Serikali iachane na chaguzi ndogo - Mtatiro

Mbunge akipigiwa KURA na wananchi husika ndo anakuwa na morali ya kazi yake..pesa wacha zitumike kwani ni halali ya watz na pesa ni zao, ndo matumizi ya pesa hayo. Tusifanye uchaguzi mdogo kwa ajili ya kuokoa gharama hapo ndo ameona pana matumizi makubwa ya fedha? Labda angesema tupunguze gharama za chaguzi lakini sio kurithishana.
 
Nakubaliana na hoja kwamba serikali inaingia gharama kubwa kushughurikia chaguzi ndogo, wazo langu ni achukuliwe aliyekuwa mshindi wa pili bila kujali chama alichotoka maana anakuwa alipigiwa kura na wananchi wote. Kumchukuwa mtu kutoka chamani mmmh!?

hahaaa yaani wewe unataka kugombana na akina Wassira ...wachukue mgombea wa pili? hahaaa akina mwigulu watapata wapi muda wa kubandua wake za watu
 
umechoka kukaa buguruni makao makuu pasipo na mvuto huku ukivaa picha ya lipumba kumgeuza mungu wako!
 
hell no!!! utakuwa ni uongozi wa inheritanace kama vile SIOI angeeplace nafasi ya baba yake sio...lakini imekaa vizuri chaguzi zote zisiwepo si kubadilishana tuuuu, baba,mama,bibi, mtoto mpaka ukoo uishe ndipo tufanye uchaguzi.
 
Mtatiro usichanganye umma. South africa na baadhi ya nchi za africa wanachagua chama na chama ndo kinamteua mwakilishi wake kwenye urais, ubunge nk. Hawa wanao uwezo na haki ya kumteua mrithi pale anapo kufa wa awali. Sie tunachagua mtu anaye pendekezwa na chama. Akifa lazima vyama vipendekeze tena na umma umchague mmoja wapo.

Ahsante Mkuu.
 
Na akifa (siombei) Maalim Seif basi Mtatiro awe Katibu mkuu wa CUF........hakuna haja ya uchaguzi.:yo::high5::rockon:
 
ajibu tuhuma za kuipoteza kata ya huko Dar maana nasikia alisema ni bora kata iende iliko enda kuliko kwenda CDM akasuka mpango wa kuwasaidia na akafanikiwa kwa kuwatumia mabaunsa
 
Naibu Katibu mkuu wa CUF Julius Mtatiro ameitaka serikali kuachana mara moja na chaguzi ndogo kwani ni kutapanya hela za walipa kodi bure.

Mtatiro amesema serikali inapaswa kupitisha sheria kwamba anapokufa mbunge sharti arithiwe kutoka chama kile kile bila kufanya uchaguzi upya.

Akizungumzia uchaguzi wa Arumeru alisema CCM ilipaswa kumteua mrithi bila kufanyika uchaguzi.

Mtatiro alitoa mfano wa nchi za Msumbiji na Ghana kwamba zinafuata mfumo huo.

Source: MWANANCHI

Mbunge ni mwakilishi wa wananchi siyo Chama. Chama ni ngazi tu ya kugombea uwakilishi wa wananchi. Nafikiri Mtatizro ameona kuwa chaguzi ndogo ndizo zinazoua au kujenga chama na kwa upande wao CUF chaguzi ndogo zinaua chama. Anajua madhara ya kutaka chama kiteue mbunge badala ya wananchi kuchagua?

  1. Itafikia mahali watu katika chama kimoja wanaogombea nafasi za ubunge wataanza kuviziana ili kutoana dunia kwa lengo la kuwa huenda atateuliwa yeye.
  2. Itaondoa uwajibikaji wa mbunge kwa wananchi wa jimbo lake na kuweka kwa chama zaidi which is bad for development of our democracy

Nafikiri Mtatiro asubiri mchakato wa katiba mpya atoe maoni yake badala ya kutungia sheria, maana haiwezekani mbunge jimbo asipatikane kwenye sanduku la kura. Uchaguzi ndiyo njia pekee ya kupata mwakilishi wa wananchi na yeyote anayetoa mawazo mbadala ni kutaka kulirejesha Taifa miaka 30 nyuma. Matumizi gani ya pesa ambayo Mtatiro anayaongelea?, je ni yale ya kununua shahada za kura au kuhonga wapiga kura?. Kama ni kuandaa uchaguzi kupitia Tume sidhani kama kuna gharama ya kutisha. Gharama zinaletwa na vyama vyenyewe kwa hela zao kama chama hakina hela kinakaa pembeni.

