Serikali iache kupiga ramli, Madktari rudini nyuma

Nakapanya

JF-Expert Member
May 22, 2012
2,096
708
Madaktari wamegoma, ni kweli;Serikali imenyoosha makucha yake tayari kumrarua yeyote atakeyejitia kimbelembele kutetea maslahi ya umma.

Serikali inapiga ramli kumjua mchawi anayepelekea serikali kupingwa vikali na Wananchi wake, serikali inahaha,chama kinahaha pia, wananchi wanahaha hawana pa kukimbilia, dhiki imewatawala ila kila leo wanaambiwa "maisha bora kwa kila Mtanzania", katikati ya mihangaiko ya kutafuta mkate wa kila siku huku tukitembea tukiwa wagonjwa tusiojijua tunakutana na mgomo wa madaktari,mke mjamzito anahitaji kujifungua kwa operesheni sina uhakika kama atasalimika, baba anaumwa miguu, presha na kisukari inatakiwa kila mwezi ahudhurie kliniki,yote hayo yamekwama kwa vile tuu madaktari wamegoma na serikali imekimbilia mahakamani kuweka pingamizi.Nani atakuwa msaada kwetu sisi makabwela tuliotelekezwa na serikali tuliyoiweka wenyewe madarakani?

Serikali ipo bize kupitisha bajeti ya kununua mashangingi na chai pale maofisini mwao,kiongozi wa Kaya kila leo kiguu na njia kwenda ughaibuni;akiulizwa tija ya safari hzoanasema tusiposafiri tutalala njaa "good".

Ombi langu kwako MKUU WA KAYA;naomba uuvae ukiongozi japo kwa siku moja tuu ili utusaidie sisi wapiga kura wako(waajiri) ili tuepukane na mateso haya halafu baada ya hapo uurejee na utawala wako.Nirudi kwa ndugu zangu,marafiki zangu na jamaa zangu madaktari;najua mnafanya kazi kwenye mazingira magumu na yote mnayopigania ni kwa maslahi ya umma wa watanzania wengi tuliomasikini(ondoa viongozi kwani wao hawahitaji huduma zenu coz hata wakiugua mafua wanaenda kutibiwa India kwa pesa zetu za kodi),tunawaomba mrudi kazini mtuhudumie huku majadiliano yakiendelea,kumbukeni wapiganapo mafahari wawili,nyasi ndio huumia,ktk mgogoro wenu anayeumia ni sisi watanzania maskini.

Naomba niishie hapo coz machozi yananitoka kila nikiwaangalia ndugu zangu,jamaa zangu hata watanzania wenzangu wanaoteseka vitandani bila kujua hatma ya maisha yao na uhai wao.Mungu ibariki Afrika,mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom