Serikali iazime walinzi wa Chadema (Red Brigade)- Mbowe

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
SIKU moja baada ya magari matano ya Ikulu kuzima baada ya kuwekwa mafuta machafu mkoani Kilimanjaro wananchi wa kada mbalimbali, wakiwamo wanasiasa wameijia juu serikali na hasa Idara ya Usalama wa Taifa kwa hatua hiyo, huku wakihoji ilikuwaje magari ya serikali yajaze mafuta kwenye vituo binafsi.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe Bw. Mbowe alisema kuwa huo ni uzembe wa hali ya juu na kwamba Rais asifumbie macho uzembe huo hata kidogo, kwani kufanya hivyo anayaweka maisha yake rehani.

Pia alisema matukio yanayomwandama Rais Jakaya Kikwete yakiwemo ya gari zake kuzimika ghafla na tairi kupata kuchomoka hivi karibuni na hili la kuwekewa mafuta machafu ni ishara ya kuwa usalama wake uko hatarini, hivyo akashauri 'serikali iazime walinzi wa CHADEMA (Red Brigade) wasaidie katika eneo hilo'.
 
Magari ya JK kuwekwa mafuta feki fedheha

Gladness Mboma, Dar na Martha Fataely, Moshi

SIKU moja baada ya magari matano ya Ikulu kuzima baada ya kuwekwa mafuta machafu mkoani Kilimanjaro wananchi wa kada mbalimbali, wakiwamo wanasiasa wameijia juu serikali na hasa Idara ya Usalama wa Taifa kwa hatua hiyo, huku wakihoji likuwaje magari ya serikali yajaze mafuta kwenye vituo binafsi.

Miongoni mwa waliozungumzia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe ambaye amesema kitendo cha magari ya serikali kujazwa mafuta kwenye kituo binafsi badala ya bohari za serikali kinaibua maswali mengi.
"Tangu lini magari ya serikali yakawekwa mafuta katika vituo vya kawaida wakati wana vituo vyao, je walilipa kwa hundi au fedha taslimu na utaratibu huo ulianza lini,"alioji.

Bw. Mbowe alisema kuwa huo ni uzembe wa hali ya juu na kwamba Rais asifumbie macho uzembe huo hata kidogo, kwani kufanya hivyo anayaweka maisha yake rehani.

Pia alisema matukio yanayomwandama Rais Jakaya Kikwete yakiwemo ya gari zake kuzimika ghafla na tairi kupata kuchomoka hivi karibuni na hili la kuwekewa mafuta machafu ni ishara ya kuwa usalama wake uko hatarini, hivyo akashauri 'serikali iazime walinzi wa CHADEMA (Red Brigade) wasaidie katika eneo hilo'.

Akizungumza na Majira jana Dar es Salaam, Bw. Mbowe alisema kuwa kutokana na matukio hayo wana wasiwasi na usalama wa maisha ya Rais Kikwete.
"Kama imefikia hatua hii tuna wasiwasi na maisha ya Rais wetu tunamuonea huruma, kwani wanamfedhehesha na wahusika hawasemi ukweli juu ya matatizo yanayomkubwa.

"Matukio ya kuzimika kwa gari la Rais, ghafla na tairi kupata pancha (kuchomoka) na jana kuwekewa mafuta machafu wahusika hawasemi, wanafanya siri hiyo ni ofisi ya umma siyo Kikwete, Watanzania wanapaswa kuelezwa kinachoendelea," alisema.

Bw. Mbowe alisema tatizo kubwa ambalo hata wao wenyewe wanashindwa wasaidie vipi ni usiri unaofanywa na utawala mzima wa rais na kwamba hali hiyo imefanya Watanzania washindwe kutoa ushauri.

"Nikisema kuwa utawala hauko makini ni juzi ilipocheza timu ya Brazil na Taifa Stars, wimbo wa Taifa uliimbwa lakini ukazimikia katikati na kurudiwa tena, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa, hiyo ni fedheha kwa nchi," alioji.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa rais sasa ni lazima atambue kuwa Watanzania wananyweshwa mafuta machafu kutokana na bidhaa chafu kuingizwa ndani ya nchi bila kufanyiwa ukaguzi wa kutosha.

Alisema magari ya watu yamekufa injini na mengine yamewekwa juu ya mawe kutokana na mchanganyiko wa mafuta hayo machafu ambayo yamejaa katika vituo mbalimbali nchini."Kumekuwepo na msafara mrefu wa walinzi na viongozi wa serikali katika msafara wa Rais na wanalipwa fedha nyingi, je, wanafanya kazi gani mpaka rais anapatwa na matatizo hayo, kwa nini wanamfedhehesha?" alioji.

Alisema ili kuondoa fedhea hiyo ni lazima Rais hawawajibishe wahusika wote, kwani uenda kuna mgomo, na ndio maana matukio hayo yanajirudia na kumtaka asicheke nao hata kidogo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu wa Chama cha Wananchi (CUF), Bw. Julius Mtatiro alisema kuwa asitafutwe mchawi katika matatizo yanayokumba magari ya rais ikiwemo kuzima na kuwekewa mafuta mabovu, bali Idara ya Usalama wa Taifa ndiyo inayopaswa kubeba lawama hiyo.

