Sera ya Chadema ya Usalama wa Taifa na Ulinzi ni ipi?

r u guys serious? yaani mnataka kukipa chama nchi na hamjui, hamtaki kujua au hamjali sera zao za usalama na ulinzi? you must be kidding me? Sasa watu waache kuuliza maswali kwa sababu ati wako wounded? Na CCM iliniumiza nini mimi kuuliza maswali kuhusu TAKUKURU, Richmond, Dowans? n.k Sikuwa wounded then, and I'm not now.

Sasa mkina na sera au mkianza kuja na mipango (maana hamna sasa) ya kulinda taifa kwa kutumia mishale na marungu na kuanzisha vikosi vya maninja tuje kushtuka?

You r off hook !!!stop your nonesense WaTz wangapi wanajua sera za usalama za CCM na still wanawapa kura miaka yote so whts wrong kutokujua za chadema? kama unataka kushiriki au kusaidia sera za usalama na ulinzi za chadema just go and help ,if u wanna know u dont look like u wanna know .Luteni has said it all ,u kinda wounded so u come up with your demand and stupid Qs.
I was supporting CJJ but now we here where we are and we need to go forward ,and Chadema is the only choice for now.
 
Mzee Mwanakijiji na wale ambao wanahitaji kuzijua Sera za Chadema zinapatikana HAPA. Vile vile unaweza kufungua attachments zifuatazo zenye Sera za Ulinzi na Utawala na Sera ya Utawala Bora. Nafikiri Sera na Ilani hizi ni toleo la 2005-2010 bado tunasubiri watoe Sera na Ilani ya 2010-2015.
 
Attachments

  • Sera ya Utawala Bora.docx
    14.1 KB · Views: 82
  • Sera za Ulinzi na Utawala.docx
    18.5 KB · Views: 82
Mwanakijiji,
Naona jaribu pia kukubali maoni ya watu wengine kuhusiana na jambo hili. Limekuwa mwiba na watu watadhani uko against Chadema yetu kwa kuwa tu imebeba baadhi ya wanachama wa sisi j. Kitu ambacho kinaonekana kama ndivyo ilivyo maana hukuwahi kuuliza maswali yote haya kabla.

embu search hapa kwa neno Chadema au mada nilizoziasha miaka michache iliyopita utaona. Hakuna swali moja ya ninaloliuliza sasa ambalo sijawahi kuliulia kabla. Kwa kusupport CCJ wengine wanaona kuwa mawazo yangu na hatima ya maono yangu yako kwa CCJ. Sina utii kwa mtu, chama au kundi la watu isipokuwa kwa Tanzania tu.

Najua utasema nilishawahi kuwapa ushauri lakini hawataki, plz elewa chama upokea ushauri mwingi na si lazima ipokee shauri zote zinazoletwa na kuzichukua kama zilivyo. Chama kina haki ya kukataa baadhi ya ushauri.

at their own peril. Na sisi wengine tutaendelea kutoa ushauri ule ule kwa sababu ushauri mzuri hata ukiukataa vipi hauwezi kugeuka kuwa mbaya.

Sipendi kuwaita wale waliohama chama na kuja Chadema kama viongozi wa sisi j maana uongozi wao haukuipeleka sisi j popote. Daima nitawaita tu wanachama wa sisi j wakati ule uliopita. Na kwa kuja Chadema watatakiwa kujenga chama kwa misingi waliyoikuta. Hawatakiwi kulazimisha kwamba ni lazima mawazo yao yakubalike. Lakini wanaruhusa yote kuleta mawazo mazuri kwa ajili ya ujenzi wa Chadema na nchi kwa ujumla wake.

I'm so over nani kaenda wapi na nini.. naamini katika demokrasia na demokrasia haina maadui au marafiki wa kudumu. Binafsi sijali kama CCJ nzima ingejiunga na Chadema au vyama vingine vyote vingejiunga na chadema.

Kwa upande wangu kwa hali ilivyo sasa naona kama haupo kwa ajili/niaba ya sisi m, bado unayo nafasi ya kuijenga hiyo sisi j unayodhani ni bora sana kisera na kimtazamo hadi kwenye kiwango unachodhani ndicho unahitaji na sisi baada ya hapo tutakuja nyuma yako. Na kama unadhani na sisi j haina unachohitaji unaruhusa kujiunga na sisi m na kuwa mpinzani within sisi m ukiwa umejiunga na lile kundi la wakina dkt Mwakyembe na wenzie. Bado una ruhusa.

Na nina ruhusa ya kukosoa chama ambacho kinajionesha kuwa ndiyo mbadala wa kweli wa CCM wakati siyo au hakitaki kweli kuwa. Ninayo ruhusa (nimejipa mwenyewe anyway) ya kuonesha kuwa si hekima kuiachilia nchi ya watu milioni 42 kwa watu ambao wanataka tu kuingia madarakani halafu ndio watuambie mipango yao katika masuala mbalimbali nyeti ya taifa. NItakuwa nina wazimu nikipanda treni la namna hiyo.

Tena ujue ili na sisi tujiunge na chama chako tueleze yooooote unayotuuliza.

Kwani nimewaalika kwenye chama kingine? au umeona ninapigia debe sasa hivi chama kingine baada ya CCJ kupigwa nyundo na msajili.
Otherwise ni watu wachache wataendelea kuwa upande wako na utashusha credibility yako hapa.

Mojawapo ya mikwara ninayoipuuzia ni hii ya "kushusha credibility". Siishi katika sifa au kupata credibility, wengine wanachukua misimamo kwa kuangalia vitu hivyo. Ningekuwa mtu wa kufuata wengine watasemaje au kunifikiria nini nisingechukua misimamo mbalimbali tu. Bora niwe mpweke katika ukweli kuliko na kundi la watu katika uongo. Upweke ni sifa mojawapo ya uhuru wa mtu. Nyinyi endeleeni kuimba "kumbaiya chadema" labda na mimi nitafika huko. Lakini nitafika kwa miguu yangu na fikra zangu siyo kwa kuimba wimbo wa "tuing'oe CCM halafu tutajua cha kufanya". Hapo aisee bado hamjaninasa!

Plz ebu pumzisha akili kidogo maana hata mimi naamini una majeraha hata kama hujaona damu ikitoka.

Ndiyo matatizo hayo... siongozwi na hisia na mimi kama Nyerere CCJ siyo mama yangu hadi niumizwe hivyo. Naona wenye matatizo ni wale wanaonza kuiona Chadema kama mama yao kiasi kwamba mtu kuikosoa ni kama mtu kasema "mama yako ana chongo" japo unajua anayo unaona kama amekutukana.
 
You r off hook !!!stop your nonesense WaTz wangapi wanajua sera za usalama za CCM na still wanawapa kura miaka yote so whts wrong kutokujua za chadema? kama unataka kushiriki au kusaidia sera za usalama na ulinzi za chadema just go and help ,if u wanna know u dont look like u wanna know .Luteni has said it all ,u kinda wounded so u come up with your demand and stupid Qs.
I was supporting CJJ but now we here where we are and we need to go forward ,and Chadema is the only choice for now.

Kwa kutumia matuzi na kejeli za namna hiyo hakufanyi hata kidogo hoja zako kuwa na nguvu kunaonesha tu ni jinsi gani umekubali kufumba macho yako katika imani isiyo na msingi. Inaonesha lakini zaidi ni kuwa unaangalia mambo kutoka katika emotions kuliko kutumia uwezo wa mantiki na kufikiri. Kwa kufanya hivyo unathibitisha tu kuwa tatizo lipo kubwa zaidi na ambalo nimejipa jukumu la kulishinda.
 
Sasa wewe MM,kwanini usisubiri Ilani ya Chadema ya uchaguzi iwekwe hadharani,kwa nini usisubiri wakati wa kampeni uwasikie watazungumzia nini kuhusu sera yao ya Usalama wa Taifa.Kumbuka hata ung'ang'anize vipi huwezi kupata jibu kwa wakati huu mbali na jibu kama kuboresha jeshi liwe la kisasa.kuboresha maisha ya askari polisi ili kuwapa motisha ya kazi n.hayo ndiyo majibu ambayo utayapata ambayo kila chama cha siasa kitakwambia hivyo hivyo.hata mwananchi wa kawaida tu atakuwa na maoni hayo hayo.Usubiri wakati wa kampeni watajieleza kwa kila nyanja,hapo ndipo uulize kama haujaridhika,au kukipa kura chama kikingine ambacho utaridhishwa na sera zao

HIzo ahadi zitakuja 2010 na hazikuwepo kuanzia 1995? Au zimebadilika ndiyo mwaka huu zitakuja? Usichanganye misimamo ya uchaguzi ambayo huja kila wakati wa uchaguzi na maono ya kiuongozi ya kichama. Kuna vitu ambavyo chama kinasimamia kabla hata ya uchaguzi. Ilani siyo sera. Sera hujulikana mapema na msingi wake ni itikadi inayojulikana. Kutokana na hiyo itikadi tunajua sera za chama zilivyo na inapokuja ilani basi inaenda in details sasa kutuelezea mambo ambayo wanataka kuyafanya katika kipindi fulani (usually miaka mitano).

Wakati wewe unasubiri ilani, miye nasubiri sera niielewe halafu ikija ilani nione inavyotakiwa kutekelezwa! senki yu.
 
Nachukulia kuwa maswali unayoelekeza kwa Chadema ni changamoto ili wajipange na kurekebisha mambo ambayo hayajakaa vizuri. Ila unaposubiria majibu ya nyongeza ya Chadema kuhusu sera zao tujulishe sera au dira ya CCM na CCJ inasemaje kwenye vitabu vya chama kuhusu Usalama wa Taifa. Pia ukiwa mtanzania toa mchango wako wa mawazo kwa Chadema yawezekana hawajabobea katika masuala fulani fulani ya kisera labda hili la usalama wa taifa. Nimeona post ya Mnyika akiomba mchango wa mawazo kutoka kwa wanachama na wananchi ukiwemo wewe MM.
 
MKJJ wakati tukiendelea kusubiri kwa hamu mipango ya Chadema ikiwemo Sera ya Usalama wa Taifa naomba nikukumbushe kuwa si wewe tu uliye na mawazo ya nini kifanyike kwa kipindi gani.

Kwenye uchaguzi uliopita wa 2005 endapo Chadema ingefanikiwa kuingia madarakani, Serikali ya CHADEMA iliahidi kufanya yafuatayo kwa kipindi cha mwaka mmoja wa kwanza:

Elimu
  1. Bajeti ya elimu kuongezeka kutoka 18% hadi 35%, kuongeza ajira za waalimu na kuboresha mishahara ya waalimu.
Afya
  1. Kufuta VAT kwenye huduma na vifaa vya kina mama waja wazito na watoto.
  2. Madawa ya kurefusha maisha kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kugawiwa kwa wote walioathirika.
  3. Kupandisha mishahara ya madaktari na wauguzi.
Kilimo
  1. Kufuta kodi zote pamoja na VAT kwa pembejeo za kilimo.
  2. Kuweka mpango thabiti wa kutofautisha ardhi kwa ajili ya umwagiliaji.
Uchumi
  1. Bajeti 2006/07 kupunguza VAT iwe 16%.
  2. Kufanya mapitio ya mikataba yote ya uwekezaji na ubinafsishaji.
  3. Tanzania kujiunga upya na COMESA.
  4. Kutengeneza ajira milioni moja kwa kufanya mabadiliko makubwa katika sekta za madini, utalii, ujenzi na huduma za jamii.
Mfumo wa Utawala Bora
  1. Kurudisha serikalini mali zote zilizochangwa na wananchi na kuhodhiwa na CCM kama viwanja vya mpira na majengo yanayotumiwa na CCM n.k.
  2. Kupiga marufuku uuzaji wa nyumba za Serikali na kurejesha zilizokwisha uzwa kiupendeleo.
  3. Kuvunja PCB na kuweka majukumu yote ya kupigana na rushwa chini ya Mkurugenzi wa makosa ya Jinai (DCI).
  4. Kuboresha maisha ya kina mama kwa kuwawezesha kielimu na kuwapa nafasi katika utawala.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx​
 
This guy call himself Mzee Mwanakijiji is not time war man, You might have nice and good view about something but not in a right time and right place.
So sometime you have to put aside the dream and deal with reality first as the way to make your dream.
This guy has failed with CCJ same thing it was good idea but in reality "Tz politics" other smart guys warned us that it not going to work unless deny reality and go by our dream.The results BOOM!! no CJJ .It ok to try to give a shot anyway .
The problem is what you need is not the right time ,the proble with CCM is not much about sera ni uwajibikaji ,uchungu wa nchi ,na system ya kulindana.Thats why people they need to get rid off CCM .Thats why people dont care much about what you call "sera".
Cause what is a meaning of good sera and no implementation of those sera.
Hakuna sera CCM inayoruhusu kura rushwa but they are god on doing that.CCM inanuka inatakiwa itoke ,ni uchafu unautoa kwanza.
Una uhuru wa kuuliza utishaingoa CCM then what? But it'd be better if you stop such kind of Q,.
 
