Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 58,779
- 78,450
20th October 10
Serikali: Bei za saruji, nondo zishushwe
Richard Makore
Serikali imeviagiza viwanda vya saruji na nondo nchini kuhakikisha vinapunguza bei ya bidhaa hizo kwa kuwa hakuna sababu yoyote ya msingi inayochangia zipande mara kwa mara.
Agizo hilo lilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara Viwanda, Biashara na Masoko, Joyce Mapunjo, alipozungumza na NIPASHE kuhusu upandaji holela wa bidhaa hizo.
Alisema uzalishaji wa saruji na nondo ni mkubwa lakini hajui kwanini wazalishaji hao wanazipandisha na kuwafanya wananchi wa kawaida kushindwa kuzinunua.
Aliahidi kufuatilia kwenye viwanda hivyo ili aelezwe sababu zinazowafanya wazidi kupandisha bidhaa zao kwa mauzo ya jumla na hivyo kuwafanya wauzaji wa rejareja nao kupandisha bei.
Bei ya nondo yenye milimita 10 yenye urefu wa futi 40 kwa sasa ni Sh.10,000 kutoka Sh. 8,000 milimita 12 Sh. 13,000 badala ya Sh. 12,000 na bei ya mfuko mmoja wa saruji hivi sasa ni Sh. 13,000 badala ya Sh. 12,000.
Na katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Wakala wa Serikali Biashara na Leseni nchini (Brela), Esteriamo Mahingila, aliwataka wazalishaji na wakulma kujiwekea malengo ili kuhakikisha wanaziwekea nembo bidhaa zao zote wanazozalisha.
Mahingila alikuwa akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wataalamu wa masuala ya hakimiliki duniani ambao wanahakikisha bidhaa zinakuwa na nembo na alama kabla ya kuuzwa.
NIPASHE

MY TAKE
Sitashangaa Mzugaji wetu kubadili sera na kusema elimu bure toka chekechea mpk chuo!!