Huna makengeza na macho yako yameona hali halisiMimi ninaona kama vile nchi inaongozwa na wahalifu jamani au nina makengeza?
Ukila na WAZEE haliharibiki NENO!
Hiyo ndo Serikali ya awamu ya nne, kama kweli wahe. wabunge walikuwa serious siku wanatoka maazimiop hayo tutaona leo wakikataa upuuzi huu. Huwezi kuwaambia Wabunge makini eti Serikali itazidai fedha ambazo IPTL imelipwa zaidi (itazidai lini? kwanini bado hawajadaiwa?). Wahusika wameandikiwa barua za kujieleza ebo! utafikiri Afisa Mtendaji wa kata anajieleza kwa Mwenyekiti wa Wilaya kumbe PM analijibu bunge. acha tu!!!
Tatizo vyama vya upinzani nao wanaganga njaa zao zao tu, hakuna upinzani wa maana Tanzania, hakuna mikakati yenye maana, wote wamekalia migogoro tu, hatuna mkombozi poor us na CCM haitakuja kubadilika kamwe. Utafikiri tunamkosi!!
Kwa mujibu wa tangazo la spika wa Bunge alilolitoa muda mchache uliopita ni kuwa Waziri mkuu atawasilisha taarifa yake siku ya alhamisi kuhusiana na utekelezaji wa maazimio 21 ya Bunge kuhusiana na Richmond.
Hivyo basi siku hiyo itakuwa ni siku ya kusikia hatua gani zimechukuliwa na nini kinaendelea.
Huenda tukaambiwa tena kuwa serikali inataka hadi April 2009 ili kuweza kutekeleza maazimio hayo ya Bunge.
Hiki kitakuwa ni kipimo kizuri kama kweli serikali inaheshimu muhimili wa Bunge ama laa ,kwani kama itashindwa kutekeleza maazimio ya Bunge ....