Serebuka Chali..kumbe ulikuwa usanii

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
975
47
Ile shoo iliyokuwa ikipaishwa hewani kila Jumapili kupitia Kituo cha Televisheni cha TBC1, Serebuka imekula mwereka kusonga mbele baada ya muandaaji wake kushindwa kukidhi mahitaji ya washiriki.

Ishu ‘imebumbuluka' juzikati pale washiriki walipotakiwa ‘kushuti' moja ya kipindi hicho lakini wakakanyagia ngumu wakidai maslahi yao ya nyuma.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Serebuka kilisema kuwa, hivi karibuni washiriki waliobaki ndani ya kinyang'anyiro hicho walishindwa kufanya zoezi hilo baada ya kuomba walipwe posho zao kabla ya ‘kushuti' lakini muandaaji huyo aliwatolea nje suala hilo ndipo baadhi yao wakatengeneza mgomo baridi.

Baada ya tukio hilo, nyeti zinadai, muandaaji huyo aliwataka washiriki hao kushuti walau hata ‘kapo' moja (mke na mume) kati ya saba zilizotakiwa kushutiwa huku akiwaahidi kuwapatia maslahi yao lakini pia walimtolea ‘out' kama siyo nje.

Sakata hilo lilizidi kuchukua ukurasa mpya mweusi kwa wasanii kuanza kuulizia zawadi ya mshindi wa pili itakuwa nini kitu kilichodaiwa kumtibua zaidi muandaaji huyo na kuamua kuwatafuta wawili kati yao ili kushuti hatima ya zoezi hilo.

Mgomo wa kuendelea na shoo hiyo iliyoanza kujipatia umaarufu Bongo uliwahusisha Michael Philip ‘Kojaki', Hemed Suleiman, Said Juma ‘Chege', Ali Baucha, Mwasiti Almasi, Nikita, Maureen, Lani na Pili aliyekuwa mwalimu wao.

Baada ya kuona washiriki hawaeleweki, jamaa aliamua kutafuta uwezakano wa kukinusuru kipindi hicho kwa kuwaomba wasanii Witness Mwaijage na More Love washuti ‘sini' moja tu ili apate kitu cha kurusha hewani na kumaliza shindano hilo.

Hivyo, Jumapili iliyopita, Serebuka ilifikia mwisho bila kutangazwa mshindi tofauti na ‘sera' za shindano hilo.

Mambo hayakuishia hapo, Juni 8, 2010 muandaaji huyo anadaiwa ‘kuwakimbia' baadhi ya washiriki pale walipokutana katika Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo walikwenda kwa ajili ya kutatua mgogoro ambapo wengi walikuwa wakidai pesa zao.

Ijumaa lilipomsaka kwa njia ya simu ya mkononi muandaaji wa shindano hilo aliyefahamika kwa jina moja la Ludovick hakupatikana hewani mara moja.

Wiki kadhaa nyuma, gazeti damu moja na hili, Risasi liliandika kuhusu kumeguka kwa shindano hilo ambapo baadhi ya washiriki waliamua kujitoa wakidai kuwepo kwa ‘longolongo' katika zoezi zima.

Mratibu huyo alipoulizwa alisema si habari za kweli, ila akajitetea kwa kusema kuwa, yeye hakuwa tayari kufanya kazi na watu wanaopenda ‘kilaji' (pombe).


source:globalpublisher's web
 
ili ndio tatizo la wasanii wa bongo, mnaanzaje kazi kabla hamjaingia mkataba, ina maana hata advance hawajachukua?
 
Mie alipojitoa mtalaam mwenyewe Masoud Masoud katika meza ya Majaji akisema kuwa anaona mambo yanakwenda ndivyo sivyo nikahisi kutakuwa na ukungu mbeleni.

Afu baadae ikaja shutuma kuwa mshindi anajulikana tayari kutokana na kupewa nyimbo nzuri wakati wakijiandaa haya yalikuja kutoka kwa washiriki wenyewe!!..Ila kilikuwa kipindi kizuri kuibembelezea J2.. wacha tusukume mwezi na Hiz WC
 
bora tu ilivyokufa, sikuona maana kwenye ile kipindi zaidi ya wauza sura tu
 
hahahahaa mbavu zangu
nilikiangalia kama mara 2 ivi,sikuweza tena
ata hawaeleweki
 
ARRRASTAVISTRA!!! Tutamiss michango ya Mzee Zahir Ally, jamaa anajua mambo mengi na ana upeo ni raha sana kumsikiliza..

TBC bwana, kila kitu wanataka !!!! lakini vinawasumbuaa!!
 
Hahaha mimi kipindi hakikua na mvuto kwangu hata kidogo hivyo wala sikua nakiangalia kikianza tu naenda kwa dk. ndodi marudio.
 
Back
Top Bottom