Sera za Majimbo ni za Lazima! Asiyetaka ahame Nchi!

I hate sare ya majimbo, sehemu ambazo hakuna resources za kutosha na ambazo zipo nyuma kimaendeleo, zitaendelea kudidimia. Híi tuliyonayo ni nzur, sema viongoz sio wazur. Tatizo sio system tatizo ni viongozi. Kwa sera za majimbo count me out!
mkuu yale majmbo yasio na resource yatajulikana na yatatafutiwa njia bora za kujiendeleza.
 
Jamani kuweni makini sana mnavyozungumzia states... it is easier to say Zanzibar state government, Tanganyika State Governement na Federal government of Tanzania.. kwa sababu historically they were independent state... kwa sasa sio muafaka kugawa taifa hili ambalo liko fully integrate na mipaka ni ishara tu ya kusaidia ****-manage... hivi mwanamume uliyezaliwa Moshi... ukakutana na Mhehe... Shinyanga na sasa Unaishi penda.. where will you pride be... tuache kujadili vitu as if the nation does not have story....

Tungekuwa states zinazoungana kama United State of America it could make sense... lakini sisi sio... we just need to continue improving our local government system ambayo already iko kwenye katiba ya nchi... sio kweli kwamba ni kitu kidogo... hata nyerere alipenda sana kulielezea hili... tuendee ku-evolve... taratibu serikali kuu, central government ijitoe every time local govenrment inavyoweza kuwa na capacity to manage... serikali iendelee na kuwa na role ya governance only.

To Tanzanians: not everything needs revolutions...

Tanzania ina mfumo wa majimbo lakini ina improve kwa system ya evolution wakati wenzetu wanataka iwe revolution... hizi ni adhari za kutawalia, kwamba we do not believe to have our own system rather lazima tu-copy....

Mkuu umeanza kugawa watu na makabila yao!! hatuko huko....kuna wachaga wako mpaka kijijini kwetu wilaya ya tukuyu vijijini! wanaishi huko, wanalima na kufanya biashara! haina maana sera hii ikianza ndio waondoke..

sera ya majimbo ni ku-empower watu wa chini wafanye maamuzi yao wenyewe, how they make money, how they collect tax, how they use their own money!!how they plan locally for the betterment of their society

Leo hii hatujui kodi zinaenda wapi! zinafanya nini na kulazimu akina Bonge kupanda migomba barabarani!

Leo hii sehemu au wilaya zilizoendelea hazijaendelea kwa sababu ya serikali imeamua...la! ni kwa sababu kuna waziri fulani au mbunge fulani ana nguvu...say haingii akilini nchi moja, leo tunalia barabara ya kwenda mtwara! wakati ya kwenda mbeya kuna mkeka!! wote hawa wanatoa kodi sawa, priority ziko sawa na kwa pato la taifa mtwara wako juu ni ya saba, leo pengine bila mkapa isinge jengwa...........na baada ya kuondoka leo kuna kipande cha km 60 sijui kitaisha lini!! mifano iko mingi....nenda kilimanjaro vijijini kuna barabara zina lami!! utachoka, wakati kigoma au rukwa km za lami zina-tembeka kwa miguu!!

Hizi LG za sasa zimejaa wezi ambao hawako accountable kwa jamii bali kwa vyama vyao!
 
Mkuu wazo na sababu ziku zote huwa vinapita sana kuliko kama wengine wanafanya au la!

Najua utakuwa graduate wa UDSM......desa kwanza

anyway , ni nchi nyingi, Nigeria, Indonesia, USA, Canada, ............

Hapana mkuu wangu, hata katika research kuna literature review, tena inashauriwa uangalie jamii yenye mfanano kiasi na

ile unayotaka kuifanyia utafiti. Lazima ujue nani anafanya hivi, amefanyaje? faida na hasara zake? na kwa vipi wewe unaweza kuovercome zile hasara za lile jambo.

Canada,USA na zinazofanana na hizo haziwezi kamwe kuwa reference kwa TZ ukizingatia kiwango cha maendeleo na elimu ya ujumla ya wananchi wake.

Ila ni wazo zuri lakini linahitaji research ya nguvu la sivyo tumeingiza migogoro ya kikanda na kikabila nchini
 
Waberoya,

..mimi naomba kujua hayo majimbo mnayopendekeza yatakuwa na mamlaka gani.

..Ghana,Kenya,Nigeria,Iraq,Afghanistan,Pakistan, India, Congo-Kinshasa, USA, etc etc kote huko kuna majimbo lakini pia yanatofautiana kimamlaka na kiutendaji kazi.

