consigliori
JF-Expert Member
- Mar 29, 2010
- 392
- 89
Hii makala imejaa ufundi wa kisheria kiasi kwamba kwa sisi tusokuwa wanasheria ukimaliza kuisoma inabidi umeze panadol!
Mimi bado ningependa kueleweshwa zaidi juu ya uwezo wa mahakama kutengua kipengele cha katiba kwa katiba. Kama nimemuelewa vizuri Lula, mahakama inaweza tu kutangaza uamuzi fulani au hatua fulani ya serikari kuwa kinyume cha katiba ( "Ni rahisi zaidi kwa mahakama kutengua sheria au kipengele fulani cha sheria kwa kutumia Katiba. Na ni rahisi vile vile kusema kuwa uamuzi au hatua fulani ya serikali ni kinyume na Katiba").
Kwakuwa tunajua kuwa swala la mgombea kuwa lazima awe mwanachama wa chama cha siasa tayari lilikwisha ingizwa kwenye katiba, je si wajibu wetu wananchi kupeleka shauri mahakani la kuiomba mahakama itangaze kuwa hatua ile ya serikari ya kuingiza kwenye katiba kifungu kinachokandamiza haki za raia ilikuwa kinyume cha sheria na hivyo kuishauri serikali kurekebisha? Kwa sababu kwa sasa sioni kama Mahakama itaweza kuruhusu mgombea binafsi kabla kipengele kinachotaka mgombea kuwa na chama hakijoka kwenye katiba.
Kama niko sahihi, mahakama haiwezi tu kutangaza, mpaka mtu apeleke shauri hilo mahakamani. ( Kwani haiwezi kushtaki na kusikiliza kesi wakati huo huo.)