Serikali imelala, miezi 3 ijayo tunaangamia

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
Miezi 3 ijayo inahisiwa 1 USD($) =TZS 2,500 Ambapo moja ya athari kubwa itakuwa ni kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali kunakotokana na kushindwa kwa sera za kiuchumi ya serikali ya Kikwete.

Serikali imekua ikiimba nyimbo za kuimarisha uchumi bila kuchukua hatua madhubuti.

Poa kama hamtajali tujiandae kuwapinga watawala hawa wa ccm kwakila hali kabla hali haijawa mbaya zaidi.
Ngoja nikanunue Mkate wangu na Sukari .

2nv4iac.jpg
 
Ni wakati sasa Kikwete akamuondoa Mkulo kwenye Wizara ya fedha haraka iwezekanavyo
 
Ni wakati sasa Kikwete akamuondoa Mkulo kwenye Wizara ya fedha haraka iwezekanavyo
Mpita Njia , ni kumuondoa mkolo na mapolicy makers pale BOT, WAMESHINDWA kututoa mahala ambapo hata Balali na aliweza kutusgeza, BOT wamekua wakidanganya kwa takwimu za kuimarika kwa hali ya uchumi ambazo wanasiasa wamekua wakizitumia kutupumbaza.
 
kazi kweli kweli. Mawaziri na watendaji wakuu hawawezi kuamua mpaka wapate mawazo ya mkulu wakati mkulu naye hana maamuzi mpaka awasikilize watendaji wake ambao (inaelekea) hawaamini!

Matokeo yake ni mzunguko usioisha na ugonjwa uliosemwa na 'gamba' mojawapo wa "kukosa maamuzi".

....sijui tumkabidhi Mungu pia jambo hili, sidhani kama 'atakubali' kutusaidia maana uzembe umezidi
 
dah! mkuu jana nimechukua laki 3 tu nimeshindwa kuziweka kwenye wallet, aibu hii, laki 3 jana mchana saizi nina buku 40 tu, chamaana kilichofanyika hamna.

mi nikawa nahisi labda nina matumizi mabaya.kumbe ndo hali halisi ya maisha yalivyo.basi tuiombe serikali kwa kipindi hiki wafanyakazi walipwe kwa dollar.mia
 
Mpita Njia , ni kumuondoa mkolo na mapolicy makers pale BOT, WAMESHINDWA kututoa mahala ambapo hata Balali na aliweza kutusgeza, BOT wamekua wakidanganya kwa takwimu za kuimarika kwa hali ya uchumi ambazo wanasiasa wamekua wakizitumia kutupumbaza.
Kwa kweli wameshindwa kusimamia uchumi. Mkapa alipoondoka aliacha macro economy ikiwa stable, kazi ilikuwa ni kuhakikisha the tricle down of the effect. lakini sasa hivi hata macro economy imeshatetereka kwa kiasi kikubwa; angalia inflation, angalia thamani ya shilingi... it is time the go before things get worse
 
inaumiza sana, inafadhaisha sana unapoona hakuna ndani ya system anaestuka na hali hii, hakuna anaestuka kabisa
 
Hapa Mbeya 25kg za unga wa Azam ilikuwa Tsh 20,000/= mwanzoni mwaka huu sasa ni Tsh 31,500/= Cement ilikuwa Tsh 13500/= sasa ni 16,000/= hadi 17,000/=
 
Hali inatisha kwa kweli, mtu umatoa dola 300 unapata Tsh 530,000.. Serikali inabidi ifanye jambo kurejesha heshima ya shilingi...
 
Kwa kweli wameshindwa kusimamia uchumi. Mkapa alipoondoka aliacha macro economy ikiwa stable, kazi ilikuwa ni kuhakikisha the tricle down of the effect. lakini sasa hivi hata macro economy imeshatetereka kwa kiasi kikubwa; angalia inflation, angalia thamani ya shilingi... it is time the go before things get worse
Ukijaribu kutafakari kwakiana lipo jambo moja dhahiri kuwa Mkuu wa nchi ameyumba , wasaidizi wake hawamuogopi, na kwakua hakuna shinikizo la kutoka juu wasaidizi wake wamerelax, kwakua wasaidizi wake hawa kina Ndulu, kamishna wa TRA, na wengine wamepumzika kwelikweli.

Hii inaathari kubwa kwa watendaji wa chini.

TRA wanakusanya mamilioni kwaajili ya familia zao, haziingii mfuko mkuu, makusanyo yameanguka, serikali imeshindwa kugharimia mambo mengi kupitia mFUKO mkuu.

Tuamke sasa, tuanze kuwapa shinikizo watawala wetu, ili nao wawape shinikizo waliochini yao
.
 
Back
Top Bottom