hippocratessocrates
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 3,598
- 1,539
- Thread starter
- #41
Kenya Doctors' strike.. the chronicity of the endemic of Global/ Worldwide strike?
Just anxiously waiting for NEWS from Madaktari halisi after their press release.
naona wamelianzisha wenyewe.amsha aliyelala utalala wewe.
Inakuwaje pale anapokuwa na kifaa hana utashi pasipo pesa?
haitakuwa ngumu kama tutaamua,tatizo tuliowapa madaraka(wanasiasa) yaani ni bumbumbu wa kutupwa, na wabinafsi wa kutupwa.
kingine ni hawa maprof na specialist doctors hawana msaada wowote katika kushinikiza mabadiliko kwani wamejaa uwoga , kutokujiamini na unafiki
kwani wewe ni raia wa nchi gani embu soma hii Ilani vizuri kwanza katika suala la AFYA
· kwa Afya: Kuhakisha kwamba kila kijiji kinakuwa na Zahanati, kila Kata inakuwa na Kituo cha Afya, kila wilaya inakuwa na Hospitali, na kila Mkoa unakuwa na hospitali ya Rufaa:
· kuwapatia mafunzo watumishi wake ndani na nje ya nchi; kwa
· kuzipatia vifaa bora na vya kisasa hospitali zetu kama vile mashine za mionzi (LINAC machine) kwa ajili ya tiba ya saratani; kununua mashine za mionzi kama vile CT-Scan na MRI kwa ajili ya upasuaji wa ubongo na mgongo.
· Lengo la kufanya hivyo ni kuwezesha upatikanaji wa huduma mahsusi zinazohitaji vifaa na ujuzi mahsusi zipatikane hapa hapa nchini na hivyo kutolazimika kupeleka watu wetu kutibiwa nchi za nje. Aidha, kuajiri wataalamu zaidi wa afya kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na kuboresha mazingira ya kazi kwa lengo la kuongeza ubora wa huduma za afya. Hospitali za Wilaya zitaendelea kuimarishwa kwa kuzipatia madaktari, wauguzi, dawa na vifaa tiba vya kutosha. Pia tutatoa motisha kwa watumishi ambao wanafanya kazi katika maeneo yenye mazingira magumu ili kuwajengea ushawishi wa kuendelea kutoa huduma za afya katika maeneo hayo. Utaratibu pia utawekwa utakaowezesha wananchi kuwa na Bima ya Afya ili kumudu gharama za matibabu.
Nianze kusema kuwa mimi ni daktari, na ningependa kwa pamoja tusio madaktari na madaktari tujadiliane katika uzi huu, si kwa kuonyesha hisia (hasira,matusi,kejeli n.k), kupoteza muda, kupotosha madai na taarifa na bali kwa kuona mapungufu ya chanzo cha mgomo kabla ya kujadili madhara yake, ili wote kama watanzania(na wasio watanzania pia) kuliweka sawa hili na kulisaidia Taifa.
MADAI NA UFAFANUZI:
-Uwajibishwaji wa watendaji wakuu wa W/Afya
Ufafanuzi: Kutokana na ubadhirifu uliothibitika, hatua za kinidhamu zilipaswa kufuatwa.
-Uboreshwaji wa Huduma za Afya katika hospitali.
Ufafanuzi: Upatikanaji wa vifaa kazi, madawa na mazingira ya Hospitali ili kutoa huduma stahiki wa wagonjwa. Yaani
Upatikananji wa vitendea kazimachine za upimaji moyo, kifua, sukari, uzito, urefu n.k), Mashine za Oxygen, vifaa vya kuongezea maji na damu mwilini n.k .
Upatikanaji wa nyenzo(Machine kama vile CT Scan, MRI, Mashine za mionzi yaani X-ray, mashine za matibabu yaani mionzi ya kutibu saratani)
Mazingira-Kuongeza vitanda, mashuka, huduma za chakula kwa wagonjwa wasio na ndugu n.k
-Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (Risk allowance) 30% au Chanjo
Ufafanuzi: Katika mazingira ya sasa ambapo unaweza kuambukizwa Kifua kikuu(TB), Homa ya Ini (Hepatitis), UKIMWI (HIV/AIDS) tunapaswa kujikinga dhidi ya magonjwa haya tunapokuwa tukitibu wagonjwa na hivyo ni vyema serikali kutoa chanjo au isipowezekana kutoa chanjo na itoe posho tajwa kujikinga, mfano chanjo ya Homa ya ini pekee kwa mwaka ni mara 3 na inagharimu 45,000 (30USD) kwa kila chanjo.
-Posho ya kuitwa kazini(On call allowance)-5%
Ufafanuzi: Kisheria(Sina uhakika na kifungu), Muda wa kuitwa kazini au katika kada/sekta nyingine huitwa Overtime ni asilimia tano(5%) ya mshahara na hivyo, sheria ifuatwe katika hili.
-Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu(Hardship allowance)-40%
Ufafanuzi: Si madaktari wote(yaani madaktari 1500) wafanyao kazi katika hospitali za serikali wanafanya kazi katika mazingira magumu bali, wachache hasa walio vijijini na hivyo, ili kuwapa motisha na kuonyesha njia ya motisha ili madaktari wasibaki mijini tu na hivyo kuwafanya waende vijijini ili kuepuka usumbufu wa wagonjwa kusafiri toka mkoahadi mkoa kwa matibabu, posho ya mazingira magumu itolewe kwa madaktari hawa walio vijijini na si wote.
-Posho ya Usafiri(10%) au mkopo wa magari.
Ufafanuzi: Kwa madaktari wale kukaa mbali na hospitali, wapatiwe posho hii au mkopo wa gari(NA PESA HII IKATWE KATIKA MSHAHARA). Hii ikiwa na maana daktari aliye zamu na anayeishi(mfano) bunju na kufanya kazi Muhimbili, au anayeishi Vikindu na kufanya kazi Amana, anayeishi kimara mwisho na kufanya kazi Temeke nk katika mikoa mingine anayetakiwa kufika usiku saa nane na hakuna usafiri anaweza kufika kwa wakati.
-Posho ya makazi (30%) au kupatiwa nyumba.
Ufafanuzi: Kisheria (Doctor is equal to high government officer and is entitled to a house).Nitapokuwa na vifungu vya sheria nitathibitisha hili. Na kwa kuwa jambo hili lipo kisheria basi na sheria ifuatwe(na ndio Seriakali ilisema inajenga nyumba 700 za madaktari), lakini isipowezekana kwa daktari kupatiwa nyumba(kwa ambao hawana) basi posho ya asilimia 30% itumike kama mbadala.
-Wafanyakazi wote wa Sekta ya Afya wapewe kadi za kijani za bima ya Afya.
Ufafanuzi: Kwa wafanyakazi wa sekta ya Afya yaani madaktari, wauguzi, wafamasia, watu wa maabara, nk. Wapewe bima za Afya wakipata huduma sawa na ile wanayotoa.
-Pendekezo la mshahara kuwa mil. 3.5/=kwa mwezi.
Ufafanuzi: Kama vile mishahara katika Serikali inavyotegemea
*Muda wa masomo wa fani.
*Kiwango cha elimu.
*Ugumu wa masomo wa fani husika.
*Ugumu wa kazi.
*Muda unaotumika kazini.
Hivyo kwa kuzingatia haya, pendekezo la mshahara tajwa utolewe kwa madaktari lakini kama ikishindikana basi Mwajiri(Seerikali) na itoe pendekezo lake.
MAKOSA:
Jumla ya madaktari wote katika hospitali zaSerikali ni 1500, hii ikiwa ni takwimu ya Wizara ya Afya yam waka 2011 na ikijumuisha zaidi ya madaktari 300 waliofukuzwa na 150 waliokwenda nje tayari hadi leo trh 17.07.2012. Hivyo tafsiri iliyotumika ni ;
-Daktari hayuko entitled kupata nyumba kama high government official kama ilivyoainishwa kisheria
-Daktari hatakiwi kulipwa overtime (call allowance)mara baada ya muda wa kazi kwa aslimia tano ya mshahara
-Tafsiri ya kuwa madaktari wote huwa wanakuwa zamu za usiku (overtime) na hivyo kuwekakiasi cha posho tajwa juu kuwa ya madaktari wote na kila siku!
-Tafsiri ya pesa ya mazingira magumu kwa madaktari wote(KWANI SI MADAKTARI WOTE WAKO MAZINGIRA MAGUMU YA VIJIJINI)
-Tafsiri ya kutaka posho ya mazingira hatarishi pekee badala nyenzo za kujikinga na chanjo
-Tafsiri kuwa wafanyakazi wengine wa sekta ya afya hawakujumuishwa katika madai.
-Tafsiri ya pendekezo la mshahara tajwa kuwa ni SHURUTI ya kurudi kazini.
-Tafsiri ya kuwa PENDEKEZO la mshahara haliwezi kupungua!
Jana,Rais Magufuli amejionea taswira ya idara ya afya na huduma kwa wagonjwa. Amewaona wagonjwa wakiwa hawana tiba ila tabu hadi aibu. Amewaona wauguzi wakisema asichokiamini. Taswira inayojaza hasira.
Dr. Stephen Ulimboka alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Taasisi za Madaktari nchini Tanzania. Alikuwa na fikra,hoja na nia za kupigania ubora wa idara ya afya hasa hospitalini. Alitaka maboresho ya maslahi ya matabibu na hata vifaa-tiba viwepo.
Dr. Ulimboka alipigania ustawi. CT-Scan na vifaa vingine vya tiba hospitalini havikuwa vikikauka kinywani mwake. Maboresho na ustawi wa kwenye afya alipambania. Yakampata ya kumpata! Rais Magufuli ameona na kuguswa. Hadi atatumia mshahara wake kumtibu mgonjwa fulani pale Muhimbili, aliyelazwa miezi miwili bila tiba.
Dr. Ulimboka atumike kukumbusha hoja za kitabibu. Rais Magufuli amekuwa shahidi mzuri. Kama Muhimbili kuna hali ile,kwingineko kukoje?
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam