Serikali imefilisika jamani?

Bangoo

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
5,597
1,005
Kwa wafanyabiashara wengi wa biashara ndogo na za kati watakubaliana nami kuhusu upatikanaji wa sarafu za sh 100 na sh 50.

Kwa kweli tunaiomba serikali itengeneze hizo sarafu kwani tunapata taabu sana ktk biasha tunazofanya,

serikali iache udhaifu kwa kushindwa kutengeneza sarafu mpya!
Haipendezi sana kupuuzia hizi sarafu.
 
Ni mwaka sasa unaenda hizi sarafu hazionekani kwa wingi.
 
heh mbona kwenye daladala zipo nyingi sana hata tsh kumi unaipata kwa wauza sigara,hizo hela zipo tena nyingi tu sema kwa shughuli yako huzipati
 
Wewe bado unaona una serikali? Hapa tumebakia usanii wewe pambana tu kikwako hadi itakapopatinaka serikali. Hawa wenzetu wako busy kutafuta kibembea, mananasi ya kushangalia, mihogo na mengine ya kwenda kukodolea macho na wala hawajui taabu zinazowakabili watanzania. Ni bora wakimbilie vimwana kila kona ya dunia kuliko kuongoza nchi.
Tujizatiti, tujifunze na tutafute serikali itakayotatua kwa makini matatizo ya nchi yetu. Tukiendelea hivi tutajachinjana hapa huku wengine wakijivinjari na mali asili zetu bila huruma.
 
Kwa sasa sh 100 nyingi ni mbovu na huwa zinakataliwa madukani!

Hivi kwa nini mlitengeneza hela mbovu, hebu angalieni 500 zinavyochakaa vibaya kabla ya kutumika!

Mbona hela za nchi nyingine huwa na ubora kuliko huu wa kwetu?

Ee Mungu nchi yetu inaangamia kwa kukosa viongozi wenye maarifa.
 
Back
Top Bottom