Sera ya Chadema ya Usalama wa Taifa na Ulinzi ni ipi?

Mzee Mwanakijiji na wale ambao wanahitaji kuzijua Sera za Chadema zinapatikana HAPA. Vile vile unaweza kufungua attachments zifuatazo zenye Sera za Ulinzi na Utawala na Sera ya Utawala Bora. Nafikiri Sera na Ilani hizi ni toleo la 2005-2010 bado tunasubiri watoe Sera na Ilani ya 2010-2015.

naomba kama unaweza save hii document iweze kufungukka kwenye office XP kwani inafunguka kwenye office 2007 na kuendelea nimeshindwa kuisoma au ibadili kuwa PDF
 
Baada ya ajali ya ndege ya mafunzo na matukio ya hivi karibuni ya ujambazi ambayo yamesababisha mauaji ya watu mbalimbali na vile vile vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mikononi na kuwatia mafuto wanaowatuhumu kuwa ni vibaka kumenifanya nihoji maswali fulani. Nikiangalia vile vile kuvuja na kulega lega kwa idara ya usalama wa taifa na mfumo mzima wa usalama wa taifa sina budi kuhoji Chadema chama ambacho kinataka kushika "madaraka" ya nchi kina sera gani juu ya:

a. Usalama wa Taifa
b. Mfumo wa usalama wa taifa
c. Muundo wa Jeshi la Polisi
d. Na kushughulikia uhalifu mdogo

Najua kwamba wengi hamtaki kujua sera hizo hadi itakapoingia madarakani ndiyo mtataka kujua, miye ningependa kujua sasa.

Unataka ujue ili iweje?u copy and pastena kuboresha kidogo kwa CCJ?
 
Sasa kwa wale wote wapenda mabadiliko na maendeleo ya ya kweli . ebu tu assume kama sisi ndo tumepewa kazi ya kuandiaka sera ya ulinzi na usalama. Kwa manufaa ya vyama vyote na CCM ikiwemo let see mawazo yetu .

Kupunguza idadi ya ukubwa wa JWTZ kwa 15% na kuongeza idadi ya Polisi kwa 15%( Ingawa sijui current idadi)
Kuhakisha JKT/JWTZ inajenga nyumba za wafanyakazi wa KCC japo nyumba 30 kila mwaka kwa mikoa mitano mkikubwa na nyumba 10 kila mwaka kwa mikoa mingine
 
hakuna mtu hatari katika demokrasia kama asiyetaka kuuliza maswali; ni katika utawala wa kiimla tu ndipo maswali hayatakiwi na wote wanatakiwa kujipanga mstari kuitia "ndiyo".

Big thanks MKJJ

.........and this is the bottom-line...........why we are not progressing as a nation...............huku kujifanya watu fulani tu ndio wanatakiwa kujua......kunatu-cost sana............mafisadi/majambazi got and still get away because of these kind of mentality........... (are we brainwashed?).................c'mon guys.............lets ask these politicians what plans they have for our Nation.............
 
r u kidding me? mistari tisa sijui ya "sera ya ulinzi" ni kitu cha kuweza kuonewa gere?

What about advise from Mnyika(the source) is that not enough,if not u can advice them and be part of those make sera :he said the door is open to anybody for anyone with critical thinking instead of kulialia hapa kama mtoto wa kambo.
 
What about advise from Mnyika(the source) is that not enough,if not u can advice them and be part of those make sera :he said the door is open to anybody for anyone with critical thinking instead of kulialia hapa kama mtoto wa kambo.

nani amekuambia tunaishi katika nchi ya kikomunisti ambapo one has to use the "official channels"? kama wewe una mawazo yako yapeleke kwa njia hiyo na mimi nachagua njia yangu alimradi yanafika. Ucha kunilalamikia kama mtoto mtukutu!
 
MKJJ naelewa hali yako uliyonayo kwa sasa si ya kawaida, kuna wengine wamekuambia 'you are wounded', ni muda mwafaka sana kwako kutumia akili ya ziada kui control hali hii vinginevyo unaweza kujikuta unapoteza hata kile kidogo ulichoanza kukijenga.

Kisaikolojia ukiona mtu anakuja na maswali mengi mengi yasiyo na mpangilio tena akiomba apatiwe jibu wakati huo huo jua kuna walakini. Mfano unakutana ghafla na mtu anayekudai na kukuambia anataka hela yake sasa hivi huku akijua fika hakuna uwezekano kwa wakati huo. Mtu wa aina hiyo hata asipopata alichokitaka lakini moyoni atajiridhisha, leo nimemkomoa.

