Serikali dhaifu huyumbishwa na wenye mali

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,185
307
Nimesikitishwa na jinsi serikali yetu inavyowababaikia wawekezaji kiasi cha kufikia kuwaua raia wake ili kuwafurahisha wawekezaji wa kigeni. Leo kweny gazeti la Mwananchi kuna habari kuwa wawekezaji wa Twiga Cement wanatishia kuondoka endapo wananchi hawatafukuzwa kwenye shamba ambalo kampuni hiyo inasema ni lake!

Kwa akili ya kawaida uamuzi wa kufunga biashara kubwa kama ya Twiga Cement ni mgumu na unaweza kufanyika pale tu ambapo hakuna namna, ile ni biashara ambayo una uhakika wa soko, una miundombinu ambayo ipo tayari na inafanya kazi..

Mtu yeyote anayetishia kufunga kiwanda kile eti kushinikiza watu kufukuzwa kwenye eneo lake ni wa kupuuzwa, hawezi kufanya hivyo. Ni aibu kwa serikali yetu kuyumbishwa na vitisho vyo kitoto namna hii na kupoteza muda kufikilia kuwa wanaweza kufunga kile kiwanda, wakiamua kufunga na wafunge!
 
Tukiwa na maafisa mipango miji,maafisa Ardhi na wapima wengi matatizo ya Ardhi nchi hii yatapungua kama sio kuisha kabisa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom