Ni kweli, ana uelewa mfinyu sana. Wiki iliyopita alitamka bila ya aibu kuwa Misri imekuwa ikiongozwa kijeshi tangu mapinduzi ya gamal Abdel Nasser ya mwaka 1952 -- hakujua kwamba Misri ilianza kuwa na demokrasia ya vyama vingi tangu wakati wa Sadat 1971 na kuwa na chaguzi ambazo kila mra chama tawala NDP ndiyo kilikuwa kinashinda, kwa kuchakachua (kama vile CCM tu) hadi 2011 Tahrir ilipotokomeza uchakachuaji huo!
Labda angesema Misri ilikuwa inatawaliwa na wanajeshi, au waliokuwa wanajeshi -- lakini siyo kijeshi!!!
MNembe afahamu kuwa tuko wengi tu ambao tuna uelewa wa historia na mambo ya ulimwengu kwa hiyo achunge sana kauli zake hasa pale, inaposemekana ana mikakakti ya kuingia Ikulu 2015.
Hivi kwa nini haya mazungumzo na hasa linapokuja suala la kumjadili Membe watu wanakosa focus. Watashika hili na baada ya muda kidogo topic inabadilishwa.
Hoja hapa ni kwamba kuna balozi zinazoshukiwa kukisaidia chama fulani cha upinzani na hadi sasa hatujui na TLP, NRA, CUF au NCCR Mageuzi. Sasa kujadili mada kwa hisia kwamba chama hicho ni kile kilicho maarufu kwa wengi humu, hazina msingi wowote. Sasa kama kuna ushahidi kwamba alichoeleza yeye hakina ukweli basi watu watoe data za kumkosoa siyo kurukia lile au hili kwa nia tu ya kujaribu kuonyesha kwamba mtu huyo haaminiki.
Kuhusu suala la utawala wa Misri yeye alitamka wazi kabisa kwamba nchi ile imekuwa chini ya utawala wa kijeshi kwa msingi kwamba wale waliofanya mapinduzi mwaka 1952 ndiyo hao hao wamekuwa wakibadilishana uongozi.
Hicho unachoita wewe mfumo wa vyama vingi kama aivyofanya Sadat ni kiini macho na ndiyo maana vyama vyote hivyo kikiwemo Muslim Brotherhood vimekuwa vinapata misukosuko na hata viongozi wao kuwekwa kizuizini.
Hicho kinachoitwa demokrasia si demokrasia na ndiyo maana hata leo ni military junta ileile ndiyo iliyopo madarakani. Kwa ujumla ukosoaji huu ni ule ule uliochochewa na chuki za mtoa mada bila kujali kile alichoongea na ndiyo maana kuna kurukia rukia mada. Wenye akili wanajua kiini cha ukosoaji huu holela!