Inawezekana kabisa akawa kati ya makundi ya jamii ifuatayo; amekasirika, amesusa, amezira, anakomoa, anajionyesha, analipiza, anakejeri au anataka shari. Atakuwa anafanya hayo kwa kuwa kuna kitu kimembana rohoni naweza kusema kama pumzi sasa anatafuta pa kupumulia 'mind refreshment'

MKJJ kulazimisha Chadema leo wakuambie mipango ya usalama wa Taifa ni sawa na niliyoyasema hapo juu hata CCM sijui kama watakuambia in short it is impossible. Kwa maoni yako unafikiri Chadema inaweza kukuambia jeshi lao la polisi litakuwa say na polisi wangapi, nafikiri hii ni hasira, unafanya hivi ili Chadema ionekane imeshindwa kujibu useme si unaona hawajui hata wanataka kufanya nini.

Kuhusu uhalifu mdogo mdogo, unataka Chadema wakuambie polisi yao itapambanaje na wamachinga wa mitaani au vibaka wa mifukoni au vijeba wa Tannesco na Deiwaka wa daladala, sioni maswali kama haya yanaleta mantiki yeyote kama si hali ya mtu kuzira au kukomoa.

Mara chache sana sera kutaja kwa idadi sera mara nyingi zinataja asilimia, tutapunguza uhalifu kwa asilimia 10 au tutaongeza bajeti ya elimu toka asilimia 20 ya sasa hadi asilimia 35 nk. Mambo ya mipango sijui ya Usalama wa taifa au polisi huwezi kukuta yameandikwa wazi sehemu yeyote ili kila mtu ayasome.

Mzee Mwanakijiji, nimeanza kwa kungoli kitufe cha 'thanks' kwenye thread hii,sio kwa kukushukuru, bali just kukujulisha nimekusoma, labda mbele ya safari, JF B itaongeza vitufe, ili kiwepo cha 'point noted' sio lazima 'thanks'.

Nilisema hapo nyuma, Mzee Mwanakijiji, you are wounded!. Ukubali usikubali, kupasuka kwa ngoma ya CCJ uliyoipiga sana, kumekuathiri kisaikolojia na kukuumiza.

Ili kuendelea kuonyesha you are still strong, hujaumia, sasa inaibuka na style ya ku hit back, na hapa na hapa target ni Chadema, walikokimbilia hao wa CCJ wengine, ili kuidiscredit Chadema.

Hakuna ubishi kuhusu uwezo wako wa uchambuzi na maono. Hakuna ubishi kuhusu vision yako na insight kwenye baadhi ya issues zenye maslahi kwa taifa, hili la kuanza kuuliza sera za Chadema kwenye national security, sio tuu ni uonevu, bali pia zinaweza kuidiscredit Chadema ionekane security risk, hivyo isichaguliwe.

Mzee Mwanakijiji, mimi binafsi, nakukubali, in fact naadmire sana uwezo wako na nasoma sana makala zako na kutembelea sana 'Mwanakijiji .com', nakuomba sana, kipindi hiki kifupi tumia uwezo wako katika kujenga, sio kubomoa. Silazimishi lazima ujenge Chadema, jenga hata CUF ama endelea kuimarisha CCM kama ulivyokuwa ukifanya kule nyumba kwa makala za kuibeba CCM, but now not at the expense of Chadema, please!.

What about advise from Mnyika(the source) is that not enough,if not u can advice them and be part of those make sera :he said the door is open to anybody for anyone with critical thinking instead of kulialia hapa kama mtoto wa kambo.

....duuhh ..............Kaazi kweli kweli.................
 
nani amekuambia tunaishi katika nchi ya kikomunisti ambapo one has to use the "official channels"? Kama wewe una mawazo yako yapeleke kwa njia hiyo na mimi nachagua njia yangu alimradi yanafika. Ucha kunilalamikia kama mtoto mtukutu!

tehe tehe tehe u real need vacation
 
there u go...thinking u know it all...hahaha! haya kila la kheri na uelewa wako uliokupeleka kushabikia CCJ iliyokuwa haina sera hata moja!
Sio sera tu, haina mwanachama hata mmoja kule Pwani. si unakumbuka msajili wa vyama alivyohangaika kuitafuta ofisi ya CCJ?
 
hii topic ya mkjj ni nzuri sana mbona tunaichakachua?????????
jamani nchi hii ni yetu sote, tutoe maoni ya kujenga.
haya mambo ya kusema tusubili CHADEMA kuwa wata solve matatizo wakipata madaraka sidhani kama mawazo sahihi. wanaoongoza CHADEMA nao ni binadamu na wanamapungufu yao. lakini msukumo wa maendeleo nafikiri hauwezi kutokea kwa wanaoongoza bali kwa wanaoongozwa!

sera, ilani ya uchaguzi nk nk ni kitu kimoja, watakaosimamia ni kitu kingine? hii ni kwa vyama vyote
hapa nafikiri tujadili bila woga mambo yanayotakiwa kwa maendeleo na pia maisha bora kwa watanzania wote. chama kitakachobolesha basi ni manufaa kwa Taifa letu
 
Tukifanya SWOT Analysis,tukitafakari kwa kina tutaona tishio lililopo.Ndani ya Miaka 50 ijayo kuna tishio la kuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe au kuingiliwa kijeshi.Kama vyama vya siaasa na hasa Upinzani vitashindwa katika siasa zake za kuiwajibisha na au ukosefu wa dhamira ya dhati na unafiki katika kukiondoa chama tawala madarakani,kuongezeka kwa Social Delicacy inayosababishwa na Udini na Ukabila uanopandikizwa na umeanza kuwaingia watu,wasomi wengi kuongezeka sambamba na ukosefu wa Ajira pamoja na Ufisadi wa kutisha basi Taifa liko hatarini

Kama demokrasia itafeli,kama watanzania na hasa vijana wengi wanaomaliza Vyuo wataishiwa na uvumilivyu na kujipanga in a very Revolutionary way kuna uwezekanao mkubwa wa kutokea machafuko.The truth is ikitokea social Uprising unadhani vyama vya siasa vitashindwa ku-bandwagon?Je,Usalama wa Taifa unashauri nini katika haya?Sera yetu ya Ulinzi kama Taifa inaweka mechanism gani na inashauri jambo lolote kweli kuhusu hili?

Unless employment conditions change dramatically in parlous youth-bulge states such as Afghanistan, Nigeria, Pakistan, and Yemen, Tanzania,Kenya and DRC these countries will remain ripe for continued instability and state failure

The populations of already parlous youth bulge states-such as Afghanistan, Democratic Republic of Congo (DRC), Ethiopia, Tanzania,Kenya,Nigeria, Pakistan, and Yemen-are projected to remain on rapid-growth trajectories. Pakistan's and Nigeria's populations are each projected to grow by about 55 million people

Mabadiliko ya Tabia nchi,yataathiri hali ya hewa amabyo yanasababisha uchumi wetu unaotegemea kilimo cha mvua,utalii,Uvuvi nk kusababisha Rural-Urban migration kwa Tanzania na mataifa mengine zaidi ya 20,hii inaweza sababisha au kuotesha mbegu za machafuko

Pia kuna uwezekano wa kuibuka sectarian struggle itakayosababishwa na kuibuka makundi ya kiharakati yenye misimao ya Kikristo vs kiisilam.Kutakuwa na uwezekano wa makundi fualani kuonekana yanaminywa,mengine kuambukizwa madhara ya extreme activism from outside the border.Je,tuna sera ya ulinzi ya kucheck haya?

Wenzetu China baada ya vita ya korea 1950-1953,walifunga Mipaka yao,wakajenga misingi ya Taifa lao ndani ya wingu la vita Baridi.Walipeleka viajana wao kusoma nchi za magharibi na mashariki(soveit Union block) kusomea Maswala ya Technology,Ulinzi na Usalama pamoija na kusomesha watu kulingana na mapungufu yaliyo sambamba na mahitaji ya Taifa lao,leo hii tunashuhudia China imeshikilia ukuaji wa double Digit kwenye Uchumi,Leo hii tunashuhudia China ikiwa inaongoza kwa Foreign Reserve kuliko hata Marekani.Sisi usalama wa taifa na sera yetu ya ulinzi inashirikishwa kiakamilifu katika palan kwa hizi weakness tulizoziona? Vision 2025 sera yetu ya ulinzi imeshiriki kuandaa seara hiyo?Nimeandika haraka haraka sana,sorry kwa makosa ya spelling nitarudi.Huu ni mjadala mzuri sana
 
Back
Top Bottom