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) jirani na jengo lililoanguka na kuua watu 21 hivyo lazima libomolewa na wataalamu kwa kutumia vifaa maalumu.
Alifafanua kuwa, licha ya jengo hilo kuwa chini ya kiwango, pia liko karibu na majengo mengine matatu pamoja na Msikiti hivyo ubomoaji wake unahitaji utaalamu wa hali ya juu na vifaa vinavyoweza kumtahimili uzito wa mabaki ya jengo hilo.
Waziri Lukuvi, amekaririwa na FikraPevu akisema ukosefu wa vifaa mbalimbali vya kubomoa majengo marefu nchini umekuwa ukiigharimu Serikali kiasi kikubwa cha fedha, kutokana na kulazimika kutafuta wataalamu wa vifaa kutoka mataifa mengine.
Taarifa kutoka ndani ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, zinaeleza kwamba, ipo kampuni ambayo ilipewa dhamana ya ubomoaji wa jengo hilo tangu mwanzoni mwa mwaka huu lakini haieleweki ni kwanini utekelezaji wake umesuasua – sua hadi Waziri mwenye dhamana alipoamua kuingilia kati suala hilo.
Jengo hili lipo katika Mtaa wa Indira Gandhi Dar es Salaam linatarajiwa vuvunjwa wakati wowote kuanzia sasaKampuni kutoka China inayojulikana kwa jina ERJE imetajwa na Afisa mmoja kutoka katika Ofisi hiyo ya Mkuu wa Mkoa (hakutaja jina lake litajwe) kuwa miongoni mwa kampuni ya 5 zilizotuma maombi katika mamlaka husika kuomba kufanya kazi hiyo, ingawa alishindwa kuithibitishia FikraPevu kwamba ni kwanini kampuni hiyo haikuanza kufanya kazi hiyo tangu makubaliano hayo yafanyike.
Soma zaidi | =>Serikali yatangaza Zabuni kwa Kampuni za Ujenzi Nje ya Nchi kubomoa Jengo la Ghorofa 16 Dar