Constituent MP must be decided by the ballot boxes. Hiyo ndiyo demokrasia.
 
Wazo la kumchukua mtu wa pili aliyefuatia kwenye uchaguzi bila kujali chama linaonekana kuwa ni rahisi kwa kuliangalia kinadharia. Lakini ukija kwenye utekelezaji kuna matatizo makubwa sana: kwanza tujue kwamba mtu wa pili lazima atakuwa wa chama tofauti na mbunge aliyekuwa akitumikia jimbo lililachwa wazi. Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa kwa wabunge kufanyiwa hujuma na wapinzani wao (yule wa pili) ili jimbo liwe wazi. Ni kweli chaguzi ndogo zinatumia fedha nyingi sana, tuendelee kuchangia mawazo ambao yataingizwa kwenye katiba mpya kwa ajili ya kupunguza gharama hizo. Mimi wazo la kumchukua mtu wa pili ninaliafiki kwa jimbo likiwa wazi kwa sababu zingine isipokuwa za kifo. Maana watu watakuwa wanawahujumu wabunge kwa kuwaua.
 
poor mind mkuuu vyama vya kurithishana watu nenda china au korea kaskazini
 
Mchumia tumbo keshaanza kutumwa!ukiwa tegemezi ni mbaya sana!shameon you.unawatia aibu wafuasi wako,sio lazima uongee hata kamahoja yakoni dhaifu,demokrasi iz not like coca-cola.read between lines.
 
Mtatiro na viongozi wenzako wa CUF mmeshindwa jenga chama chenu sasa wenzako wamekutuma mawazo ya kipuuzi kama haya ili chaguzi ndogo zifutwe kusitiri aibu yenu?! Haya sasa ktk Katiba Mpya akirudishwa mgombea binafsi,akifariki arithi nani? Mke ama watoto? Sikujua kama ni mufilisi wa kisiasa kiasi hiki!
 
Demokrasia ina gharama zake brother. Sasa huyo wa kuteuliwa atakuwa na tofauti gani ni kina Vicky Kamata?

Labda tuwe tunachagua kama raisi na makamu wake, at least tunajua tunachagua mtu na atakayemrithi kama kutakuwa na tatizo. Kuteuana, hell no.

msiwe mna coment kabla hujasoma post. Mtatiro amesema huyo nassari angekuwa mbunge badala ya kufanya uchaguzi kwani alishika nafasi ya pili hilo nijambo zuri kupunguza gharama, huu ni ufisadi mwingine tunao ukataa
 
ajibu tuhuma za kuipoteza kata ya huko Dar maana nasikia alisema ni bora kata iende iliko enda kuliko kwenda CDM akasuka mpango wa kuwasaidia na akafanikiwa kwa kuwatumia mabaunsa

acheni unafiki tamaa za chadema. Cdm fika inajua kata ya vijibweni ina shikiliwa na cuf kulikuwa hakuna haja ya kuweka mgombea na kugawa kura.
 
Mtatiro na viongozi wenzako wa CUF mmeshindwa jenga chama chenu sasa wenzako wamekutuma mawazo ya kipuuzi kama haya ili chaguzi ndogo zifutwe kusitiri aibu yenu?! Haya sasa ktk Katiba Mpya akirudishwa mgombea binafsi,akifariki arithi nani? Mke ama watoto? Sikujua kama ni mufilisi wa kisiasa kiasi hiki!

nyinyi wanafiki gharama zinazopotea bure kurudia uchaguzi na kulikuwa na njia nzuri bila kutoa gharama nyingi. Mfano nasari alishika nafasi ya pili basi angepewa akamalizia kipindi kilicho baki. Kisinge haribika kitu
 
Nakubaliana na hoja kwamba serikali inaingia gharama kubwa kushughurikia chaguzi ndogo, wazo langu ni achukuliwe aliyekuwa mshindi wa pili bila kujali chama alichotoka maana anakuwa alipigiwa kura na wananchi wote. Kumchukuwa mtu kutoka chamani mmmh!?

una hoja ya msingi sana mkuu, tuliangalie hili kwa mapana wana JF!
 
Back
Top Bottom