Serikali acheni siasa, toeni huduma kwa jamii

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,600
8,741
Serikali yetu ya Tanzania imekuwa kwenye siasa nyingi wakati watu wanamatatizo ya mafuta, maji na umeme.

Serikali imechaguliwa kutatua haya matatizo badala yake serikali imekuwa ikipoteza muda mrefu kufuatilia masuala ya siasa na kushindana maneno na Vyama vya upinzani kucha kutwa.

Nchi yetu kwa sasa ipo pabaya na serikali ipunguze siasa na inatakiwa kuimarisha mahitaji ya watu. Watanzania hawahitaji vitu vingi lakini barabara, umeme, maji, na mafuta watu binafsi hawawezi kutatua haya matatizo!

Serikali inatakiwa iangalie policy vizuri na itatue haya matatizo haraka kwani nchi sasa haina hope kabisa. Acheni kelele za kulaumu wapinzani wakati vitu vichache muhimu kwa maisha ya kila siku havipo Rwanda inakuaaje wana huduma zaidi yetu wakati ni nchi ndogo haina gas wala bandari!

Serikali acheni porojo na fanyeni kazi bila ubinafsi kabla hamjaleta vita Tanzania.
 
Inabidi ufafanue unamaanisha nini by serikali ta Tanzania mkuu..maana ndani ya serikali kuna viongozi wa chama tawala waliopewa ridhaa na wananchi kuipa mwongozo serikali, hao ni wanasiasa na siasa ni sehemu ya majukumu yao. Ila pia serikali inahusisha watumishi wa umma ambao wameajiriwa na wanalipwa mishahara (na posho anyway) kujenga nchi, siasa kwao ni uanachama na hawapaswi kufanya siasa.

Ila pia tafsiri yako ya siasa inazungumzia siasa mbovu na za ulaghai zisizo na tija au maendeleo. Literally siasa zinapaswa kuwa mhimili wa maendeleo kwa maana ya utengenezaji wa sera nzuri na usimamizi madhubuti katika kuzitekeleza..
 
niko pamoja nawe kwa hilo ila tatizo sio serikali tu ila pia wananchi wanaendekeza sana siasa na kutupiana vijembe badala ya kutaka kujiimarisha.
 
Back
Top Bottom