Serikali imepata ugonjwa mbaya

Loooooh! WaTanzania lipi jema kwetu? miaka yote tunalalamika kuwa serikali haina utashi wa kisiasa kuhamia Dodoma leo JPM amepata huo utashi badala ya kumpongeza tunalalamika wamekurupuka. Black people got problems, big problems.
1469603731819.jpg
 
Viongozi wengi wanajua kuhamia Dodoma ni wao ma familia zao huku idara zote za wizara kubaki dar ndio maana wanatoa matamko yao tusubiri ila najua idara zitabaki dar kuhamisha wafanyakazi wote kwa pamoja siyo kitu kidogo Na kwa bajeti yetu hii ngoja tusubiri muda ndio utaamua maana najua 2018 to 2020 ndio miaka ya kujipendekeza kwa wananchi kuanza kutekeleza hahadi ni kutaka watu waishi kama malaika tena baada ya kuishi kama mashetani
 
Huko tuendako ni kubaya...

Walioweka mfumo wa utawala wa sheria na mgawanyo wa madaraka na majukumu walifanya hivyo kutokana na uzoefu na shida zilizopata kutokea
Nasikitika kusema kuwa tunachanja mbuga kuelekea vichakani na hatari ni kubwa kwakuwa vichaka vina mengi.

Sasa hivi hakuna mipango thabiti ya tulipo na tunakoelekea, akiongea tu Mkuu wa nchi serikali nzima inalipukia huko...tushukuru Mungu mpaka sasa hakuna matamko mabaya sana....lakini hatujui ya kesho...huwezi jua ataamka kesho aseme nini....!

Kwenye mkutano wa kukabidhiwa uenyekiti wa chama pale Dodoma mkuu aliweka nadhiri ya kuhamia Dodoma kabla ya kipindi chake cha kuongoza kwisha...bado ana miaka minne na miezi miwili.

Kilichofuatia ni matamko ya mlipuko toka kwa watendaji wake...waziri mkuu akasema atahamia Dodoma mwezi wa tisa, lakini jana waziri Chizeba (kilimo?)akasema yeye atahamia wiki jayo na magazeti yakalipuka na Chizeba ampiga bao waziri mkuu (sort of comedians).

Tusubiri matamko zaidi toka kwa wengine usishangae hata wakuu wa mikoa na wilaya nao wakatoa matamko ya kuhamia Dodoma .

Mkuu wenu kasema akishahamia Dodoma wengine watafuata..! Sasa haraka ya nini? Sifa au nidhamu ya woga? Kumbukeni kuhamisha wizara ni tofauti kabisa na kuhamisha familia..!

Kuna mengi ya muhimu ya kufanya kwa sasa acheni hizo

UKIHAMISHWA DODOMA DAI RISITI
 
Mshana jn, hoja yako ni nzito. Uamuzi wa kuhamia Dodoma ulifikiwa 1973 na waziri mkuu wa wakati huo, Rashidi Kawawa alinukuliwa na Daily News akisema, "The decision to move the govn't seat to Dodoma is irreversible". Mpaka hapo hakuna tatizo na pia isingekuwa mara ya kwanza serikali kuhama. Mwaka 1891 ilihamia Dar kutoka Bagamoyo. Kwa zaidi ya miaka 40 sasa watawala wamekuwa wanakumbuka suala la kuhamia Dodoma pale tu wanapokuwa Dodoma! (Labda kuna mtaji fulani wa kisiasa unapatikana kwa kufanya hivyo). Hakujawa na mikakati na mipango thabiti ya kuhamia Dodoma! Kwa mfano, ilimshinda nini Magufuli kufanya suala la kuhamia Dod katika miaka 5 ijayo agenda yake ya kampeni mwaka jana au hata kulizungumzia kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa bunge ili baadaye lipangiwe bajeti? Tuchukulie kuna majengo tayari Dod kwa ajili ya wizara zote. Je hizo fedha (mabilioni) za kuhamisha maelfu ya wafanyakazi, familia zao na mizigo yao (personal effects) zitatoka wapi wakati tayari bajeti ya mwaka huu ina nakisi ya zaidi ya 45%?
 
Nimeshangazwa mno na baadhi ya replies nilidhani ugonjwa huu upo serikalini tu kumbe mpaka kwa wananchi tena wenye title za great thinkers

Iko hivi uhamisho wa serikali kwenda mahali parakapojulikana kama makao makuu ya nchi, ambapo shughuli na maamuzi mengi ya nchi yatafanyika

.Hapo ndipo wageni wote wa kitaifa na kimataifa watapokelewa ...Airport yetu inakidhi hiki kigezo? Eneo iliyopo kwa sasa ni sahihi ?

.wizara nyingi kwasasa zina ofisi ndogo je kuna mkakati gani wa kujenga ofisi kubwa zitakazotosheleza matumizi au ndio utarudi mtindo wa misururu kama zamani? Bajeti ya ujenzi je?

.Makao makuu ya jeshi TISS na polisi yako Dar bado hapo itakuwaje? Tukumbuke hizi ni organs very sensitive bila kusahau bank kuu nk

. Miundombinu ya Dodoma iliyopo kwasasa je inakidhi viwango vya kuwa na makao makuu ya nchi?

Narudia tena hatuhamishi familia tunagmhamisha kitu chenye impact kwa nchi na wananchi kwa ujumla

Kilichotakiwa ni mkuu wa nchi kuweka mpango mzima wa kuhamia Dodoma kisha kukabidhi wizara husika ama kutengeneza timu itakayotimiza hilo jukumu kwa muda utakaokubalika, kuongea tu kuwa utahama na watendaji nao kukurupuka kuhama ni tatizo kubwa kiutendaji

Hatuandiki haya kwa sababu ya UKAWA, bali kwa maslahi mapana ya nchi na dhana ya mgawanyo wa madaraka
Mkuu wa nchi asiwe ndio kila kitu ni hatari
 
Kwa hiyo nyie chadema hata hili la kuhamia Dodoma mnalipinga ??

Nakumbuka Mbowe na Lowasa wakati wakiomba kura Dodoma waliahidi serikali ya UKAWA itahamia Dodoma haraka Mara tu baada ya kuapishwa.
Je mlikuwa mnawadanganya watanzania??

Kwa unafiki wenu huu mnafaa kweli kuongoza hata mtaa??
Umesoma kwa makini nilichoandika lakini? Au umekurupuka tuu?

Hahahahahaha, mzee anahamia dodoma,bahari anaiogopa kama mmasai bwana, au siku hizi zile honi za bwaaaaaaaaa za meli za makontena hazipo tenaaaaa??? akisikia sauti anauliza, vijakazi wake wanamwambia mzee hiyo ni AZAM MARINE
 
Mshana jn, hoja yako ni nzito. Uamuzi wa kuhamia Dodoma ulifikiwa 1973 na waziri mkuu wa wakati huo, Rashidi Kawawa alinukuliwa na Daily News akisema, "The decision to move the govn't seat to Dodoma is irreversible". Mpaka hapo hakuna tatizo na pia isingekuwa mara ya kwanza serikali kuhama. Mwaka 1891 ilihamia Dar kutoka Bagamoyo. Kwa zaidi ya miaka 40 sasa watawala wamekuwa wanakumbuka suala la kuhamia Dodoma pale tu wanapokuwa Dodoma! (Labda kuna mtaji fulani wa kisiasa unapatikana kwa kufanya hivyo). Hakujawa na mikakati na mipango thabiti ya kuhamia Dodoma! Kwa mfano, ilimshinda nini Magufuli kufanya suala la kuhamia Dod katika miaka 5 ijayo agenda yake ya kampeni mwaka jana au hata kulizungumzia kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa bunge ili baadaye lipangiwe bajeti? Tuchukulie kuna majengo tayari Dod kwa ajili ya wizara zote. Je hizo fedha (mabilioni) za kuhamisha maelfu ya wafanyakazi, familia zao na mizigo yao (personal effects) zitatoka wapi wakati tayari bajeti ya mwaka huu ina nakisi ya zaidi ya 45%?
Unajua watu dhana nzima ya kuhamia Dodoma wengi hawajaielewa au wanajitia uchizi tu hao..Mkapa alishindwa baada ya kuletewa road map yenye bajeti ya kutisha akaahirisha...!
Huyu ndugu yetu huyu na wafuasi wake Mh ....labda watatumia super natural powers....!!!
 
Nimeshangazwa mno na baadhi ya replies nilidhani ugonjwa huu upo serikalini tu kumbe mpaka kwa wananchi tena wenye title za great thinkers
U
Iko hivi uhamisho wa serikali kwenda mahali parakapojulikana kama makao makuu ya nchi, ambapo shughuli na maamuzi mengi ya nchi yatafanyika
.Hapo ndipo wageni wote wa kitaifa na kimataifa watapokelewa ...Airport yetu inakidhi hiki kigezo? Eneo iliyopo kwa sasa ni sahihi ?
.wizara nyingi kwasasa zina ofisi ndogo je kuna mkakati gani wa kujenga ofisi kubwa zitakazotosheleza matumizi au ndio utarudi mtindo wa misururu kama zamani? Bajeti ya ujenzi je?
.Makao makuu ya jeshi TISS na polisi yako Dar bado hapo itakuwaje? Tukumbuke hizi ni organs very sensitive bila kusahau bank kuu nk
. Miundombinu ya Dodoma iliyopo kwasasa je inakidhi viwango vya kuwa na makao makuu ya nchi?

Narudia tena hatuhamishi familia tunagmhamisha kitu chenye impact kwa nchi na wananchi kwa ujumla
Kilichotakiwa ni mkuu wa nchi kuweka mpango mzima wa kuhamia Dodoma kisha kukabidhi wizara husika ama kutengeneza timu itakayotimiza hilo jukumu kwa muda utakaokubalika, kuongea tu kuwa utahama na watendaji nao kukurupuka kuhama ni tatizo kubwa kiutendaji
Hatuandiki haya kwa sababu ya UKAWA, bali kwa maslahi mapana ya nchi na dhana ya mgawanyo wa madaraka
Mkuu wa nchi asiwe ndio kila kitu ni hatari

WATAKAOSHINDWA KUHAMIA DODOMA TUTAWAPA RISITI PIA WASIKANYAGE TENA DODOMA.:D:D:D:D:D
 
Huko tuendako ni kubaya...

Walioweka mfumo wa utawala wa sheria na mgawanyo wa madaraka na majukumu walifanya hivyo kutokana na uzoefu na shida zilizopata kutokea
Nasikitika kusema kuwa tunachanja mbuga kuelekea vichakani na hatari ni kubwa kwakuwa vichaka vina mengi.

Sasa hivi hakuna mipango thabiti ya tulipo na tunakoelekea, akiongea tu Mkuu wa nchi serikali nzima inalipukia huko...tushukuru Mungu mpaka sasa hakuna matamko mabaya sana....lakini hatujui ya kesho...huwezi jua ataamka kesho aseme nini....!

Kwenye mkutano wa kukabidhiwa uenyekiti wa chama pale Dodoma mkuu aliweka nadhiri ya kuhamia Dodoma kabla ya kipindi chake cha kuongoza kwisha...bado ana miaka minne na miezi miwili.

Kilichofuatia ni matamko ya mlipuko toka kwa watendaji wake...waziri mkuu akasema atahamia Dodoma mwezi wa tisa, lakini jana waziri Chizeba (kilimo?)akasema yeye atahamia wiki jayo na magazeti yakalipuka na Chizeba ampiga bao waziri mkuu (sort of comedians).

