Serekali imeshindwa basi sisi wananchi tuanze na hili

Kabathe

Member
Jan 18, 2011
23
5
Africa ni moja,matatizo yetu yanafanana,mfano kilichowafanya vijana wa Tunisia na Misri kuingia mitaani is the same as to what we are facing in our country; ufisadi, ukosefu wa ajira, bei ya bidhaa muhimu kupanda kila siku, hakuna haki, wananchi wananyanyaswa ndani ya nchi yao na serikali yao. Mafisadi tunawajua, serikali inawajua. Hakuna wa kuchukua hatua. Sidhani kama kuna vijana wakitanzania wanaweza kuingia mitaani kudai HAKI yao, labda si kwa sasa. Hawa watu tunawajua, baadhi ya biashara zoa tunazijua, kwanini tusichukue hatua ya kuzigomea.Mfano kama kuna fisadi tunafahamu kuwa anamiliki kampuni au kituo cha mafuta basi watu wote tuacha kununua mafuta kwenye vituo vyake.
 
wazo zuri sana , tatizo utekerezaji na uhamasishaji; wanasiasa kwenye mikutano yao wangekuwa wanaongea haya taratibu watu wangeanza kuerewa haya
 
Back
Top Bottom