Sera hii itatumaliza.

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Ubinafsishaji.Ni neno zuri,lilobuniwa katika utaalamu wa kifisadi.Kwangu mimi lakini, hakuna tofauti ya ubinafsishaji na wizi wa hila,ambao ni wizi tuu.Kwa bahati mbaya viongozi wetu wamekubali tuibiwe.Kama ni katika hali ya kujua au kutojua sina hakika,lakini ukweli unabaki palepale,tunaibiwa.Wizi huu siku hizi za karibuni umekuja na wazo geni kidogo,'Biofuel Project'.Kama kawaida yetu sidhani kama viongozi wetu wana ubavu wa kukataa wazo hilo.Lakini naomba nitoe angalizo mapema kwa serikali yetu.Wezi hawa wanaokuja kuchukua maeneo makubwa hapa kwetu, walishafanya hivyo kwingineko na Ulaya kwenyewe.Walipochukua maeneo ya wananchi hawa maskini,wanachi wale walikimbilia mijini kutafuta kazi.Kwa bahati nzuri wenzetu tayari walikuwa na viwanda,kwahiyo wananchi wale waliajiriwa viwandani.Ni vizuri kujiuliza,sisi leo wananchi wetu tutawapeleka wapi?Jibu ni kwmba hakuna,kwa vile hatuna viwanda vya kutosha.Kwa hiyo wananchi wetu wataishia kuwa watumwa na omba omba kwenye mashamba na viwanda vya wakubwa hao.Ushauri wangu siku zote ni kwamba tunazo rasilimali za kutosha.Kama hizi zikitumiwa vizuri tunao uwezo wa kuwa na maendeleo yaliyo 'more rational' kuliko ilivyo sasa.
 
Back
Top Bottom