hakuna mtu hatari katika demokrasia kama asiyetaka kuuliza maswali; ni katika utawala wa kiimla tu ndipo maswali hayatakiwi na wote wanatakiwa kujipanga mstari kuitia "ndiyo".
 
classical Tanzanian mentality!!! mtu akizidiwa hoja anakimbilia "anajifanya anajua sana",.. "ana ringa sana'.. "oo anatamba mno"..

classical 'mjuaje' defence mechanism...generalisation...such a weak stance! I wonder wat research proved WaTz wana similar mentality!

Anyway...let me keep my tanzania mentality (whatever that is)...Alafu kitu kinachonishangaza zaidi...kama kweli hili jambo linakukera, si una personal contacts za watu wa juu wa Chadema? Sasa kinachokufanya ushindwe kuwa-contact na kuamua kuja kumwaga maswali ya ajabu hapa jamvini kwa ajili ya kupumbaza the public ni nini?
For your information, sidhani kama the number one problem tanzania ni ulinzi na usalama wa taifa! Ishu nzima ya ulinzi inaweza kumalizwa bila hata sera specific, bali usimamiaji bora. Unataka kuleta politics za marekani hapa na wakati level ya political matureness ni tofauti! The real problem ni CCM. Na ndi hilo tuna-deal nalo katika uchaguzi huu.
Ivi Sera ya CCJ ya ulinzi ilikuwa ipi? Ivi hata walifikia level ya kuunda sera? Chief objective yao ilikuwa sio kuindoa CCM? Sasa kama ulikuwa mwanachama huko, objective si imebaki pale pale, isipokuwa badiliko la jina la chama?
 
well, kwani haya maswali ni ya siri hivyo hata yasiulizwe hadharani? MBona tumeuliza maswali mengi CCM na viongozi wake kwenye mtandao huu huu na hatukuambiwa kwanini tusifanya mazungumzo nao pembeno kwa sababu tunazo contacts zao? Mnataka tutumie kipimo kimoja kwa CCM na kingine kwa Chadema? kwanini?
 
Mzee Mwanakijiji,
Si lazima uanike kila kitu hadharani. CCM wana tabia ya kuiba sera za wenzao na kukimbia nazo. Malalamiko katika suala la madini hayakuwa sera za CCM lakini hao hao walioowaingiza wachimbaji kwa mikataba mabomu ndio hao hao wanatuambia wanatuletea win win situation. Ningekuwa CHADEMA nisingeanika kila kitu hadharani kwa saa hivi, lakini masuali yako ni valid.
 
mzee nadhani hapa ndipo penye tatizo kwa chadema. Kuna baadhi ya mambo ambayo Chadema ni lazima iyaweke wazi kwa sababu ni tofauti mno na yale ya CCM kiasi kwamba CCM haiwezi kuyakopi au hata kuyaigizia.

Obama kwa mfano, alisema kuwa akiingia madarakani atahakikisha Guantanamo inafungwa kwani ni kinyume na Umarekani. McCain hakuweza kabisa kutaka kufunga Guantanamo kwa sababu kwake lilikuwa ni suala la usalama wa taifa. Tofauti hizi hazikuwa siri bali ni tofauti za msingi. Hata ukija kwenye masuala ya majeshi ya US kule Iraq Obama alikuwa ametofautiana na wagombea wengine kwa kuwa far to the left kuliko wengine.

Sasa tofauti hizi zinasaidia kumfanya mpiga kura kujua upande upi anakubaliana kwa sababu ya tofauti za msingi.

Kwa mfano sera ya CCM ilikuwa ni kupitia mikataba mbalimbali ya madini na kufanya marekebisho ya sheria ya madini na sera ya madini. Kikwete juzi kasema kuwa wamefanya hivyo na makampuni matatu yamekubali kuondoa kipengele fulani cha kodi wakati Barrick inasuasua. Je Chadema imeridhika? Well, kwangu mimi ningependa kwenye madini Chadema ina sera ambayo ni more radical kuliko ya CCM na haiitaji kificho kwa sababu CCM haiwezi kuiiga hata kidogo bali kuipinga lakini itakayopata mashabiki kwa wapiga kura.
 
Mwanakijiji

Ni sawa Chadema inatakiwa iwe critical zaidi kwenye ilani yake kwa sababu CCM haiwezi kuwa critical kwa vile iko madarakani itakuwa inajifunga yenyewe.

Ila elewa ilani ya Chadema inatakiwa iwe offensive wakati ya CCM inatakiwa iwe defensive, ndiyo maana Chadema wanachelea kuitoa mapema hali itabadilika Chadema itakapokuwa madarakani itakuwa inawahi sana kutoa ilani ili kupima upepo wakati huo CCM itakuwa inaficha ilani yake, maswali yako utayageuzia kwa CCM hautaiuliza Chadema utakuwa unaiuliza CCM What Next. So it is just matter of time things will change automatically

Ila wakati mwingine MKJJ unachanganya sana siasa za Tanzania na Marekani, elewa kuwa kwanza Tanzania hatuna tume huru ya uchauzi tofauti na Marekani na uelewa wa watu wetu bado ni mdogo wala hautegemei sana kujua sera au ilani, ni mimi na wewe na wana JF na wachache wengine ndio tunauwezo wa kuyauliza hayo sijui ya What Next au ya mrahaba lakini yule mchimbaji mdogo wa Nyarugusu hajui hilo anachotaka ni kupata kipande cha kuchimba shimo basi.
 
Ila wakati mwingine MKJJ unachanganya sana siasa za Tanzania na Marekani, elewa kuwa kwanza Tanzania hatuna tume huru ya uchauzi tofauti na Marekani

Usiniambie kuwa hili la tume huru ya uchaguzi mmeligundua leo hii? Kati ya vitu ambavyo binafsi sitaki kusikia Chadema wanalalamikia ni hili la tume ya uchaguzi. Mmekubali kucheza mpira kwenye uwanja wao, sheria zao na refa zao na hata washangiliaji wao basi hamna haki ya kulalamikia matokeo yake.

na uelewa wa watu wetu bado ni mdogo wala hautegemei sana kujua sera au ilani, ni mimi na wewe na wana JF na wachache wengine ndio tunauwezo wa kuyauliza hayo sijui ya What Next au ya mrahaba lakini yule mchimbaji mdogo wa Nyarugusu hajui hilo anachotaka ni kupata kipande cha kuchimba shimo basi.

Jamani acheni kuwatukana Watanzania hivi. Hawa waliosimama na kukimbia mchakamchaka kutaka kumchagua Mrema mwaka 1995 na kupira kura karibu milioni 3 hawakuwa na cell phones wala internet walikuwa na uelewa gani? Kama watu wetu "wana uelewa mdogo" kwanini mnataka kuwaomba kura, watawaelewa kweli?
 
kwa hiyo mnataka tuwape nchini chama ambacho hatujui sera yake kuhusu national security. My position ni kuwa it has to be stronger and more articulate kuliko ya CCM, would you agree? au tuwape tu uongozi wa nchi watajua mbele ya safari kama wengine wanavyotaka iwe? Au tuamini tu kuwa wanayo hata kama hatujui kama wanayo au kutuambia japo kwa juu juu ikoje?

Kwani hili linakupa tena wasiwasi? Kama chadema hawana hizo sera si tayari zipo za ccj ambao wameshaingia ndani? au kabrasha lote ulibaki nalo wewe na kina kyb hawana riksa?
 
well, kwani haya maswali ni ya siri hivyo hata yasiulizwe hadharani? MBona tumeuliza maswali mengi CCM na viongozi wake kwenye mtandao huu huu na hatukuambiwa kwanini tusifanya mazungumzo nao pembeno kwa sababu tunazo contacts zao? Mnataka tutumie kipimo kimoja kwa CCM na kingine kwa Chadema? kwanini?

