Serikali acheni midhaa na maisha ya watu

Jun 17, 2011
20
5
Serikali kupitia Waziri wetu mkuu Bwana Mizengo Pinda inasema imejipanga vyema kuhudumia jamii katika mgomo wa madaktari,hivi mwanzoni mbona watu walipoteza maisha ina maana mlikuwa hamja jipanga au?

Pia hii kauli ya kusema " wao kama watanzania kwa taaluma na miiko yao sitegemei kuwaona wanagoma wakati maisha ya watu yanapotea" hivi kama serikali mnasema hivyo nami najinukuu, "nyinyi kama serikali sitegemei kuona watu wanapoteza maisha wakati mpo na hamtatui matatizo ya MADAKTARI ili wawahudumie wananchi"

Upanga unakata huku na huku, madaktari na wauguzi pia mnajidharirisha, kama mmeamua kugoma basi msioneshe nyuso zenu sehemu zenu za kazi manawatesa wananchi, kilichotokea Hosptali ya temeke sio kitu kizuri,mnachukua hela za watu kisha hamwahudumii?
 
Wajipange wasijipange,wanaokufa ni watza wasiokuwa na uwezo wa kwenda kutibiwa ng'ambo!Kama wamejipanga,kwann walikuwa wanawasihi madokta wasigome?Wana bahati hii ni nchi ya Kichaa chini ya mfalme juha!Nchi ambamo hata takwimu za waliokufa kutokana na athari za mgomo hazikuwekwa wazi nahakuna aliyeziulizia!Waliofiwa wakazika wafu wao na kuamini kuwa BWANA ALITOA,BWANA AMETWAA.
 
Back
Top Bottom