..nilipata nafasi ya kuchunguza mfumo wa majimbo ya Ghana. I did not find enough material about it lakini niliona kwamba wakuu wa majimbo ya Ghana wanateuliwa na Raisi kitu ambacho nadhani wa-Tz hawatakipenda.

..kwa mtizamo wangu hakuna mfumo usiokuwa na matatizo. kama ni suala la upotevu wa rasilimali zetu, Nigeria wanayo majimbo lakini bado wananchi wanaotoka maeneo yenye mafuta hawajaweza kufaidika na rasilimali hiyo. nimeleta mfano wa Nigeria na mafuta yao kwasababu kila mara wa-Tz tunapozungumzia majimbo basi tunatumbukiza na hoja za rasilimali na maliasili.

..binafsi naamini majimbo yata-reverse mafanikio yaliyopatikana katika kujenga utaifa wa Mtanzania. Bado hatujafanikiwa vya kutosha ktk kuuzika ukabila, pamoja na udini, ktk jamii yetu, sasa tukirudi kwenye majimbo matatizo hayo yanaweza kuchomoza tena kwa kasi na kuleta instability ktk jamii yetu.

..kuna nchi zina mfumo wa majimbo lakini zina matatizo na hali mbaya kutushinda wa-TZ. mapendekezo yangu ni kuuboresha mfumo tulionao badala ya kuanza na mfumo mpya ambao hatuna uhakika kama utaleta mafanikio kuliko huu tulionao sasa hivi.

Joka kuu!

Yes I agree with u, kama leo hii wakuu wa mkoa, wilaya n.k watachaguliwa kwa kura na hawatawajibika kwa rais moja kwa moja basi inaweza kuwa poa.....

so ye partly I can agree with u...sasa we sema tuboreshe vipi..........ukiboresha sana ku-empower mikoa ndio LENGO lenyewe!
 
Hatuhitaji majimbo ili kuweza kuyapata hayo aliyoyaorodhesha waberoya, infact kwa system hii tuliyokuwa nayo tunaweza kuyapata hayo iwapo (1) sheria tunazozitunga zinafuatwa vizuri (2) viongozi wetu wanafanya kazi vizuri na kwa moyo wa kizalendo (3) wananchi kuwa alert na pia kuhakikisha wanawawajibisha viongozi wao (4) mipango na sera zinazotungwa ziwe nzuri na kusimamiwa vyema tanzania si nchi kubwa ya kushindwa kuwa governed iwapo tuko serious, kiufupi ni kwamba kama tumeshindwa kuigovern tanzania ambayo inazidiwa ukubwa na jimbo moja la xinjiang la china, basi usitegemee kwamba hata hayo majimbo yanaweza kuwa governed vizuri( wenye ueledi wa kanuni ya mathematical induction wanaweza kunipata nazungumzia nini). Nchi zinazopaswa kugawanywa katika majimbo ni zile (1) zenye eneo kubwa sana na population kubwa. Kwa standard ya eneo la tanzania na population yake ya watu milioni 45, mfumo wa sasa wa mikoa chini ya serikali kuu unatufaa sana, kinachotakiwa ni kuziongezea serikali za mikoa na wilaya nguvu fulani fualani katika kufanya maamuzi katika mikoa hiyo, lakini sera kuu ipangwe na serikali kuu ikishirikiana na mikoa husika. Hasara za serikali ya majimbo kwa nchi kama ya tanzania ni (1) udini majimbo yenye watu wa dini fulani wengi, yanaweza yakatrump religious minority katika majimbo husika. Hii inaweza ikasababisha backlash kwenye majimbo mengineyo na matokeo yake ukajenga nchi yenye tension ya udini vibaya sana. Kwa mfumo tuliokuwa nao sasa hii inaondoshwa na serikali kuu. Kama muasisi wa chadema mwenyewe mzee mtei ambaye ni msomi anaonekana yuko religious sensitive, unategemea nini kwa wale ambao wanatamani wawe na dola ya kidini uwape jimbo ambalo wao ndiyo majority?

Mkuu umeongea na umefika kwenye point............hilo ndilo lengo hasa, sasa serikali kuu haiwezi kuamua hayo...haiwezekani kwa serikali zetu za kifisadi hizi...watajaribu sana kuweaken hizo serikali

hujasikia kuwa kuna maeneo ambayo wakishabikia sana CCM haipati kabisa huduma za jamii?? why?? is it fair??
 
Naunga mkono hoja .Hao kina ridhiwani na wenzake wanaupofu wa kufikiri ndio maana hawajui wanalosimamia.Mfumo wa majimbo na mfumo wa Local gvt ambapo reform ilianza fanyika 1998 hauna tofauti sana,majimbo ni hatua ya juu zaidi ikilenga kuongeza ufanisi na kuwafikia wananchi kwa karibu kiutendaji na kiutawa na mara nyingi hatua ya majimbo utekelezaji wake ni rahisi husani kwa nchi kubwa kama Tanzania.

Huyu ridhiwani hana tofauti na ambao wanauhujumu mfomo wa Local gvt kwa maslahi yao binafsi.

Sishangai wakiubeza mfumo wa majimbo kwani hata mfumo uliogharimu fedha nyingi chini ya utawala wa CCM umekwamishwa na kuhujumiwa.Siri ambayo CCM hawaitaki ijulikane ni hizo faida za kuwapa wananchi mamlaka kamili ya kuamua mambo yao kiutawala na kiutendaji kwa manufaa ya nchi.Wanajua madudu yao ndio maana wanapinga wananchi kushikilia nyanja kuu za uchumi na kijamii . Hawa ni nyoka wenye sumu kali sana hawapaswi kupewa nafasi kwenye hadhira ya watanzani,wanataka wananchi tuendelee kuwa masikini huku tukiimba KIDUMU CHAMA CHA MAPINDU
 
Joka kuu!

Yes I agree with u, kama leo hii wakuu wa mkoa, wilaya n.k watachaguliwa kwa kura na hawatawajibika kwa rais moja kwa moja basi inaweza kuwa poa.....

so ye partly I can agree with u...sasa we sema tuboreshe vipi..........ukiboresha sana ku-empower mikoa ndio LENGO lenyewe!

Weberoya,

This is where you get it wrong and absolutely wrong.... do not mix Distric Commissioner with Municipal Mayor.... They are there for different roles and they are real important.

1. Distric Commisioner --- Represent Central Government in discrit level and he is responsible for execution of central government responsibility at district level and he is the head of all central government organs at the level,... Mkuu wa polisi, mkuu wa usalama, and anything for central government.
2. Municipal Mayor: this is the one you talk about.... he is responsible for local government, at the time being is selected by madiwani, but you can decided to be selected by people direct... this is majimbo you are talking about... in short Tanzania has majimbo... but the majimbo in Tanzania are called halmashauri/Manispaaa..... .... thus why central govenment can decide to have two majimbo in one district....

Please jueni nchi yetu kabla ya kukurupuka. Huwezi kuwa na 100% Local Government au Majimbo at Majimbo/District level... lazima kuwe na central government organs to supervise those organs that are centrall managed.
 
Waberoya,

Huo ni udikteta huwezi kusema mtake msitake wakati waamuzi wa mwisho sisi wananchi!. Hata kama hiyo sera ina faida lukuki lakini mwamuzi wa mwisho sisi wananchi na tukisema hatutaki baas!
 
Weberoya,

This is where you get it wrong and absolutely wrong.... do not mix Distric Commissioner with Municipal Mayor.... They are there for different roles and they are real important.

1. Distric Commisioner --- Represent Central Government in discrit level and he is responsible for execution of central government responsibility at district level and he is the head of all central government roles at the level,... Mkuu wa polisi, mkuu wa usalama, and anything for central government.
2. Municipal Mayor: this is the one you talk about.... he is responsible for local government, at the time being is selected by madiwani, but you can decided to be selected by people direct... this is majimbo you are talking about... in short Tanzania has majimbo... but the majimbo in Tanzania are called Manispaaa.....

Please jueni nchi yetu kabla ya kukurupuka. Huwezi kuwa na 100% Local Government au Majimbo at Majimbo/District level... lazima kuwe na central government organs to supervise those organs that are centrall managed.

bahati mbaya vyeo ulivyotaja vyote vimekaa ki-chama zaidi! sera za majimbo hazizuii kuwa na central government mkuu

hizi LG government au mayors zina/wana nguvu gani?? zinakusanya kodi, zinatengeneza mapato yao wenyewe?( zaidi ya mabango na kodi za masoko!), zinapanga matumizi ya kodi, zinaplan ya miaka 5 ijayo?? dont u see what we have is something functionless
 
Mkuu umeanza kugawa watu na makabila yao!! hatuko huko....kuna wachaga wako mpaka kijijini kwetu wilaya ya tukuyu vijijini! wanaishi huko, wanalima na kufanya biashara! haina maana sera hii ikianza ndio waondoke..
Pole ila mimi sio mkabila... if that how you perceive that is your right.

sera ya majimbo ni ku-empower watu wa chini wafanye maamuzi yao wenyewe, how they make money, how they collect tax, how they use their own money!!how they plan locally for the betterment of their society

Na sera ya local government ni empowerment au umeambiwa ni nini? Umesikia mara ngapi wabunge wajibiwa bungeni kwamba swali hilo muongelee kwenye vikao vyenu vya madiwani?
Leo hii hatujui kodi zinaenda wapi! zinafanya nini na kulazimu akina Bonge kupanda migomba barabarani!

Huu ni uongo, jifunze jinsi serikali za mitaa zinavyoendeshwa... umesikia mara ngapi kwamba manispaa ya temeke/ilala/uyui imepitisha bajeti ya soo... na umeona mara ngapi kwenye magazeti wakiweka mahesabu ya mwaka... kutosoma ni jambo lingine mkuu do not mix issues.

Leo hii sehemu au wilaya zilizoendelea hazijaendelea kwa sababu ya serikali imeamua...la! ni kwa sababu kuna waziri fulani au mbunge fulani ana nguvu...say haingii akilini nchi moja, leo tunalia barabara ya kwenda mtwara! wakati ya kwenda mbeya kuna mkeka!! wote hawa wanatoa kodi sawa, priority ziko sawa na kwa pato la taifa mtwara wako juu ni ya saba, leo pengine bila mkapa isinge jengwa...........na baada ya kuondoka leo kuna kipande cha km 60 sijui kitaisha lini!! mifano iko mingi....nenda kilimanjaro vijijini kuna barabara zina lami!! utachoka, wakati kigoma au rukwa km za lami zina-tembeka kwa miguu!!
Mkuu barabara zote ambazo sio za kitaifa au kimkoa haziko chini ya central government ziko chini ya manispaa... it is clear kwamba central government haijamaliza barabara zote... lakini ukumbuke tu... bado less than 60Km kuwa na mkeka mpaka Mtwara....


Hizi LG za sasa zimejaa wezi ambao hawako accountable kwa jamii bali kwa vyama vyao!

True, is solution to rename them as majimbo or to sort out corruption issues?

Indeed mimi sijaona hoja... i'm still read to learn... but i caution people not to give simple answer to complex question, policy related and even constitution related like this.... be carefully guys
 
Waberoya,

Huo ni udikteta huwezi kusema mtake msitake wakati waamuzi wa mwisho sisi wananchi!. Hata kama hiyo sera ina faida lukuki lakini mwamuzi wa mwisho sisi wananchi na tukisema hatutaki baas!

Mkuu lugha ya mamlaka hiyo!! yaani umeniona rais tayari?? nina nguvu gani wakati hata sura na jina langu kamili ni HIDDEN!
 
bahati mbaya vyeo ulivyotaja vyote vimekaa ki-chama zaidi! sera za majimbo hazizuii kuwa na central government mkuu

You get it wrong once again... who appoint the distric commisioner... for now it is head of the state... but this can be discussed... in any case they will be people accountable to the central government and not to the local government. Ila ku-discuss this is not a problem... but ni uongo mkubwa hata kwa Mungu kusema tanzania haina utawala wa majimbo,,, wakati tume ya uchaguzi kila siku inatangaza mbunge wa jimbo x amefariki uchaguzi utafanyika x day.

hizi LG government au mayors zina/wana nguvu gani?? zinakusanya kodi, zinatengeneza mapato yao wenyewe?( zaidi ya mabango na kodi za masoko!), zinapanga matumizi ya kodi, zinaplan ya miaka 5 ijayo?? dont u see what we have is something functionless

Soma katiba ya sasa mkuu... imewekwa kwenye katiba... na kinachotokea serikali ya Tanzania inaendelea kuwaachia madaraka... this is what Kikwete is proud of ... evolving giving the the power...

Hili sio wazo jipya fuatilia vizuri serikali za mitaa zinavyoendeshwa na sheria zake... utaona serikali za majimbo ziko... sasa issue ya idadi, appointment these can be discussed...

Kwa mfumo wa sasa halmashauri zote ni majimbo... ila kwa definition yenu na CDM mnataka kurudisha provinces zile za ukoloni... wish you all the best...
Ila hili hamtakuwa wagunduzi b'se these idea are they and are working...

Unakumbuka kwa nini Waziri Mkuu aliambiwa amevunja katiba kwa kuwa na Tume ya Jiji ya Keenya? do you remember....
 
Serikali za Mitaa a.k.a majimbo kwa upepo wa kisasa.... kwenye katiba ya Tanzania toleo la 77.

SURA YA NANE MADARAKA YA UMMA​
145. Serikali za Mitaa.​
146. Kazi za Serikali za Mitaa.