Tusubiri matamko zaidi toka kwa wengine usishangae hata wakuu wa mikoa na wilaya nao wakatoa matamko ya kuhamia Dodoma .

Mkuu wenu kasema akishahamia Dodoma wengine watafuata..! Sasa haraka ya nini? Sifa au nidhamu ya woga? Kumbukeni kuhamisha wizara ni tofauti kabisa na kuhamisha familia..!

Kuna mengi ya muhimu ya kufanya kwa sasa acheni hizo

Watoto wa mujini wanaita "Miripuko ya Sifa"!
 
Tanzania,na watanzania ni wapevu kimakwelikweli...! Serikali iliyochaguliwa na watanzania, inaakisi upevu wao...sasa tofauti ni kujiliwaza kwa "wafuasi", wa walioshindwa 25/12/2015!
...hakuna kukurupuka!
...serikali inahamia Idodomya kabla ya 2020, na asiefurahishwa na hilo, akale malimao!
Malimao huwa hayaliwi
 
Huko tuendako ni kubaya...

Walioweka mfumo wa utawala wa sheria na mgawanyo wa madaraka na majukumu walifanya hivyo kutokana na uzoefu na shida zilizopata kutokea
Nasikitika kusema kuwa tunachanja mbuga kuelekea vichakani na hatari ni kubwa kwakuwa vichaka vina mengi.

Sasa hivi hakuna mipango thabiti ya tulipo na tunakoelekea, akiongea tu Mkuu wa nchi serikali nzima inalipukia huko...tushukuru Mungu mpaka sasa hakuna matamko mabaya sana....lakini hatujui ya kesho...huwezi jua ataamka kesho aseme nini....!

Kwenye mkutano wa kukabidhiwa uenyekiti wa chama pale Dodoma mkuu aliweka nadhiri ya kuhamia Dodoma kabla ya kipindi chake cha kuongoza kwisha...bado ana miaka minne na miezi miwili.

Kilichofuatia ni matamko ya mlipuko toka kwa watendaji wake...waziri mkuu akasema atahamia Dodoma mwezi wa tisa, lakini jana waziri Chizeba (kilimo?)akasema yeye atahamia wiki jayo na magazeti yakalipuka na Chizeba ampiga bao waziri mkuu (sort of comedians).

Tusubiri matamko zaidi toka kwa wengine usishangae hata wakuu wa mikoa na wilaya nao wakatoa matamko ya kuhamia Dodoma .

Mkuu wenu kasema akishahamia Dodoma wengine watafuata..! Sasa haraka ya nini? Sifa au nidhamu ya woga? Kumbukeni kuhamisha wizara ni tofauti kabisa na kuhamisha familia..!

Kuna mengi ya muhimu ya kufanya kwa sasa acheni hizo
miji hujengwa na maplaners architects na engineers, sidhani kama CDA wanao wataalamu wa kutosha???
 
hata kama tutafanikiwa kuhamia Dodoma, bila mpango madhubuti wa review ya mastetplan ya mji wa Dodoma baada ya muda mfupi matatizo ya Dar yatahamia dodoma
 
Suala lingine ambalo lina changamoto kubwa ni ofisi za kibalozi na mashirika ya kimataifa yenye hadhi ya kibalozi kutakiwa (kulingana na taratibu za kidiplomasia) kuwa pale serikali ilipo. Kuna nchi ambazo ziliwekeza katika miaka ya karibuni katika majengo makubwa ya ofisi zao za kibalozi Dar kama Marekani, EU (Umoja House) na Kenya. Bila shaka kabla ya kujenga walipata uthibitisho kutoka Wizara ya Mambo ya Nje kuwa hakuna mpango wa serikali kuhamia Dodoma. Sasa kuhamia Dodoma limekuwa jambo la dharura. Eti Dodoma kuna shule ngapi za kimataifa kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi katika ofisi za kibalozi?
 
Back
Top Bottom