Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,268
- 17,097
PICHA za mgombea wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizobandikwa katika eneo baadhi ya maeneo zimechanwa na watu wasiojulikana hali ambayo ofisi ya Mkuu wa Mkoa imesema inafuatilia kubaini wanaofanya vitendo hivyo.
Eneo ambalo gazeti hili limeshuhudia picha hizo zikiwa zimechanwa ni katika chuo cha teknolojia Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi alisema, "tutalifanyia kazi suala hilo na ngoja tuanze kulishughulikia kwa kuwa lipo ndani ya mkoa wangu ina maana lipo chini yangu pia," alisema Lukuvi.
Gazeti hili lilipita katika maeneo hayo na kushuhudia picha za mgombea huyo zilizobandikwa katika mabati na kuta zilizozunguka eneo hilo zikiwa zimechanwa hali iliyoleta maswali mengi kwa watu wengine waliokatisha katika eneo hilo.
Wakizungumza na gazeti hili baadhi ya watu hao ambao hata hivyo hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini walisema kinachotakiwa kufanywa kwa sasa ni kwa mamlaka zinazohusika kuwatafuta waliofanyakitendo hicho ili wafunguliwe mashitaka.
Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alipozungumza na gazeti hili, alisema, "kwa sasa siwezi kusema neno lolote kwa kuwa si mhusika wa mkoa huu, ingekuwa hapo zamani wakati huo mkoa unatambulika kama mkoa wa Mmakamba ningeweza kulisemea suala hilo," aliongeza katibu huyo.
Maoni
Acheni hizo na nyie bwana mambo ya CCM yaenze kutumia fedha za serikali kuyashughulikia. CCM watafute namna yao watakayoweza kuyalinda mabango yao. Kama zingechanwa za chadema au CUF serikali ingezishughulikia? Mambo ya nchi ndo yanaponichoshaga hapo.