145​
.-(1) Kutakuwa na vyombo vya Serikali za Mitaa katikakila mkoa, wilaya, mji na kijiji, katika Jamhuri ya Muungano, ambayo vitakuwa vya aina na majina yatakayowekwa na sheria iliyotungwa na Bunge au na Baraza la Wawakilishi.(2) Bunge au Baraza la Wawakilishi, kadri itakavyokuwa, litatunga sheria itakayofafanua utaratibu wa kuanzisha vyombo vya Serikali za Mitaa; miundo na wajumbe wake, njia za mapato na utaratibu wa utekelezaji wa shughuli za vyombo hivyo.
====>Also refer Serikali za MitaaSheria ya 1984 Na.15 ib.50

146.-(1) Madhumuni ya kuwapo Serikali ya Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi. Na vyombo vya Serikali za Mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki kuwashirikishawananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wa maendeleo katika sehemu zao na nchini kote kwa jumla.(2) Bila ya kuathiri maelezo ya jumla yaliyomo katika ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, hiki chombo cha Serikali za Mitaa, kwa kuzingatia masharti ya sheria iliyokianzisha, kitahusika na shughuli zifuatazo -(a) Kutekeleza kazi za Serikali za Mitaa katika eneo lake;(b) Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na ulinzi wa wananchi; na(c) Kuimarisha demokrasi katika eneo lake na kuitumia demokrasi kuharakisha maendeleo ya wananchi.
====>Also refer Kazi za Serikali za Mitaa Sheriaya 1984 Na.15ib.20
 
sikubaliani na hiyo hoja na nchi sihami na chakunifanya huna. siku nyingine utakuja na uzi wa kuhusu katiba na uhuru wa wananchi kuchagua sasa leo unawalazimisha sasa haki yao ya uhuru kuamua umeizingatia?
next tym weka hoja kistaarabu great thinkers nvr ask for attention they are jst given
 
mnazifahamu changamoto wanazozipata watendaji wa Halmashauri kutoka serikali kuu

pasipo dhamira na nidhamu yatajirudia ya wa serikali kuu kutisha kuzifuta HAlmashauri na hata kuziona si chochote ktk kutatua kero za wananchi
 
Mapato yatakayo patikana katika majimbo mengi yatakayo anzishwa hayataweza kulipa gharama za wafanyakazi waliopo katika majimbo husika hapo mtafanyaje? Manake 90% ya kodi inatoka dar we huoni bomu hilo
Mzinga,
Kwa hali ya kawaida ni vigumu ku manage Overhead ambazo zinazidi kipato. Tatizo tulilonalo kwenye Halmashauri zetu nyingi ni kuwa na watumishi wengi kuliko mahitaji kwa kuwa wanajua Mishahara yote Hazina inacover through Block Grant. Ndiyo maana kwenye Halmashauri nyingi unakuta kuna Wahasibu 60, Madereva 90, Wahudumu 50, Maafisa Utumishi 15, nk na hadi wengine wanawekwa Pool. Hilo la kwanza.

La pili. Kitendo cha Dar kuchangia almost 90% ya pato la Taifa ni matokeo ya Mfumo tulionao ambao umekuwa ukichochea ujenzi wa vitega uchumi kwenye miji mikubwa. Wawekezaji wanawekeza sana Dar ili ku realise inherent benefit za Dar against other Regions.

TUMBIRI wa JF..

 
Last edited by a moderator:
PYAAAA!!!! KAMA BATA KANYA.
WANALAZIMISHA,WAMEVUNJA KATIBA YA JMT IBARA YA 18/19.

Unajua kuna kipimo cha ujinga na upumbavu lakini heri mjinga maana anaweza kueleweshwa na mpumbavu katu anajua ukweli ila anaupindisha kwa faida zake

Ridhwan Kikwete na wana CCM wenzie ni moja ya makundi dhaifu kiakili na kihuhalisia, huku kundi linguine la wenye ulemavu wa akili ni baadhi ya wanachadema ambao ni fuata mkumbo, wasiozijua seraza chama chao na hawawezi kuzitetea..poleni!


Faida za sera za majimbo


1. Faida za utawala

Sera za majimbo zinaweza kabisa kufananishwa na Decentralisation system, ambako maamuzi hufanywa na watu wa chini kabisa, kwa jambo husika na kwa wakati husika.

Wananchi wanapewa uwezo wa kujitafuatia uongozi wao, na hivyo kumjweka mtu ambaye anajua mazingira ya eneo hilo, shinda walizonanzo na way forward kuzitatua. Mtu huyu pengine anajua utamaduni wa eneo husika, tabia zao na kupanga mikakati ya kujikwamua kutokana na walivyo.