"Asitafutwe mchawi, ulinzi wa rais siyo mzuri, kuna udhahifu mkubwa katika masuala ya usalama wa viongozi na inaonyesha wazi kuwa usalama ndani ya nchi hakuna," alisema.
Alisema kuwa kuyumba kwa Idara ya Usalama wa Taifa ndani ya nchi itapeleka Taifa pabaya na kwamba rada iliyokuwa inunuliwe kwa fedha kiduchu imenunuliwa kwa fedha nyingi, hiyo yote inatokana na idara hiyo kutokuwa makini.

Nikisema hakuna usalama wa Taifa ni hakuna kweli juzi kuna mshabiaki aliingia uwanjani kwenda kumkumbatia mchezaji wa Brazil, Usalama wa Taifa, polisi walikuwa wapi, je, kama shabiki angekuwa na kisu akamdhuru mchezaji, Tanzania tungeficha wapi aibu ," alioji.

Bw. Mtatiro alitoa mfano wa CUF kuwa Professa Ibrahim Lipumba siyo Rais, lakini lazima wawe makini kuakikisha kwamba vyombo anavyotembelea vinakaguliwa mara kwa mara na havipati dosari yoyote pindi vinapokuwa safarini.

Mawazo kama ya wanasiasa hao yametolewa pia baadhi ya wafanyabiashara na wananchi wa kawaida mkoani Kilimanjaro, wakiomba serikali kuiwajibisha Idara ya Usalama wa Taifa na maafisa wa serikali mkoani hapa, kwa tuhuma za uzembe unaohatarisha usalama wa Rais Kikwete.

Pamoja na hali hiyo, jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro,limepata kigugumizi kuhusiana na tukio la kuwekwa kwa mafuta machafu katika magari hayo yaliyoandaliwa kwa ajili ya ziara ya Rais Kikwete mkoani hapa iliyomalizika jana.

Wananchi hao Bw. Daniel Ngowi, Martin Mushi na Bw. Abdalah Sudi na wafanyabiashara ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema. Idara ya Usalama wa Taifa na maafisa wa serikali mkoani hapa wanapaswa kuwajibishwa kwani hali hiyo ikiachwa ilivyo huenda rais akadhurika zaidi.

Bw. Ngowi alisema ni vyema kwa idara hizo wakapanguliwa na kuwekwa watu wenye ujuzi na wanaowajibika kikamilifu kwani
hali iliyopokwa sasa inaonyesha watu hao wamebweteka na huenda wakawa hayajui vyema majukumu yao.
“Pamoja na hilo lakini acha serikali ishuhudie yenyewe, tumekuwa tukipiga kelele kuwa tunauziwa mafuta machafu lakini hakuna
jambo linalofanywa na EWURA…huo ni mfano tosha ili sasa waamke kutoka usingizini,” alisema Ngowi.

Akielezea baadhi ya mbinu zinazofanywa na wamiliki
wa vituo vya mafuta, mfanyabiashara mmoja alisema, wamiliki hao huchanganya lita 10,000 za Petrol na lita 500 au zaidi za mafuta ya taa ili kujipatia faida zaidi.
“Wanachotafuta ni faida ya ziada, ukiangalia bei ya lita moja ya petrol ni sh. 1,770 na bei ya mafuta ya taa ni sh. 1,150, ukichanganya hapo utapata lita 10,500 za Petrol….utaona
huyu mtu anapata faida kubwa sana akiuza mafuta yote,” alisema.

Mtaalamu mmoja wa masuala ya mafuta alilieleza Majira jana kuwa kama serikali haitapandisha ushuru wa mafuta ya taa au kushusha ule wa petroli na dizeli, tatizo la kuchanganya mafuta halitakwisha.
Mtaalamu huyo alisema wakati ushuru wa dizeli ni sh 529 na petroli sh 519, ule wa mafuta ya taa ni sh 52 na hivyo kufanya tofauti kuwa kati ya sh 467 na sh 477 kwa kila lita moja.

"Kwa hivyo mtu akichanganya mafuta ya taa lita 1,000,000 kwenye petroli, akiuza anapata sh. milioni 467,000,000. Hizi si pesa ndogo, ndio maana tatizo hili haliwezi kumalizika," alisema bila kutaka kutajwa jina.

Mtaalamu huyo aliongeza kuwa serikali inataka kugusa ushuru wa mafuta ya taa wanaonufaika nao wanakuja juu, wakidai kuwa wananchi maskini wataumia, kumbe ingewezekana kuupandisha ukawa sawa na ule wa mafuta mengine, kisha ikatumia fedha hizo kuwapatia nafuu wananchi mahali pengine.

Mfanyabiashara mwingine mjini Moshi alihoji sababu za serikali kutoweka mafuta katika bohari za serikali kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwani kwa kufanya hivyo kuna njama za kujipatia fedha kwa njia zisizo halali.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Lucas Ng’hoboko jana alisema hawezi kuzungumza hatua zaidi kuhusiana na suala hilo kwa sababu ya msafara wa rais na kwamba angekuwa tayari kuzungumza baada ya kiongozi huyo kuondoka mkoani humo.
 
Back
Top Bottom