Sera ya Kilimo na Mifugo imewasaidiaje Watanzania?

Jaribu kubadili swali lako maana ni pana sana.

Ila kwa kifupi swala la kupima ufanisi wa sera ni gumu sana hata kwa nchi zilizoendelea. Inahitaji muda mrefu na gharama za kutafiti katika kutengeneza ushahidi kwamba mabadiliko yalioonekana yasingetokea kama si sera husika.

Hata hivyo unaanza kujiuliza kuhusu mafanikio ya sera kama kuna mpango wa utekelezaji wa hiyo sera. Unaangalia ufanisi wa mpango wenyewe na namna unavyoshabihiana na mapendekezo ya sera, kisha unachambua mchango wake katika maendeleo...

Sasa tukianza kuangalia mpango wa maendeleo ya mifugo au pengine ASDP?, toka zianzishwe?, vp kuhusu value for money? je zimegusa matatizo halisi ya mkulima au mfugaji?...........mkuu hii inahitaji utafiti wa kina siyo value judgement.

Ila kwa mtazamo wangu kama lengo lako ni kupata snapshot ya endapo hii sera ina umuhimu kwa taifa letu mi naweza kusema ni NDIYO ingawa utekelezaji umekuwa mapungufu mengi ambayo siwezi kuyachambua hapa.
 
Faida zipo,kwa mfano watanzania sahv wamewekeza kwenye kilimo kwa kauli mbiu na makongamano,pili,yale maeneo yanayofaa kwa kilimo leo wawezekaji wamenyang'anywa na kupewa wakulima...tatu hata viongozi wetu leo wanaweza kusimamia kilimo kwanza kule vijijini kwa remote wakiwa wamekaa pale magogoni na kwingineko huku wanagonga glasi,faida ni nyingi sana kwakweli.
 
Rweye,
Umezungumza maneno magumu kidogo kwa sababu hoja yako ya pili kwangu mimi naona sijaielewa. Ningeomba, kwa faida yangu, pengine na wanajamii, ututajie ni maeneo gani ambayo wawekezaji walinyang'anywa na wakapewa wananchi. kwa sababu kelele za wananchi kuporwa ardhi zinaendelea hadi sasa. ni wapi please, japo kwa mfano kdogo tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom