Sera za Ubepari hazitatusaidia kama nchi

Inaweza kukubalika au kutokukubalika both ways are possible

Je ubepari kama sera kwa faida ya nani..
Ahhh mkuu wangu hata sijui niseme nini kwa sababu sisi tunaiga vitu ambavyo havilingani na mazingira yetu. Kwanza kabisa mrengo wa KULIA (conservatives) ulitakiwa utokane na misingi ya Uhuru wetu na dira tulochukua ktk ujenzi wa Taifa letu. Kisha Upinzani wa kifikra ungekuja kupingana na misingi hiyo kuunda mrengo wa KUSHOTO na maadam siasa zinaambatana na Uchumi basi tofauti za sera zingejitokeza kulingana na imani tangulizi.

Hivyo, nijuavyo mimi Kisiasa, Ubepari hauna mrengo kwa sababu dhumuni la Uhuru wetu halikupingana na wananchi kumiliki mali, wananchi wetu waliweza na wanaweza kumiliki mali na Utajiri maadam wanafuata sheria na wanalipia kodi. Isipokuwa UKOLONI MAMBOLEO ndio ungekuwa mrengo wa - KUSHOTO, pinzani na ule tulowang'oa wakoloni na kutaka hifadhi ya mali, mila na desturi zetu ambapo sisi Watanzania tulikuwa wamiliki na tulipigania Uhuru kuhakikisha njia kuu za Uchumi zipo mikononi mwa wananchi..Then ktk policies au niseme sera ndipo tungeona Kushoto ambao wanataka turudishe uwekezaji wa wageni (ukoloni mamboleo) dhidi ya zile za kuwawezesha wananchi wenyewe (utajirisho) ktk imani ya kwamba Tanzania itajengwa na Watanzania, dhana ambayo ilitangulia harakati za Uhuru wetu..

Leo hii Chadema kama vyama vinginevyo, wamesimama kati kwa maana ya kutumikia mrengo na sera za wazungu ambao wamezijenga itikadi hizi kulingana na mazingira yao. Tunachokifanya sisi leo hii ni kuiga, kutafuta ustaarabu wa wazungu aidha tunavaa suti wakati ni jua kali la nyuzi 40 ama tunafuga ng'ombe wa Kizungu ili tupate maziwa mengi zaidi hali consumption ya maziwa nchini haijaongezeka ingawa ng'ombe wetu wanatosheleza matumizi yetu kabisa isipokuwa pengine it's out of fashion na Uncivilized kwa macho yetu kama tulivyofundishwa.

Kwa hiyo tunajipa mitihani migumu zaidi kutokana na kubeba vitu vya Ulaya na kujaribu kuvipandikiza Tanzania na visiweze kuota. In all naweza sema tumechukua mbegu za mti wa Mapleleaf kujaribu kuzalisha miti hiyo inayohitaji maji mengi sana hali mazingira yetu yanakumbwa na ukame, na kwa sababu tu miti hii ina kivuli kizuri sana kuliko Mchongoma wa Tanzania. Leo tunafuga zaidi kuku wa kizungu, nguo na mavazi yetu ni ya kizungu au kiarabu, vyakula vya makopo kutoka nje na kadhalika ili mradi tunamtumikia bwana wetu, Uzalishaji wetu wenyewe ni Zero. hapo tu tayari tumeshapoteza dira!

Mwisho wa yote Ubepari sii tena mrengo bali ni UCHUMI wenyewe unayoziweka njia za uzalishaji mikononi mwa wananchi badala ya serikali na tumekuwa Mabepari kabla hata mkoloni hawajafika nchini..Hivyo kufikiria kwamba Ubapari umeshindwa ni muhimu zaidi tukumbuke maneno ya mwalimu alipokuwa akizungumzia Ubepari kwa kupitia soko huria na Wall street, imani ya Uchumi wa puto (baloon) ambao mali zinapigwa bei pasipo kuwepo sokoni tukitumia imani ya kufikirika...Mfumo huu ndio utaanguka lakini Ubepari utabakia palepale kwa sababu ulikuwepo toka enzi za Ibrahim..
 
Nimelipenda jibu lako.
Free market economy ndio order of the day dunia nzima kwa sasa, hata hao wanaojiita wakomunisti/wajamaa (China, Russia, Cuba etc) nao wameingia kwenye soko huria.
Free market economy has been there for days in the eastern block....but the west didn't want to trade with the east. Even now, Cuba found 6billion barels of oil, the embargo is still on, China is stepping in, US is hating.....reason, "environmental concerns" - Fareed Zakaria, 18th sept 2011.
 
Ahhh mkuu wangu hata sijui niseme nini kwa sababu sisi tunaiga vitu ambavyo havilingani na mazingira yetu. Kwanza kabisa mrengo wa KULIA ulitakiwa utokane na misingi ya Uhuru wetu na dira tulochukua ktk ujenzi wa Taifa letu. Kisha Upinzani wa kifikra ungekuja kupingana na misingi hiyo kuunda mrengo wa KUSHOTO na maadam siasa zinaambatana na Uchumi basi tofauti za sera zingejitokeza kulingana na imani tangulizi.

Hivyo, nijuavyo mimi Kisiasa, Ubepari hauna mrengo kwa sababu dhumuni la Uhuru wetu halikupingana na wananchi kumiliki mali, wananchi wetu waliweza na wanaweza kumiliki mali na Utajiri maadam wanafuata sheria na wanalipia kodi. Isipokuwa UKOLONI MAMBOLEO ndio ungekuwa mrengo wa - KUSHOTO, pinzani na ule tulowang'oa wakoloni na kutaka hifadhi ya mali, mila na desturi zetu ambapo sisi Watanzania tulikuwa wamiliki na tulipigania Uhuru kuhakikisha njia kuu za Uchumi zipo mikononi mwa wananchi..Then ktk policies au niseme sera ndipo tungeona Kushoto ambao wanataka turudishe uwekezaji wa wageni (ukoloni mamboleo) dhidi ya zile za kuwawezesha wananchi wenyewe (utajirisho) ktk imani ya kwamba Tanzania itajengwa na Watanzania, dhana ambayo ilitangulia harakati za Uhuru wetu..

Leo hii Chadema kama vyama vinginevyo, wamesimama kati kwa maana ya kutumikia mrengo na sera za wazungu ambao wamezijenga itikadi hizi kulingana na mazingira yao. Tunachokifanya sisi leo hii ni kuiga, kutafuta ustaarabu wa wazungu aidha tunavaa suti wakati ni jua kali la nyuzi 40 ama tunafuga ng'ombe wa Kizungu ili tupate maziwa mengi zaidi hali consumption ya maziwa nchini haijaongezeka ingawa ng'ombe wetu wanatosheleza matumizi yetu kabisa isipokuwa pengine it's out of fashion na Uncivilized kwa macho yetu kama tulivyofundishwa.

Kwa hiyo tunajipa mitihani migumu zaidi kutokana na kubeba vitu vya Ulaya na kujaribu kuvipandikiza Tanzania na visiweze kuota. In all naweza sema tumechukua mbegu za mti wa Mapleleaf kujaribu kuzalisha miti hiyo inayohitaji maji mengi sana hali mazingira yetu yanakumbwa na ukame, na kwa sababu tu miti hii ina kivuli kizuri sana kuliko Mchongoma wa Tanzania. Leo tunafuga zaidi kuku wa kizungu, nguo na mavazi yetu ni ya kizungu au kiarabu, vyakula vya makopo kutoka nje na kadhalika ili mradi tunamtumikia bwana wetu, Uzalishaji wetu wenyewe ni Zero. hapo tu tayari tumeshapoteza dira!

Mwisho wa yote Ubepari sii tena mrengo bali ni UCHUMI wenyewe unayoziweka njia za uzalishaji mikononi mwa wananchi badala ya serikali na tumekuwa Mabepari kabla hata mkoloni hawajafika nchini..Hivyo kufikiria kwamba Ubapari umeshindwa ni muhimu zaidi tukumbuke maneno ya mwalimu alipokuwa akizungumzia Ubepari kwa kupitia soko huria na Wall street, imani ya Uchumi wa puto (baloon) ambao mali zinapigwa bei pasipo kuwepo sokoni tukitumia imani ya kufikirika...Mfumo huu ndio utaanguka lakini Ubepari utabakia palepale kwa sababu ulikuwepo toka enzi za Ibrahim..

Kwa hiyo unachosema ni kwamba chadema wameiga neno ubepari lakini infact "hawawezi kuelezea unawezaje kufaidisha wananchi wake"

Sasa si watafuate local name ys sera yao kama ccm wanavyosema ujamaa na kujitegemea through wawekezaji?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom