Serikali ifanye mambo haya kumaliza mgomo-Maoni

Kizimkazimkuu

JF-Expert Member
Nov 8, 2007
337
234
Binafsi ni daktari kwa taaluma, na nimepata kufanya kazi katika hospitali za erikali kabla sijaachana na kutibu moja kwa moja na kujiunga na masuala ya afya ya jamii/public health. Sababu zilizonifanya kuondoka ni kudharauliwa, kupuuzwa na kunyimwa stahili zangu (simaanishi mshahara, ila ni zile stahili zilizoainishwa katika mkataba wangu wa ajira kama vile nyumba/au kulipwa kodi ya pango, nk). leo, takribani miaka kumi tangu nimeacha kupractice hali bado ni ile ile, vilio vile vile kutoka kwa madaktari. Ni wazi kuna matatizo.

Tangu kuanza kkwa mgomo serikali(na wakati mwingine vyombo vya habari) imekuwa ikipaza sauti katika dai moja tu la madaktari, na kutaka kuwaonyesha madaktari ni wapenda pesa tu. Hata majuzi akijibu swali la MBOWE bungeni, pinda aliishia kusema "tumetekeleza madai yao wa asilimia kubwa, yamebaki mambo madogo". Hawataki kusema mambo waliyotekeleza ni yepi. Nimejaribu kufuatilia madaktari waliomba nini na serikali wametekeleza nini, nimeona kuna upotoshaji mkubwa unaofanywa na serikali. (hili linahitaji thread ya peke yake). Sasa acha nitoe mapendekezo yangu kwa serikali nini inaweza kufanya na faidi zake kwa serikali, madaktari na wananchi.

1. Madaktari waliomba nyongeza ya mshahara; Kwa kuwa serikali haina fedha za kutosha (au wanaogopa kuamsha madai ya nyongeza za mishahara kutoka katika kada zingine) wanaweza kufanya yafuatayo:-

1.1. Kutambua udaktari, unesi, nk kama ujuzi/utaalamu maalum (special skills) na hivyo kulipa special skills allowance (Hii inafanywa Botswana kwa mfano, ili kuvutia wataalam kwenda kufanya kazi nchini humo)Kwa kuwa hii itakuwa ni posho, haitagusa mabadiliko ya mishahara kwa watumishi wote wa umma

1.2.serikali iainishe mikoa/wilaya zenye uhaba mkubwa wa madaktari (takwimu zilizopo sasa, 55% ya madaktari wote nchini wako DSM) na itoa posho ya kufanya kazi wilaya/mikoa yenye hali hiyo. Hii itawachochea madaktari kwenda mikoani/wilayani na ndugu zetu walioko huko watafaidika, na madokta "wallet zao zitatuna".

2. Madaktari waliomba posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi: serikali ifanye yafuatayo:-
2.1. Serikari na madokta waainishe(criteria) mazingira hatarishi ni yepi na ni kada zipi (in priority order) wanakuwa katika risks zaidi. Kisha wachagua walio katika risk zaidi ianze kuwalipa posho hizo. Pia kuwa na timeline ni lini posho hiyo itatolewa kwa madakatri wote wanaostahili

3. Madaktari waliomba serikali itekeleza makubaliano yaliyomo ktk mkataba wa ajira ya kupatia nyumba au kuwalipia pango. Serikali inaweza kufanya haya:-
3.1.Kwa kuwa serikali imetangaza kujenga nyumba zaidi za madaktari, in the meantime serikali inaweza kuchagua mikoa yenye uhaba wa madokta mf. Mtwara, Lindi, Rukwa, Songea na kusema katika mwaka wa kwanza itahakikisha madaktari katika mikoa hiyo wanapata stahili hizo, na kuwekwe timeline waliosalia watalipwa lini.

4. Madaktari waliomba green card ya matibabu:
4.1. Kwa kuwa mishahara yao (na pengine hata ikiongezwa) haiwaingiza katika category ya kupata kadi hiyo, serika iwaombee waiver kutoka mfuko wa bima ya afya wapewekadi hizo kwa upendeleo maalum (after all, madaktari ndio wanaozalisha mapato ya mfuko huo kwa kuwaona wateja wao)

5. Kuboresha sekta ya afya Nchini:

5.1. Serikali iweke wazi mipango yake ya kuongeza bajeti ya wizara ya afya (watimize makubaliano waliyosaini wakuu wa nchi Abuja, Nigeria ya kutenga 15% ya bajeti kwa Afya).

Mawazo ya jumla:
1. Serikali iangalie uwezekano wa kupata fedha kutoka Global funds (GF) kwa ajili ya kulipa baadhi ya posho (wajifunze Zimbabwe wanafanyaje; wao wameweza kupata fedha kutoka GF kuwalipa posho watumishi wa afya kufuatia inflation iliyopelekea brain drain)
2.Katika kipindi chote cha mazungumzo, serikali iwe wazi kuwa haina fedha....hivyo msingi wa maamuzi yote unaongozwe na ufinyu wa bajeti.

Karibuni tuchangie kuisaidia serikali kuwaondoa wananchi katika kadhia hii, na tuepuka mijadala ya kubomoa....
 
Hayo ni mawazo ya busara sana. Amini usiamini Tz, washauri na wasomi halali wamewekwa benchi,
mf. vyuo vikuu vyetu. Havidhaminiwi ktk kutoa maelekezo ya kimaendeleo kama wakati wa Mwl.
Ila wasio wasomi ndio wanaongoza nchi bila hata kuwa na karisma ya wisdom. La kufanya ni kuishauri srk yetu
siku zote badala ya kutukana tukana ccm/cdm.

Tuzitumie njia hizi za mitandao ya kijamii kuishauri srk kwani sisi ndo tulioko kwenye uwanja wa mapigano.
 
...Katika mgogoro huu,lawama nyingi zinawaendea Pinda na Waziri wa Afya. Pengine tujiulize washauri/wataalamu wanaotakiwa kuwasaidia mawaziri wanafanya kazi yao? Utumishi wametoa ushauri gani? walisikilizwa? Je wizara ya afya wanamsaidi waziri ipasavyo? Anawasikiliza?

Inashangaza kusikia serikali ikisema itatumia hospitali za jeshi, kama vile wanao wataalam wa kutosha huko jeshini. Takwimu rasmi zilizopo zinaonyesha daktari mmoja Tanzania anahudumia watu >20,000 (doctor patient ratio 1:20,000). Maana yake Tanzania kuna madaktari (wenye degree) takribani 2,000 na ushei hivi.

Mimi naamini kuna jambo ambalo hatujaambiwa na serikali kwanini haitaki kuwasikiliza madaktari.
 
...Katika mgogoro huu,lawama nyingi zinawaendea Pinda na Waziri wa Afya. Pengine tujiulize washauri/wataalamu wanaotakiwa kuwasaidia mawaziri wanafanya kazi yao? Utumishi wametoa ushauri gani? walisikilizwa? Je wizara ya afya wanamsaidi waziri ipasavyo? Anawasikiliza?

Inashangaza kusikia serikali ikisema itatumia hospitali za jeshi, kama vile wanao wataalam wa kutosha huko jeshini. Takwimu rasmi zilizopo zinaonyesha daktari mmoja Tanzania anahudumia watu >20,000 (doctor patient ratio 1:20,000). Maana yake Tanzania kuna madaktari (wenye degree) takribani 2,000 na ushei hivi.

Mimi naamini kuna jambo ambalo hatujaambiwa na serikali kwanini haitaki kuwasikiliza madaktari.

haitaki kuwasikilza madaktari kwa kuwa inaamini kuwa madaktari wametumwa na chadema
 
Gama,,,anayefikria hivo hafai kuwa mtawala,au kama ana ushahid atoe kabisaaaa,,,,
 
Last edited by a moderator:
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom