Serikali: CHADEMA inapewa pesa kutoka nje kuleta machafuko Tanzania

Fareed

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
328
135
Waziri wa Jakaya Kikwete, Sophia Simba, akiongea kwenye TBC leo asubuhi amesema kuwa viongozi wa CHADEMA wanapewa pesa nyingi kutoka nje ili kufanya maandamano kwa lengo la kuifanya nchi isitawalike.

Sophia amesema kuwa CHADEMA wamekuwa wakiwapa wananchi pesa ili washiriki maandamano hayo.

"Eti wanaandamana kuhusu DOWANS na uchumi. Kwa kuwa kesho ni siku ya kimataifa ya wanawake, nachukua fursa hii kuwasihi wanawake wasishiriki maandamano ya kikundi hiki. Kwanza wanakupa pesa za siku moja tu, huko kwenye maandamano kuna uchumi?" Alisema.

"Haya maandamano hayana tija."

Sophia aliwataka wananchi, hasa wanawake, wasipoteze muda kwenda kwenye maandamano ya CHADEMA kwani muda huo wangeutumia kufanya ujasiriamali.

"Kama kuna matatizo yoyote, serikali itayashuhulikia," alisema.
Matamshi haya ya Sophia yanaonesha kuwa serikali ya Kikwete inaamini kuwa foreign governments are funding CHADEMA ili kifanye maandamano na kuleta vurugu nchini.

Watawala wanajiaminisha kuwa eti CHADEMA inawalipa wale maelfu ya Watanzania wanaojitokeza kwenye maandamano.

Msimamo wa serikali ya Kikwete imenikumbusha ya Gadaffi wa Libya ambaye US President Ronald Reagan alimuita kama "The Mad Dog of the Middle East" way back in 1986.

Gaddafi alisema: "Wananchi wa Libya wananipenda sana. Wanaoshiriki maandamano wamelishwa madawa ya kulevya na Al Qaeda na Marekani."

Pia kwa kusema "Kama kuna matatizo yoyote, serikali itayashuhulikia," hii ina maana kuwa watawala hawatambui matatizo lukuki ya wananchi wa Tanzania ambao ni kama kila mmoja kabeba gunia la misumari -- mgao wa umeme, Dowans, ufisadi, umasikini, ukosefu wa ajira, mfumuko wa bei, maisha magumu, kuporomoka kwa elimu, afya duni, ukosefu wa maji, maradhi, viongozi serikalini kutokuwa na maadili, wananchi kunyimwa haki zao, na mengineo mengi.

The CCM government is in denial.
 
mfano wako wa gaddafi na mada yako mezani haviendani! Jaribu kuleta mfano relevant na mada yako
 
Ama kwel mambo yanavyozd kuwa magumu ndipo ninapogundua kuwa kumbe CCM ina vilaza(poyoyo) weng sana. Huyu mama naye keshajihakishia uwepo wake ktk hyo group ya vlaza.

Jaman ngoja ninywe chai halafu baadaye ntawasilisha majina yote ya vilaza waliopo ccm...
 
Hiyo ndiyo aina ya viongozi wenye nguvu ndani ya CCM. Kama kuna matatizo yoyote, inamaana yeye hajui kuwa kuna matatizo.

Serikali ya CCM imeshindwa kushughulikia matatizo kipindi cha nyuma itawezaje sasa? Wameshindwa kazi wawaachie wengine wafanye.
 
Mfano wa Ghaddafi ni sawa kabisa. Yametokea maandamano ya kudai demokrasia Libya Ghaddafi akadhani kuna mkono wa nje (na unga). Sasa yako maandamano ya kudai uongozi bora Tanzania, Sophia Simba amedhani kuna mkono wa nje. Vinashabikiana vizuri tu.

Ni haki ya kikatiba kwa vyama vya siasa kufanya maandamano ya kuhamasisha wananchi. Viongozi wa CCM waache kuogopa. Ila kati yao wako waliopanga maandamano ya kuishinikiza serikali (UVCCM) na hiyo ni sawa tu.

Sophia is not ministerial material. Si huyu huyu alikuwa anapoteza muda kupanga wanawake wavae nini?

Wanaojitokeza kukemea CHADEMA wanatafuta umaarufu tu. Hawana chochote wala si lolote.
 
Maneno ya Simba yana mantiki, si rahisi kuandaa maandamano kila kukicha, unahitaji bajeti nono. Jee fedha zinatoka wapi?
 
mfano wako wa gaddafi na mada yako mezani haviendani! Jaribu kuleta mfano relevant na mada yako

Tabaka la watawala Tanzania ni sawasawa na Gaddafi kwa sababu zifuatazo:

1. Wote wanaimani potofu kuwa serikali yao inapendwa sana na wananchi
2. Wote wanaamini kuwa maandamano yanachochewa na serikali/taasisi/wafadhili wa nje
3. Wote wanaamini kuwa wananchi wanapewa kitu ili kushiriki maandamano, eg pesa/madawa ya kulevya
4. Wote wanaamini kuwa wananchi hawana shida yoyote (eg Sophia akisema "kama kuna matatizo."
5. Wote wametawala kwa muda mrefu sana (CCM miaka 50 na Gadaffi miaka 42)
6. Wananchi wa nchi zote wamechoka umasikini, ufisadi, manyanyaso, ukosefu wa ajira, uporaji wa pesa za umma, etc
7. Chama tawala Tanzania/Libya miaka yote kimekuwa kikishinda uchaguzi wa Urais na wabunge kwa kuiba kura
8. Need I say more?
 
Sophia Simba is a sexy slave na alishatuambia wanawake tuwanyime uyumba waume zetu kama wanaunga mkono upinzani so yeye anawaza kingono kila kitu

UGUMU WA MAISHA UNATUUMIZA/UNATUADHIRI WANAWAKE ZAIDI YA WANAUME so sophia is on the bed waiting for ***** especially when she calls for wanawake to drawback from this maandamano.
 
Kuna sababu kubwa ya viongozi wengine wa CCM kukaa kimya huku Mh. Sofia Simba akiwa ni mmoja wa wachache wanaoongoza kwa kuijibu Chadema. Huyu ni mtu wa mipasho mipasho hivi, upeo wake wa kufikiri na kuchanganua mambo ni mdogo sana na ndio maana kauli zake ni za hovyo hovyo tu.

Kumpa jukwaa la kumjadili huyu mama ni kupoteza nguvu na malengo. Kapewa kazi ya kuongea utumbo huo na hivyo sio kosa lake.
 
Maneno ya Simba yana mantiki, si rahisi kuandaa maandamano kila kukicha, unahitaji bajeti nono. Jee fedha zinatoka wapi?


Mi nadhani Sofia amevumbua siri kutumia intelejensia, huyo ndiyo mmoja wa Intelligence agent wa serikali,aliyetoa habari kuwa maanamano ya CDM arusha yatakuwa na uvunjifu wa amani. hahahah
 
Matamshi haya ya Sophia yanaonesha kuwa serikali ya Kikwete inaamini kuwa foreign governments are funding CHADEMA ili kifanye maandamano na kuleta vurugu nchini.

Watawala wanajiaminisha kuwa eti CHADEMA inawalipa wale maelfu ya Watanzania wanaojitokeza kwenye maandamano.

Msimamo wa serikali ya Kikwete imenikumbusha ya Gadaffi wa Libya ambaye US President Ronald Reagan alimuita kama "The Mad Dog of the Middle East" way back in 1986.

Gaddafi alisema: "Wananchi wa Libya wananipenda sana. Wanaoshiriki maandamano wamelishwa madawa ya kulevya na Al Qaeda na Marekani."

Pia kwa kusema "Kama kuna matatizo yoyote, serikali itayashuhulikia," hii ina maana kuwa watawala hawatambui matatizo lukuki ya wananchi wa Tanzania ambao ni kama kila mmoja kabeba gunia la misumari -- mgao wa umeme, Dowans, ufisadi, umasikini, ukosefu wa ajira, mfumuko wa bei, maisha magumu, kuporomoka kwa elimu, afya duni, ukosefu wa maji, maradhi, viongozi serikalini kutokuwa na maadili, wananchi kunyimwa haki zao, na mengineo mengi.

The CCM government is in denial.
its a good sign kwamba serikali inayumba kwani kila mtu sasa anabwabwaja tu!!! adn they are running from their own shadows
 
this woman must be mad!

Not mad, sick- she must be sick, terribly sick! You simply do not thrush out an argument by asking your good gender to disengage from the other side! WHY single out women!

Secondly what evidence is there to suggest that those attending the rallies are being paid and being paid from funds sourced outside the country! Just reminds me of those other sick persons blaming everything on being religiously/Tribally marginalized! Bureee kabisa!
 
Maneno ya Simba yana mantiki, si rahisi kuandaa maandamano kila kukicha, unahitaji bajeti nono. Jee fedha zinatoka wapi?

Wewe usiwe JUHA. Wananchi wa EGYPT waliandamana mfululizo kwa siku 18 mpaka wakamg'oa Mubarak madarakani. Je, nani aliwapa pesa na walitumia bajeti gani?

Wananchi wanapodai haki yao hujitolea kwa hali na mali na wako tayari kulipa gharama yoyote ile ikiwemo JASHO, MACHOZI na DAMU.

Kwa taarifa yako tu, baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, CHADEMA sasa inapewa ruzuku ya shilingi milioni 200 kwa mwezi. Hizi ni pesa tosha kugharamia maandamano ya nchi nzima. Wala huhitaji pesa za wafadhili.
 
crapppppp!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
huyo mama na ccm yake na wengine wote wenye mawazo hayo wote bongo zao zitakuwa na matatizo.

fedha hizo za mikutano iliyofanyika kanda ya ziwa ni mchango wa wanachama mbalimbali(pipoz power) ikiwemo kila mbunge wa chadema kuchangia laki nne na nusu na kiwango kingine kutoka kwenye ruzuku na hii mikutano haijagharimu mabilioni kama wanavyofikiria.
 
Hivi Sofia simba ni kiongozi wa wapi vile? Sio ubao wa matangazo aqmbao hauna mwenyewe? Nasikia mtu yeyote anaweza kwenda kuandika pale, kwa hiyo sidhani kama asemayo ni ya kwake, katumwa kuwa kisemeo.

Logic na asemayo naona siku zote haviendani
 
Mfa maji haachi kutapatapa ccm wanambwela hadi naona kifo chao kinakaribia. Huyu mama si mzima anatakiwa kupelekwa milembe eti cdm inawalipa pesa watu waandamane huu ni ushankupe na uzandiki wa hali ya juu.

Huwezi ukawalipa umati mkubwa kama wa maandamano ya shinyanga. Na bdo mtambwela hadi ifike 2015 wananchi watakuwa wamejua wapi kuna mazezeta na wapi kuna viongozi wa kweli.

Huu moto hauzimiki kwa maji ya mgao. Huu moto unahitaji maji yote ya bahari ya hindi sio ya dawasco.
 
CCM ndo wamezoea kuwapa hela watu ili waje kwenye mikutano. pia wamekua wakiwatumia wasanii njaa kama Orijino Comedy na wengine kuweza kuwavutia watu waje kwenye mikutano.

wanadhani na CHADEMA wanafanya hivyo. Wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea uraisi wa CCM pale Mwanza nilipotoka nje ya uwanja nilishuhudia watu wakishikana mashati wamedhulumiana pesa walikua wameletwa na mabasi kutoka vijijini.

Washabiki wa CHADEMA wanakuja wenyewe uwanjani tena wengine wanaendesha baiskeli kwa umbali mrefu kuja kumsikiliza Dr wa ukweli
 
HAO Ndiyo mawaziri wa serikali ya JK ambayo wananchi milioni arobaini wanasubiri maendeleo toka kwayo. wanaongea hoja zisizo na mashiko, kwa wananchi wenye dhiki kuu ya maisha. kwanini CDM kisipate umaarufu? " CDM ongeza kasi hilo pigo la mwisho na kumwangusha mpinzani kwa KO.

Waziri mzima uliye na dhamana ya serikali unaweza ukawaambia watu waliokuzunguka na wanakusikiliza utumbo huo , ni aibu sana, sijaelewa Rais anangalia vigezo gani kumteua waziri. kama angetuambia CV anazoangalia tungemsaidia kwa ushauri.

Huwezi kuamini matamshi ya watu hawa yanatolewa na kuandikwa na vyombo vya habari na wananchi kuyasoma ama kuyasikia "shame"
Mwingine waziri mkuu mzima anasema CDM kufanya maandamano ni kwamba hawana kazi, Sasa tunamwambia muda siyo mrefu atagundua kumbe CDM walikuwa kazini.

Hatushangai kwa serikali iliyopo madarakani kusimplify issues ndiyo kawaida yao, hata wananchi kuishi bila umeme kwao simple issue, maisha magumu na matatizo lukuki kwao wao ni simple issues they don't care it is not their responsibilities.

Mimi nadhani huyu mama na waziri mkuu wake wanatapatapa kisiasa, wapeni maji wafe salama.
wasalaam
 
Back
Top Bottom