Serikali: Hatuna mpango wa kuwafukuza Madktari 374 waliogoma

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
Serikali imesema haina nia ya kuwafukuza madaktari 374 waliokuwa kwenye mafunzo kwa vitendo katika hospitali mbalimbali nchini baada ya mgomo wao.

Akizungumza na NIPASHE Jumapili, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando, alisema serikali haina nia hiyo. Alisema hadi sasa hakuna daktari aliyefukuzwa kazi kutokana na mgomo huo na hakuna pia aliyefutiwa usajili wake wa kudumu.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu huyo, serikali ilichokifanya kwa madaktari hao ni kuwahoji, na kazi inayoendelea sasa ni kuyafanyia kazi majibu yao na kisha kuwaita mmoja mmoja kwenye Baraza la Madaktari Tanganyika ili wakajitetee dhidi ya mashitaka yatakayo wakabili na hatua za kisheria zitafuata lakini si za kufukuzwa.

"Zipo adhabu mbalimbali zinatakiwa kufuatwa na sio kuwafukuza kazi na serikali haina malengo hayo ya kuwafukuza. Kumekuwa na uzushi usio na maana kuwa madaktari wamefukuzwa kazi, sisi tunatambua umuhimu wao," alisema Dk. Mmbando.

Dkt. Mmbando alisema kitendo cha madaktari hao kuambiwa kuwasilisha usajili wao wa muda, sio kwamba wamefukuzwa kazi, bali ni utaratibu katika masuala ya kazi. Alisema hata daktari anapohamishwa na kupelekwa eneo jingine, ni lazima awasilishe usajili huo wa muda ambao ulikuwa umempa maelekezo ya kuwa katika hospitali husika, "...hivyo kitendo cha kuwaambia walete usajili wao sio tumewafukuza, na ujue ule ni usajili wa muda na sio ule wa kudumu," alisisitiza.

CHANZO; GUMZO LA JIJI
 
Madaktari 146 wamefukuzwa katika hospitali mbalimbali nchini
Tanzania kutokana na kushiriki mgomo unaoendelea nchi nzima kwa
lengo la kuishinikiza Serikali kutekeleza madai yao. Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa, madaktari hao walitimuliwa
katika Hospitali za Bugando na Sekou Toure mkoani Mwanza na
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na ile ya Rufaa Dodoma. Wakati Serikali ikichukua hatua hiyo, mgomo huo Ijumaa uliendelea
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Ocean Road, Taasisi ya Mifupa
Muhimbili (MOI) za jijini Dar es Salaam, Hospitali ya Mkoa wa Dodoma
na Hospitali ya Rufaa ya KCMC mkoani Kilimanjaro.Kusoma zaidi bofya Katika kile kinachoonekana kuwaunga mkono wenzao, madaktari
bingwa wa MOI, MNH na Ocean Road jijini Dar es Salaam, jana
walitangaza rasmi kuingia kwenye mgomo huo hadi madai hayo
yatekelezwe. Madai ya madaktari ni hali bora ya mazingira ya utoaji huduma nchini,
ongezeko la mishahara, posho za kufanya kazi katika mazingira
magumu, posho za kufanya kazi katika mazingira hatarishi na posho za
kuitwa kazini. Tamko la madaktari hao bingwa, lilitolewa jana na msemaji wao, Dk
Catherine Mng’ong’o muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao chao
kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Tamko hilo limekuja siku moja baada ya baadhi yao kuanza kushiriki
mgomo huo juzi, kushinikiza pamoja na mambo mengine, Serikali itoe
tamko juu ya tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dk Ulimboka. Hata hivyo, wakati madaktari hao wakitoa tamko hilo, uongozi wa Moi
jana ulitoa tangazo kuwataka madaktari wote walioshiriki mgomo huo
kurejea kazini ifikapo Julai 2, mwaka huu, vinginevyo watafukuzwa
kazi. Jana jengo la MOI lilikuwa limefungwa kwa makufuli, huku wagonjwa
wakielezwa kuwa huduma zote hazitolewi zikiwamo za dharura
ambazo awali ziliendelea kutolewa.
Mmoja wa walinzi aliwambia waandishi wa habari kuwa, amefunga
mageti kutokana na amri ya mkuu wake wa kazi.
“Mimi ninatekeleza amri ya bosi wangu, amenitaka kufunga geti na hakuna mtu kuingia, awe mgonjwa au ninyi waandishi wa habari kwa
kuwa hakuna huduma zinazotolewa humu,” alisema.
Mkoani Mwanza
Madaktari 63 walio katika mafunzo ya vitendo kazini wa Hospitali ya
Rufaa ya Bugando, Hospitali ya Mkoa Sekou Toure wametimuliwa na
kurejeshwa wizarani kutokana na mgomo huo. Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dk Charles Majinge
alisema kuwa, juzi aliwataka madaktari waliokuwa katika mgomo
kurejea kazini, lakini hawakufanya hivyo na jana akaamua kuwarejesha
47 wizarani. Katika Hospitali hiyo ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure, Mganga Mkuu
wa Mkoa, Dk Valentino Bangi alisema, madaktari 16 wamesimamishwa
kufanya kazi kutokana na agizo la wizara. Kilimanjaro Madaktari walioko kwenye mgomo katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC,
Moshi mkoani Kilimanjaro walisema jana kuwa, kinachofanywa na
Serikali kuwafukuza kazi waliogoma, ni njia mojawapo ya vitisho, lakini
wakasema kuwa kamwe hawataogopa. Madaktari hao ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini
walisema, wao wanaendelea na mgomo mpaka pale Serikali
itakapotekeleza madai yao. “Tumesikia wenzetu wa Dodoma na Mbeya wamefukuzwa ….Hiyo
haitufanyi turudi kazini na kama Serikali inaona hiyo ndiyo njia ya
kumaliza mgogoro huu waendelee sisi tutarudi kazini pale
itakapotimiza tunayotaka,” alisema mmoja wa madaktari hao. Mbeya Juzi Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, ilitoa tangazo la kuwataka madaktari
waliopo mafunzoni waliogoma kurejea kazini jana, na endapo
wangekiuka agizo hilo wangekuwa wamejifukuzisha kazi. Na hadi jana
jioni hospitali hiyo ilikuwa imewafukuza madaktari 72. Ocean Road Katika Taasisi ya Taifa ya Saratani, (Ocean Road), kutokana na
madaktari sita kusitisha kutoa huduma tangu Dk Ulimboka
alipojeruhiwa kwa kipigo, waligoma na jana Mkurugenzi wa Tiba na
Huduma Diwani Musemo alionekana akitembelea wagonjwa. Dodoma
Madaktari 11 wa mafunzo kwa vitendo katika Hospitali ya Mkoa wa
Dodoma nao wamefukuzwa, tukio ambalo jana lilileta usumbufu
mkubwa katika upatikanaji wa tiba hospitalini hapo.
“Kwa hakika matibabu yanaendelea ingawa ni katika hali ya kusuasua.
Hatuna uhakika kama kweli kuna mgomo wa chinichini au la, maana mimi nimefika mapema, lakini bado sijahudumiwa,” alisema mmoja
wa wagonjwa waliozungumza na mwandishi wa habari.
Arusha
Katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, huduma
zimedorora lakini Mganga Mkuu, Dk Omar Chande alisema jana kuwa,
imekuwa ni vigumu kuchukua hatua kuwabana madaktari ambao wanatuhumiwa kufanya mgomo baridi, kwani wote wanaripoti kazini. “Ni kweli kuna taarifa hizi za kuwapo mgomo baridi, lakini madaktari
wote wapo kazini, ila kama kuna kufanya kazi chini ya kiwango,
tumeanza uchunguzi,” alisema Dk Chande.
Amana Katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam utoaji wa huduma
ulisuasua kutokana na mgomo huo jambo lililofanya uongozi kuwekatangazo kwenye Ofisi ya Mganga Mkuu kuwataka watumishi wote
ambao hawakuwapo kazini kuanzia Juni 25, 2012 waandike barua za kurejea kazini. Tangazo hilo pia linawataka madaktari walioko mafunzoni kuandike barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia kwa mganga mkuu wa hospitali hiyo.

CHANZO:MWANANCHI June 30,2012
 
Serikali imemeza maneno yake?

.
Aha ha haa. Ni kama gari imemeza moto kwenye kilima. Msemo huu wa gari kumeza moto unatumika pale gari hasa yale makubwa ya mizigo gear NO' moja inaposhindwa kazi. Hivyo serikali kwa hili la ma-doc's imemeza moto.
.
 
.
Aha ha haa. Ni kama gari imemeza moto kwenye kilima. Msemo huu wa gari kumeza moto unatumika pale gari hasa yale makubwa ya mizigo gear NO' moja inaposhindwa kazi. Hivyo serikali kwa hili la ma-doc's imemeza moto.
.

Mkuu inabidi nicheke tu manake kila siku wanazidi kuji contradict mbele ya Camera na kalamu za wanahabari!..
 
wamezidiwa na matukio wanajaribu kupunguza kasi ya kuchokwa.
 
Back
Top Bottom