Hapana....mimi sijasema kuwa tusitumie kipimo kimoja kwa CCM na Chadema. Lakini ningependa kuuliza...ni kipimo gani utakachotumia ambacho kitapima hivi vyama viwili fairly? Kumbuka, chama kimoja kimeongoza nchi miaka 40 na kingine ndo kwanza kina wabunge sijui 6 tu! What is a fair test between the two? Cant one agrue that, it will only be fair if Chadema was given the same power and responsibilities, and only then we will be able to see which party was the best?
Pili...nadhani Mnyika (mtu aliye ndani ya Chama) amekujibu vizuri kwenye ile thread nyingine. link hii hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/67023-yah-kuunga-mkono-chadema-kwa-sasa-7.html. Check post #124. Chadema haijatoa nakala yake ya ilani ya uchaguzi, na wamekaribisha maoni ya wote. Ivyo...nadhani discussion ingekuwa na manufaa zaidi kama inge-base katika kutoa maoni badala ya ku-question? Pale ambapo Chadema itatoa ilani yake, na wewe kupingana nayo, basi utakuwa umefanya hilo in the fairest manner. Na chadema kukosa kura yako itakuwa fair. Lakini kudai sera kabla hawajatoa, na wakiwa wamekaribisha maoni...hiyo sio busara! Ama sivyo tutaendelea kukesha hapa tukijibizana na kuitana majina. Ivyo ni bora thread igeuke kuwa proposal yako to Chadema.

P.S. Mfano wako wa shamba ulitoa kule kwingine nao una shida fulani. Mimi binafsi sioni tatizo la ku-clear shamba tayari kwa kupanda. Cha kupanda kitakuwa ni maamuzi ya wote, kitu ambacho ni tofauti kwa sasa, ambapo cha kupanda ni maamuzi ya mafisadi! Na kama watatugeuka, sidhani kama itakuwa impossible kuwatoa wa wao maana precedent itakuwa imeshatolewa and it will be easy to follow.
 
Kikwete juzi kasema kuwa wamefanya hivyo na makampuni matatu yamekubali kuondoa kipengele fulani cha kodi wakati Barrick inasuasua. .
Mzee Mwakijiji, hili ni kiini macho!. Sheria mpya ya madini imetamka bayana makampuni ya madini yatalipa kodi. Katika hotuba ya bajeti ya mwaka huu wa fedha, Waziri wa fedha alionyesha taifa litapata kiasi kadhaa cha mapato kutokana na kodi za madini, halafu kwenye bajeti hiyo hiyo, Mkulo akoweka nyongeza kwenye kiambatisho A kuwa kodi itakayotozwa kwenye makampuni ya madini, itatozwa kuanzia kwa makampuni yatakayingia nchini baada ya kuwekwa kwa sheria mpya, hii ikimaanisha ile mikataba ya zamani itaendelea kuheshimika na kutekelezwa kwa mujibu wa makubaliano yale yale ya zamani.

Nimeita hii kama kiini macho kwa sababu makampuni yaliyopo, yataendelea kujivunia madini yetu kwa mikataba ile ile ya zamani, na by the time mikataba imemaliziki, madini nayo yamekwisha, labda kama hayo makampuni mapya yatakuja na ugunduzi mpya wa minerals deposits.

Rais kweli kasema makampuni matatu yalishakubali kuanza kulipa kodi tangu 1st July, 2010. Barrick akagoma kwa valid arguments za kisheria, kuwa mikataba yao ni halali na haiwezi kubadilishwa labda ivunjwe, na kuwa sheria ya madini, haiwezi ku-act retrorespective ya mikataba ya awali, any retrorerespective law is a bad law, arguments zikakubalika, Barrick wakakubaliwa, ndipo na waliokubali kulipa, wakaiandikia serikali kuwa hawawezi kukubali double standards, ama walipe wote, na kama Barick halipi, basi wasilipe wote. Serikali ikakubali wasilipe wote, sasa hizi ahadi za JK kuwa watalipa ni sehemu tuu ya kutafutia kura October, kwenye madini, tumeliwa na tunaendelea kuliwa!.
 
Kimsingi mwanakijiji nakubaliana na wewe lakini fanya kitu pale kinapohitajika. Hebu rudi nyuma kwenye sera ya majimbo ya chadema... imekuwaje na imewachafuaje? nafikiri unajua. Life style yetu bado haiko katika utayari wa kusikia sera.... Hivi utazibadika tu hapa then 19k membas wa JF ndo wasome tu? Hakika CCM ikaondoka, tukaanza kutumia kila aina ya mawasiliano kuhusu sera hakika tutaeleweka na kufikisha pale tunapotaka but kwa style hii ya KUTOAMINIANA ambako ndo tatizo la msingi letu hapa bora kuanza juu kuja chini kuliko kusubiri chini kuja juu. Utaliwa tu.......Ninaomba CHADEMA tukubali kuwa CCM wamejenga tabaka la kutoaminiana na hili ndo linaturudisha back.
 
Back
Top Bottom