Kwa kifupi ita improve quality of decision kwa jambo loloye liwe kwa eneo husika kitu ambacho hakipo kwa sasa

2. Faida za uchumi

Mtu yeyote mjinga na asiyeelewa ni yule anayedhani au kufikiri kuwa kuna maeneo nchi hii ni maskini na mengine ni tajiri.

Kansa ya mawazo haya iko kwa viongozi wa CCM na serikali yao wakihubiri kuwa majimbo ni mifarakano na wengine watakuwa maskini
Sema jimbo gani ni maskini, nitakueleza wafanye nini kupata utajiri..

Hakuna kijiji, mkoa au wilaya maskini Tanzania haipo!!! Umaskini ukiwapo ni wa ubongo mdogo wa raia wa mahali hapo

Sera ya majimbo itaharakisha maendeleo kwani ita ‘motivate’ au ku’stimulate brain za watu wa eneo husika kuwaza na kufikiri kipi kifanyike kuleta maendeleo

Wataalamu wa sosholojia wanatanabaisha kuwa, jamii inayotengeneza sere zake, au kuamua mambo yake hufanya kazi kwa bidii ili maamuzi na malengo waliyoyaamua yafikiwe….kwa mfano sera ya kilimo kwanza haitaweza kufanikiwa kwa sababu haijaamuliwa na wananchi na haijaingia akilini au mioyoni mwao ..kwa nini ‘kilimo kwanza’ hata kama sera hii ni nzuri!!

Ni matatizo waliyoyapata akina Nyerere enzi hizo..wakati mpaka leo hii israel ina vijiji ya ujamaa kama alivyoanzisha Nyerere sisi vyetu havipo na kama vipo ni kibahati tu!!

Leo wengi hawajui wilaya ya Mbinga ndiyo tajiri kuliko zote Tanzania kwa kilimo cha kahawa, ufugaji na sasa wanapanda miti!!Nani anajua kuwa mkoa wa mtwara ni wa saba kuliingizia pato taifa?

Au hamjui kuwa wilaya za Ngaka, kiwira zina makaa ya mawe na liganga kuna chuma, nani asiyejua utajiri wa madini na kilimo morogogoro na mazao ya madawa mkoa wa Pwani?

Au nani asiyetamani kuona utajiri za zabibu Dodoma unavuka mipaka na kushindana na Israel ambayo inategemea zabibu kwa sana
Tanzania haina sehemu maskini, J

Juzi Mkongeumeongelewa sana, Mafuta na ziwa ni utajiri wa Kigoma na Rukwa inasifika kwa kilimo…semeni tujue wilaya maskini ni ipi?

Au haiumi kuona Lindi na Mtwara wana gesi ambayo inasafirishwa kuletwa DSM huku wao wakihangaika kucheza ngoma kwa kukosa kazi??

Haiumi kusikia Tanzania ni wazalishaji wakubwa wa dhahabu duniani uku wilaya husika ni maskini wakutupwa, au Almasi ya shinyanga ikiliwa kimya kimya!!! Kweli asali ya tabora na kijani cha Bukoba sio mtaji wa maendeleo ya taifa hili? Nani anabisha??

Sera hii italeta ushindani wa majimbo katika kuongeza kipato cha kaya, kijiji, kata, jimno na taifa!!

Dubai wameweza kuuweka mji wao kuwa sehemu ya kibiashara duniani sehemu ambayo ni jangwa kabisa!!

Kama kuna sehemu kuna jangwa, basi tutaweka DAR LIVE nyingi sana (Ridhwan tenda hiyoo dogo), na starehe nyingine zote ili watu wakipiga kazi ngumu wanaenda kupumzika na kujiburidisha sehemu ambazo zitakuwa haziwezekaniki..japo hamna hizo sehemu

3. Faida za kulinda utamaduni

Hakuna utumwa mbaya na wa kipekee kama kuacha tamaduni zetu, tumeiga wazungu mpaka wanatushangaa, vijana wetu wamekuwa kama mabinti, eti wanabana pua na MASCULINE behavior haipo!!

Malezi duni!!!
Kijana gani leo yuko tayari kupigana na kusema msitu huu wa baba yangu, na yuko tayari kuua simba na kulinda hadhi za kikoo, kifamilia, kikabila na hatimaye taifa??

Sera majimbo japo zimejikita ki-uchumi zaidi, lakini zina faida kubwa sana hata kiutamaduni

Utamaduni wa eneo husika huleta ubunifu wa eneo husika na kuongeza hadhi ya eneo hilo…leo hatuangalii nyimbo za wamasai ila tunanunuA MAKHIRIKHIRI kwa raha zooote huku tukijiona tumeendelea!

Kumbuka pia utamaduni hapa pia ni kurithisha vizazi vijavyo mambo ambayo kizazi cha sasa kinafanya, kama kulima, kufuga nyuki, kuchimba madini , kutengeneza vitu mbali mbali! kurithisha kizazi kijacho.......this is called informal education which is sometime far better than formal education!!

kuna faida gani kumaliza na degree uchwara ya uhandisi wa ujenzi na huwezi kazi wakati kuna fundi aliyejifunza tangu utotoni alianzia kubeba vifaa vya baba yake!!! anajua kila kitu kuliko injinia aliyekuwa na stress za bodi ya mikopo na shida za kukosa vifaa vya mafunzo??


4.
Faida ya kukusanya mawazo

Unapoona mwenzio kaendelea utajiuliza how? Kafanyaje? Maendeleo ya baadhi ya sehemu Fulani Fulani zitaleta ‘data collection’ na mawazo kuwa kwa nini wengine wameendela wanafanyaje fanyaje.

Sera za majimbo zinaweza kupelekea kubadilisha sera za uongozi wa taifa na kufikia kufanya maamuzi ambayo huwezi kuyajutia na una mifano yake.


5.
Kulinda Rasilimali za Taifa

Kumbuka ikiwa kama majimbo yatagawanywa na kuwa mfumo wa states….basi taifa la Tanzania lina weza kuitwa ‘United Sates of Tanzania’ majimbo ambayo yana dola ya local na kitaifa, kulinda maeneo husika.

Ukiwa na mali lazima ulinde mali…kutorosha vitu kama wanyama hakutakuwepo, kuiba michanga ya madini hakutakuwepo, kukata miti ovyo na kuuza kwa bei ya kutupa hakutakuwepo!!! Do I need to say more here??...no!


6.
Kujenga Taifa Imara na viongozi wazuri wa kitaifa


Tuna taifa dhaifu kwa sababu tuna viongozi dhaifu! Tuna viongozi dhaifu kwa sababu tuna taasisi dhaifu, tuna taasisi dhaifu kwa sababu tuna familia dhaifu!


Taasisi kama uongozi wa ngazi mbalimbali ukiwa makini unaleta viongozi makini, taasisi hata za kidini zinaweza kuchochea kupata viongozi wazuri na akina baba wazuri
Ikiwa tyuna kiognozi wa jimbo Fulani aliweka strategy za kupata maendelao na yakaoneka, je hawezi kuwa ndio candidate mzuri wa wizara husika na hata taifa??

Viongozi watakuwa judged na kazi zao za kwenye majimbo na tutakuwa na hakika ya kuwa atafanya jambo akiwa rais let say…sio kuwa na viongozi vimeo kama hawa wasasa ambao haujui katoka wapi, kafanya nini, anaweza nini, unashtukia tu kiongozi na kesho mnalia HAWEZI…kwani nani alisema anaweza??


7.
Mwingiliano wa watu


Uzuri wa sera hizi kwa sababu tunaongelea taifa moja, mtu ataishi sehemua mabayo anajua atazichanga. ‘atatoka’ atatengeneza fedha kulingana na akili zake na ujuzi wake!! Hili huleta maendeleo ya haraka kwa wenye akili! Sio wanaokalia majungu, kuchezabao na kuwaza uchawi!

Sera za majimbo kwa maendeleo ya Taifa, kumbuka kuna limitation zako au hasara zake, japo ni ndogo sana kw ataifa letu change sera za majimbo is not a matter of discussion…is a must!!

8. Kodi husika

Kodi inakatwa kulingana na eneo husika, kwa mfano kodi ya jimbo la Ontario nchini kanada iko tofauti na kodi ya British Columbia japo wako nchi moja, ukasanyaji wa kodi utakuwa rahisi na itafanya kazi iliyokusudiwaLeo hii kaodi zetu hatujui zinafanya nini na haujui umuulize nani! Aibu

9. Watu watapungua DSM (miji mikubwa) ha ha ha ha!!

I hate DSM but I am in!..ila nina kazi yangu na some prospects…ila naona watu wakitaabika, hawajui wafanye nini, hawana future, asubuhi tunajaziana foleni wengine wakiwa na decent jobs wengine hawana na cha ajabu ambao hawana kazi wanaishi maisha mazuri kabisa…sisi wafanya kazi tunakatwa kodi kubwa na ilimradi vituko tupu

Hawa wenyeji wengi waDSM ambao ni jobless ambao wanaweza kwenda elfu arobaini kwenye msiba wa kanumba siku ya kazi asubuhi..wakisikia wenzao mikoani wanazalisha na maisha yao yanaenda vizuri watarudi tu!!

Hata kama wasipoondoka hawa kwasababu wameishalemaa at least tutazuia watu kukimbilia mijini. Maisha ya bahati bahati , maisha yasiyo na muda wala malengo…maisha ambayo unatoka nyumbani saa kumbi na mbili na kufika kazini saa nne!!

Unafikia chai,kucheza karata kufacebook kidogo, lunch na unasinzia kidogo saa tisa unaanza kuangalia usafiri wa kurudi…asilimia 90 ya wafanya kazi wa serikalini ndio wanavyoishi!! Ha ha ha ha!


Watu hukimbilia mijini wakidhani ndiko kuna hela, sera ya majimbo itazuia hili! Japo hatari yake ni kuwa jimbo Fulani kukiwa kuzuri zaidi watu watakimbilia huko….

lakini kama wanazalisha is okay hakuna shida, siyo kama wakazi wa DSM wengi…hawaishi bali wanatafuta maisha!


10.
inatosha

wenu

Waberoya s. Waberoya

N.B huu sio uchambuzi wa sera rasmi ya chadema, maneno rasmi ya sera za chadema kuhusu hili , tafuta sera zake fika ofisi ya chadema iliyo karibu nawe utaipata, hapa nimeelezea tu kwa ufahamu wangu ubora wa sera hii, kumbuka pia kuwa mimi sio mwana chadema wala chama chochote cha siasa.[/QUOTE]
 
Serikali za Mitaa a.k.a majimbo kwa upepo wa kisasa.... kwenye katiba ya Tanzania toleo la 77.

SURA YA NANE MADARAKA YA UMMA​
145. Serikali za Mitaa.​
146. Kazi za Serikali za Mitaa.


145​
.-(1) Kutakuwa na vyombo vya Serikali za Mitaa katikakila mkoa, wilaya, mji na kijiji, katika Jamhuri ya Muungano, ambayo vitakuwa vya aina na majina yatakayowekwa na sheria iliyotungwa na Bunge au na Baraza la Wawakilishi.(2) Bunge au Baraza la Wawakilishi, kadri itakavyokuwa, litatunga sheria itakayofafanua utaratibu wa kuanzisha vyombo vya Serikali za Mitaa; miundo na wajumbe wake, njia za mapato na utaratibu wa utekelezaji wa shughuli za vyombo hivyo.
====>Also refer Serikali za MitaaSheria ya 1984 Na.15 ib.50

146.-(1) Madhumuni ya kuwapo Serikali ya Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi. Na vyombo vya Serikali za Mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki kuwashirikishawananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wa maendeleo katika sehemu zao na nchini kote kwa jumla.(2) Bila ya kuathiri maelezo ya jumla yaliyomo katika ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, hiki chombo cha Serikali za Mitaa, kwa kuzingatia masharti ya sheria iliyokianzisha, kitahusika na shughuli zifuatazo -(a) Kutekeleza kazi za Serikali za Mitaa katika eneo lake;(b) Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na ulinzi wa wananchi; na(c) Kuimarisha demokrasi katika eneo lake na kuitumia demokrasi kuharakisha maendeleo ya wananchi.
====>Also refer Kazi za Serikali za Mitaa Sheriaya 1984 Na.15ib.20

madaraka yapi hayo mkuu? unaweza kutoa mfano mmoja wapo

Madaraka sawa, madaraka bila pesa siyo madaraka,ndiyo nasema hiyo imekaa kisiasa na please imefanya nini for the past 50 yrs??

Ninachosema mimi, zipange mipango yao, njia za mapato yao, zikusanye kodi, zipange matumizi ya kodi, zichaguliwe na wananchi...n.k!! leo hizo serikali zinapata fedha toka serikali kuu tena not equally!! serikali kuu zimetoka wapi?

hizi zilizotajwa hapa eti "
-(a) Kutekeleza kazi za Serikali za Mitaa katika eneo lake;(b) Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na ulinzi wa wananchi; na(c) Kuimarisha demokrasi katika eneo lake na kuitumia demokrasi kuharakisha maendeleo ya wananchi''

a) kazi za serikali za mitaa ni zipi?
b) kuimarisha demokrasia?? really?

ulinzi na usalama sawa kabisa, hizo zingine mbili ziko kisiasa zaidi!! tuna vyama vingi sasa
 
Back
Top Bottom