Serikali haina nia ya kweli kumaliza tatizo la maafisa ugani katika sekta ya uvuvi

Nteko Vano

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
434
111
Serikali yetu kupitia wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi haina nia ya dhati kumaliza tatizo la maafisa ugani katika sekta ya uvuvi. Hali hii inasababishwa na kupandishwa kwa ada ya vyuo vyake kutoka Tsh. 400,000 hadi 1,600,000/= kwa mwaka.

Waziri husika kupitia bunge leo jioni amekiri kuwa kuna upungufu wa maafisa ugani 15,700 katika sekta ya uvuvi na wanafanya jitihada kumaliza tatizo hili. Mpango wa wizara hii katika kumaliza hili ni kuvitumia vyuo vyake vya Nyegezi-Mwanza na Mbegani-Bagamoyo.

Vyuo hivi vimekuwa vikitowa elimu ya cheti na stashahada katika fani mbalimbali za uvuvi kwa ada nafuu kwa kipindi kirefu sasa na kufanya kuwa kimbilio la wanafunzi wengi maskini. Ada ilikuwa 750,000/= ikapunguzwa mpaka 400,000/= ili kuruhusu wanafunzi wengi kusoma masomo hayo. Serikali imekuwa ikitoa ruzuku kwa ajili ya kufidia gharama nyinginezo ingawa kwa kusuasua ukilinganisha wanavyofanya kwenye vyuo vya mifugo.

Hivi karibuni vyuo hivyo vimekuwa wakala (Agency) na kuna mkakati wa kupandisha ada mpaka Tsh. 1,600,000/=. Hii itasababisha wanafunzi kutoka nchini hapa kukosa fursa ya kusoma masomo hayo, serikali kupunguza uhaba wa wana ugani na hatimaye kurudisha nyuma maendeleo ya sekta hii. Wanafunzi wameshapewa fomu kwa mabadiliko ya ada hizo.

Kwa mantiki hiyo naona kama waziri leo alikuwa analiongopea bunge juu ya mikakati ya kupunguza tatizo la wagani hao na serikali haina mikakati ya dhati juu ya suala hili.

Nilikuwa naona kama ingekuwa vema wangetafuta mbinu mbadala ya kufidia gharama za uendeshaji kuliko kupandisha ada kwa kiwango kikubwa kiasi hicho. Wangetumia rasilimali zao kama meli za uvuvi kujiingizia mapato na ada wangepandisha kidogo lakini sio kwa kiwango hicho.

Nawasilisha.
 
'ugani' maana yake 'uenezi''? Bado sijaelewa . Maafisa ugani wanaeneza nini?

Wanaeneza elimu na mbinu kwa wadau katika sekta husika. Kwa mfano katika sekta uvuvi:elimu ya ufugaji samaki, kuhifadhi samaki nk, kilimo; elimu ya ukulima wa embe kwa mfano, elimu na mbinu za kilimo cha kahawa n.k, mifugo; ufugaji bora wa kuku n.k.
 
'ugani' maana yake 'uenezi''? Bado sijaelewa . Maafisa ugani wanaeneza nini?
Mfano: Maafisa ugani wa kilimo wanaeneza teknolojia za kilimo, wa mifugo na uvuvi nao wanaeneza teknolojia husika.
 
Back
Top Bottom